Kuyaona mawazo yetu kama 'Kelele' ni kutudharau Watanzania

Kuyaona mawazo yetu kama 'Kelele' ni kutudharau Watanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Tulipoamua kupandisha Tozo za Miamala tulikuwa tuna lengo zuri tu ila tulipoanza kusikia Kelele za Wananchi basi Serikali tukaona kwakuwa tunawajali Wananchi wetu tuingilie kati na sasa nimeunda Kamati ili kuliangalia hili na itakuja na majibu muda si mrefu" Rais Samia.

Hasira yangu na Uchungu wangu zaidi haipo katika Kauli nzima bali ni hilo neno tu la 'Kelele' ambalo Mimi nalitafsiri kama vile Rais 'ametudharau' mno na kwamba anataka Watanzania tuwe ni Watu wa kukubali tu kila Kitu ambacho Serikali inaamua.

Kama ni kweli Mheshimiwa Rais Samia alilisema hili neno la 'Kelele' kama alivyonukuliwa popote pale alipo ajue kuwa binafsi 'amenikera' japo huenda Watanzania wengi wakawa 'wameridhika' nalo.

Watu wa Mkoa wa Mara (Musoma) ambao ndiyo 'Mashujaa' wa nchi hii ya Tanzania kuambiwa tuna 'Kelele' ni Kosa Kubwa mno na Dharau japo kwa Watu Washamba wao neno hili huenda wakalifurahia zaidi.

 
Mkuu kwani Morogoro ziarani lile neno la 'mmesikia kelele za kupanda kwa bei ya mafuta......' hukulisikia? Hata hilo la katiba neno 'chokochoko' kwa wenye nchi wanapodai njia bora zaidi ya kuendesha nchi yao halikupi shida?
Nikiwa kama mwana Mkoa wa Mara ( Musoma ) hili neno la Kuambiwa tuna 'Kelele' tena na Mwanamke limeniumiza na kunipandisha sana Hasira zangu za 'Kichuri' Mkuu.
 
Wewew mwenyewe hapa umepiga kelele tu aliyekuambia watu mara ndio mashujaa nani? yani unajikunja unaandika utumbo kama huu wa kutaja makabila ya watu negatively? Halafu ndio utegemee jamii iwatumie watu kama wewe na ulevi huu kuwa na mipango mizuri?
 
Neno sahihi ambalo lingetumika badala ya kelele ni "malalamiko". Kelele ni sauti ambazo hazina mpangilio na mara nyingi ni za kupuuzwa.
Kwahiyo leo hii Rais Samia Suluhu Hassan anatuambia Sisi Great Thinkers na Invisible Think Tanks wa Tanzania yake hii anayoiongoza akina GENTAMYCINE kuwa ni wapiga 'Kelele' kwa Maamuzi yake na Serikali yake? Yaani nimekereka kupita Maelezo.
 
Tanzania hakuna Rais
Naanza sasa Kumkumbuka Hayati Rais Dkt. Magufuli kwani sikumbuki kama nae japo alikuwa ni Mkali ila alikuwa na Kauli za 'Kidharau' kama hizi za Sisi Watanzania tunaolalamika kuitwa Wapiga 'Kelele' kiukweli nimeumia mno kama kweli Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jana alisema hivyo.
 
Back
Top Bottom