Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Hili jukumu nakuomba ulifanye wewe, mimi napita katika mapito yangu, kisha tutakuja kuulizana maswali, ili tuone nani mkweli katika hili.

Hakuna shida Boss, Cha Muhimu Reference tuwe tunaweka.
 
Hakuna shida Boss, Cha Muhimu Reference tuwe tunaweka.
Safi kabisa, mimi kama nilivyo tangulia katika utangulizi wangu hapo, ni kuwa haya ninayo andika au nitakayo yaandika siyo mapya bali nanukuu toka kwa wakubwa zangu, na mwisho nitaweka marejeo ya vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimenishibisha juu ya historia ya watu hawa.
 
Safi kabisa, mimi kama nilivyo tangulia katika utangulizi wangu hapo, ni kuwa haya ninayo andika au nitakayo yaandika siyo mapya bali nanukuu toka kwa wakubwa zangu, na mwisho nitaweka marejeo ya vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimenishibisha juu ya historia ya watu hawa.

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Hapo kuna Masuala mawili tayari yamejitokeza

1. "Nukuu toka kwa Wakubwa Zangu" hapa lazima watakua wanazuoni wa Ki-Islamu
2. " Mrejesho wa vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimeshibisha historia ya hao watu"....natarajia hivyo vitabu viwe Quran na Hadithi

Nway hilo suala nimekisia tu, nangojea hoja zako Boss.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Hapo kuna Masuala mawili tayari yamejitokeza

1. "Nukuu toka kwa Wakubwa Zangu" hapa lazima watakua wanazuoni wa Ki-Islamu
2. " Mrejesho wa vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimeshibisha historia ya hao watu"....natarajia hivyo vitabu viwe Quran na Hadithi

Nway hilo suala nimekisia tu, nangojea hoja zako Boss.
Sahihi kabisa, kama ambavyo wewe umerejea katika Biblia, na mimi marejeo yangu ni huko huko, ila tutakuja kuachana katika kujibu maswali na kujenga hoja, sababu ukweli ni mmoja tu siku zote.
 
WAYAHUDI wanajinasibisha na NABII MUSA kwa Mantiki ya kwamba Wao ni Muendelezo wa Uzao wa Kabila la YUDA(Ref Biblia Kitabu Cha MWANZO 29:35),
Unaweza kunipa ushahidi ya kuwa uzao wa Yahuudha (Yuda) upo mpaka leo ? Ili kauli yako iwe na nguvu ya kuwa Uyahudi ni muendelezo wa uzao wa Yahuudha ?

Pili, je ni lini Uyahudi ulikuwepo au ulianza kuwepo, je kipindi cha Musa Uyahudi ulikuwepo ?
Na YUDA alikua ni Mmoja kati ya Watoto Kumi na Wawili wa Uzao wa YAKOBO(ISRAEL), Katika hao Watoto 12 wa YAKOBO mmoja wao Aliitwa LEVI( Ref Biblia kitabu cha MWANZO29:34)
Hili nakubaliana na wewe bila shaka yoyote.
Na Huyu AMRAM ndo Baba Mzazi wa NABII MUSA.....Kwahiyo Ukiangalia hii Family Lineage utaona WAYAHUDI na NABII MUSSA Ulikua Muendelezo wa Uzao wa YAKOBO( ISRAEL)
Nacho taka hapa unithibitishie ya kuwa kipindi cha Musa Uyahudi ilikuwepo, maana hii ni dini, na tunajua Musa hakuwa Myahudi kwa dini.
Katika BIBLIA YA KIEBRANIA MUNGU amejitanabaisha kua ni MMOJA kwa Mantiki hii

KITABU CHA KUTOKA20:2-3 inasema "Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Usiwe na miungu mingine ila mimi".......Ukiangalia hapa MUNGU katua Neno "MIMI" kuashiria ni MMOJA.
Hapa unawaongelea wana wa Israeli,yaani Kuamu ya Musa,na ai Wayahudi kama dini. Inabidi tuelewane uzuri hapa.
 
Kuhusu Torati kwa Mujibu wa Dini ya UYAHUDI ni Mjumuiko wa Vitabu Vitano Vya Mwanzo katika BIBLIA YA KIYAHUDI vinavyeleza MAFUNDISHO, MWONGOZO na SHERIA kwa Wana Wa ISRAEL, Na hii Torati Iliandaliwa na MUSSA kwa Maono Ya MUNGU WA ISRAEL...Kwahiyo Kwa Mantiki hii WAYAHUDI Moja kwa Moja Lazima wajinasibishe na TORATI ya MUSSA.
Safi kabisa, je kila myahudi ni wa ukoo wa Israeli ?

Je kuna sehemu yoyote inayo sema ya kuwa Musa alitumwa kwa Wayahudi au Musa alitumwa kwa Wana Wa Israeli ?
KUMBUKUMBU LA TORATI 4:39 inasema "Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. "

Kuna mistari mingine Mingi sana Inayooneshwa katika BIBILIA YA KIEBRANIA KUWA NI MMOJA....Unaweza pitia Na Hii...KUMBUKU LATORATI 6:4, 2
Bila shaka haya umeyatoa katika Biblia na si katika vitabu vya Wayahudi, sasa ni kipi kinachokujulisha haya yanawakusudia Wayahudi na si Wana wa Israeli ?
 
Pia Tukiangalia kwenye KURAN Utaona kuna Mkanganyiko Kidogo Kuhusu Wana wa Israel kuabudu MUNGU MMOJA Mfano Ukiangalia
SURAH AT-TAWBA 9:30 inasema wana wa Israel wanasema kua UZAIR ni Mwana Wa Mungu na Wanamuabudu.....Lakini pia kwene KURAN pia kuna Mistari Inasema Wana wa Israel waliabudu katika Mungu Mmoja.

Hiyo aya haiwataji "Wana wa Israeli" aya inawataja "Mayahudi",Qur'aan haijawahi kujichanganya hata kidogo, mnaojichanganya ni nyinyi, anasema Allah aliye juu :

9_30.gif

30. Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa! (at-Tawbah : 30)

Ukisoma katika Tafsiri "at Tankir" ya Ibn Ashuri au Tafsiri ya Ibn Kathiri utaona ya kuwa walio kuwa wanaongelewa hapo ni kikundi cha Mayahudi wanne walio enda kwa mtume ndiyo walikuwa wana dai ya kuwa Uzair ni mwana wa Mungu na kadhalika kikundi kingine cha Mayahudi wa al Isfahani walikuwa wana dai hilo. Mara nyingi aya katika Qur'aan zilikuwa zinashuka kwa sababu maalumu.
 
Sehemu ya pili

Hakika ni ngumu sana kuwazungumzia Wayahudi pasi na kumzungumzia nabii Yakub na ndiyo maana hili likawa vazi lao la kujipamba na kujinasibu na ukoo wake, hali ya kuwa ukweli ni kwamba wako mbali nao,kama tutakavyo lionyesha hili huko mbeleni.

Tunapo lizungumzia tamko "Israeli/Israili" basi huyo ni Yakub mtoto wa Is'haaq mtoto wa nabii Ibrahiim. Yakub aliishi Palestina, pale ambapo babu yake aliishi, lakini walikuwa wana hama hama katika maeneo tofauti tofauti ndani ya Palestina. Kwa jina hili la "Israeli" ndiyo linalo tumika kuwanasibu "Wana wa Israeli au Ukoo wa Israeli (Banu Israili).

Kupitia hili, sasa ndipo tunaanza kuielezea historia ya Uyahudi kutokea kwa nabii Yakub na mpaka walipoingia katika ardhi ya Misri.

Safari ya nabii Yakubu kuelekea Misri.
Nabii Yakub alianza safari hii akiwa na watu wake wa karibu pamoja na watoto wake kuelekea Misri baada ya wito wa mtoto wake kipenzi nabii Yusuf (Hapa kuna historia ndefu kiasi ya ilikuwaje nabii Yusuf akafika Misri, ila kwa ufupi alienda kule kama mtumwa lakini Mola akampa utukufu na kuaminiwa na mmoja wa viongozi na akaja kuwa kiongozi). Hili lilifanyika baada ya nabii Yusuf kumakinika huko Misri.

Wayahudi katika vitabu vyao wanasema ya kuwa, kipindi nabii Yakub anaingia katika ardhi ya Misri jumla yao walikuwa ni watu sabini na wote walikuwa ni waumini. Wakaishi humo maisha mazuri mno yenye kutajika, lakini baada ya kufariki nabii Yusuf, hali ikabidilika na kuanza kuishi kwa dhiki na mateso yasiyo na kifani chini ya utawala wa kifirauni.

Mateso haya yalikuwa yakifanywa na "Faraina/Firauni", hili ni jina maalumu kwa ajili ya Watawala wa Misri kwa wakati huo. Mateso kwa wana wa Israeli yalikuwa makali mpaka ikafikia hatua watoto wa kiume wanao zaliwa na wana wa Israeli wanauliwa na watoto wa kike wakiachwa hai, huu ni miongoni mwa ufisadi mkubwa sana kufanywa katika uso wa ardhi. Hali hii ya dhiki na mateso kwa wana wa Israeli ilienda kwa kitambo kirefu sana mpaka alipokuja nabii Musa. Nabii Musa akawa anawafundisha watu imani ya kweli na kuwausia juu ya subira (Hii ni baada ya Wana wa Israeli kuishi katika dhiki, ikawafanya wachupe mipaka na kuanza kumuasi Mola wao) na kuwakemea juu ya kuwaabudu watu na nafsi zao. Hali ya mateso kwa Wana wa Israeli ikaondoka na waka amriwa na nabii Musa kuondoka katika ardhi ile ya Musa, na hii ni desturi ya Mola wetu muumba katika kuwatakia kheri waja wake, huwa ana waamuru waondoke katika ardhi ambayo wanaishi kwa dhiki.

Lakini mafirauni wakaanza kupata majanga, matufani, dhiki na mabalaa na umwagaji wa damu ukakithiri lakini kwa haya yote Mafirauni hawakutanabahi kwayo basi wakawa wanaleta kiburi na kujiona,na Mola wetu mlezi akamfunulia nabii Musa ya kuwa awaamuru wana wa Israeli watoke katika ardhi ile.

Baada ya hapa, tutakuja kuangalia katika sehemu ya tatu, ilikuwaje safari yao ya wao kutoka Misri.

Itaendelea....
 
Tofauti na Mahindu na Mabudha hawa hawajinasibishi na mtume yeyote ila Mayahudi wanajinasibisha na nabii Musa hali ya kuwa hawana uhusiano wowote na nabii Musa,hili nitalithibitisha huko mbeleni panapo majaliwa.
Hapa tayari uongo hapo
 
Maana ya Uyahudi kiistillahi: Ni kundi la watu wanaofata utamaduni na Mila za Dini ya Kiyahudi ambao asili yao ni waebrania wa kizazi Cha Israel hata Abrahamu.

Na UYAHUDI ni Dini inayo amini katika Mungu mmoja aliyejidhihirisha kwa Abrahamu, Mussa na Manabii wengine wa Kiebrania.


Kuwaelezea Wayahudi na Kuja na Hoja nzuri na zakueleweka inatakiwa urejee Vitu hivi

1. Biblia ya kiebrania
2. Biblia ya Wafuasi wa Kristo
3. Ushahidi wa Akiolojia(Archeological eveidence) wa mambo ya kale hapo mashariki ya kati na Historia
4. Talmud ya wayahudi
5. Kuran na Hadithi za wafuasi wa Dini ya Uislamu
Hapo nimekuelewa
 
Safi kabisa, sasa vipi Wayahudi wanajinasibisha na nabii Musa huku wakidai wanafata Torati ?

Swali lingine la msingi, sababu Historia imeshaandika, na dhuria ya wana wa Israeli inajulikana, je ni uzao gani au ni nani katika wana wa Israeli walikuwa ni Mayahudi ?

Unaweza kulithibitisha hili ? Naomba ushahidi wa hili.
Soma biblia kitabu cha Nabii Samweli hata kutoka pia
 
Ukweli ni upi kaka mkubwa.
Ukweli ni huu Wayahudi ni watoto wa kabila la Yuda. Yuda ni miongoni mwa watoto 12 za Mzee Yakobo jina lingine Israel. Musa ni Mtoto wa ukoo huo huo wa Israel ila yeye ametoka kabila Lawi. Lawi ni miongoni mwa watoto hao 12 pia. Sasa ukisema Wayahudi hawana uhusiano na Musa huoni hapo tayari ni uongo?
 
Ukweli ni huu Wayahudi ni watoto wa kabila la Yuda. Yuda ni miongoni mwa watoto 12 za Mzee Yakobo jina lingine Israel. Musa ni Mtoto wa ukoo huo huo wa Israel ila yeye ametoka kabila Lawi. Lawi ni miongoni mwa watoto hao 12 pia. Sasa ukisema Wayahudi hawana uhusiano na Musa huoni hapo tayari ni uongo?
Uyahudi ni ukoo au ni dini ?

Je kuna kitabu chochote kabla ya Musa au kipindi cha Musa kimetaja jina la "Uyahudi"hata katika vitabu vyao wenyewe Mayahudi ?
 
Unaweza kutuwekea hapa hayo maandiko ili tusome wote.
Bila shaka kwa sio tuliosoma biblia mwanzo mwisho historia ya Adamu hadi Yesu. Huwa ipo wazi kabisa na maandiko yake yapo ndio maana nlikupa vitabu hivo uvisome kama mtafiti halafu ulete marejeo.

Na kama ni kukuandika humu mistari tutachoshana tu Soma vitabu vyote hivo utaelewa Chimbuko la Hilo kabilà
 
Uyahudi ni ukoo au ni dini ?

Je kuna kitabu chochote kabla ya Musa au kipindi cha Musa kimetaja jina la "Uyahudi"hata katika vitabu vyao wenyewe Mayahudi ?

Ukisema Uyahudi ni sawa useme Umasai au Uchagha Ila wayahudi ni kabila na ni ukoo wa Wayuda. 2.Ndio Vitabu vyote vya Musa vimetaja jina La kabila la Yuda.
 
Bila shaka kwa sio tuliosoma biblia mwanzo mwisho historia ya Adamu hadi Yesu. Huwa ipo wazi kabisa na maandiko yake yapo ndio maana nlikupa vitabu hivo uvisome kama mtafiti halafu ulete marejeo.

Na kama ni kukuandika humu mistari tutachoshana tu Soma vitabu vyote hivo utaelewa Chimbuko la Hilo kabilà
Naona hujaelewa suala la mjadala likoje, mwenzako nimeona huko juu ana fata adabu za mjadala, anaweka na vifungu.
 
Ukisema Uyahudi ni sawa useme Umasai au Uchagha Ila wayahudi ni kabila na ni ukoo wa Wayuda. 2.Ndio Vitabu vyote vya Musa vimetaja jina La kabila la Yuda.
Tupe andiko linalosema Uyahudi ni kabila au ni mila fulani.

Siongelei jina la Yuda na ongelea tamko Uyahudi, sababu uyahudi unaingia katika sifa na si jina la mtu.
 
Back
Top Bottom