Kuzaa au Kutozaa: Lazima kila Mwanamke awe na Mtoto?

Last_Joker

Senior Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
174
Reaction score
261
Katika jamii nyingi za Kiafrika, kuna mtazamo uliojengeka kwamba mwanamke ni lazima azalie watoto ili awe "kamili" au awe amekamilisha wajibu wake kwa familia na jamii. Lakini hivi kweli tunapaswa kufikiria hivyo? Mbona kuna wanawake wanaoamua kwa hiari yao kutopata watoto, wakisisitiza kuwa maisha yana maana zaidi ya kulea familia? Na je, uamuzi huo ni wa kuonekana kuwa ni uasi wa tamaduni zetu au ni jambo la kawaida kabisa?

Kwa upande mmoja, kuna watu wanaoamini kuwa jukumu la mwanamke lina mizizi katika kuzaliana na kulea kizazi kijacho. Hii ni sehemu ya utamaduni na mfumo wa jamii nyingi – wanawake wamekuwa wakihimizwa tangu zamani kulenga katika familia, kutunza watoto, na kuendeleza ukoo. Hii inachukuliwa kama sehemu ya urithi wa kiutamaduni na vilevile usalama wa jamii. Sasa, pale mwanamke anapoamua kutozaa, mara nyingi anakutana na maswali, shinikizo, na wakati mwingine lawama kutoka kwa familia na jamii kwa jumla. Inachukuliwa kama "kukwepa" wajibu au "kutoroka" majukumu yake kwa jamii.

Lakini upande mwingine wa sarafu ni kuwa, kuna wanawake wanaochagua kutozaa kwa sababu zao binafsi, zikiwemo kupenda uhuru, kutaka kujikita zaidi kwenye kazi au malengo yao binafsi, au hata kwa sababu za afya au kifedha. Kwao, kuzaa si lazima – ni chaguo. Wanajiuliza, hivi, kama wanaume hawakosolewi wanapochagua kutopata watoto, kwa nini mwanamke achunguzwe kwa kila hatua anayochukua kuhusu mwili na maisha yake? Pia, wanaamini kuwa mtu hawezi kuwa mzazi bora kama hataki kwa hiari, na kuna vitu vingi vya kufanya ambavyo pia vinaweza kuchangia jamii, si lazima kwa kuzaa tu.

Jamii zinapaswa kuelewa kuwa si kila mwanamke anayeamua kutopata watoto anakosea au "kupoteza mwelekeo." Badala yake, tunaweza kuunga mkono wanawake hao na kuacha kuwashinikiza. Uamuzi wa kuzaa au kutozaa unapaswa kuwa wa mtu binafsi, si wa jamii. Tunaweza kujadili pamoja kama hivi vyote ni sehemu ya uhuru wa mwanamke au ni kujinasua kutoka kwenye utamaduni wa zamani. Hivyo, je, ni lazima kila mwanamke awe na mtoto? Au ni wakati tufikirie upya jinsi tunavyoona wajibu wa mwanamke katika jamii yetu?
 
I tend to agree with you.. Kweli tunawapa pressure kubwa ya kijamii wanawake au wanaume ambao pengine kwa sababu moja au nyingine wana amua kutokuwa na watoto.
 
Inategemea na jamii husika. Katika makabila yetu mengi mwanamke (hata mwanaume) asiye na mtoto anaonekana kama hajakamilika. Hata mazishi yake akifa yanakuwa tofauti.

Wanyantuzu kule, kwa mfano, mwanaume ukifa bila mtoto kaburi lako haliwekewi alama yo yote. Ni kama vile hawataki utambulike maana hakuna hata mtu atakayekuja "kukusalimia". Mwanamke hali kadhalika. Anakuwa hana heshima yo yote.

Kwa wazungu huko mambo ni tofauti kidogo maana jamii zao nyingi zina mitazamo tofauti kidogo kuhusu maisha, wajibu wa mwanajamii; na kutokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii hawaoni hata faida sana ya kuwa na mtoto.

Hapa kwetu nawafahamu feminists wengi (halisi na wale uchwara) lakini wote wana mategemeo ya kuzaa hata kama hawapendi kuwa chini ya mikatale ya wanaume; na ni wasimbe tu kwa sasa.

Jamii zetu nyingi bado zinachukulia kuwa na mtoto kama kikamilisho muhimu na halisi cha maisha ya mwanajamii (me na ke). Na kwa vile mifumo yetu ya maisha inabadilika kwa kasi, miaka michache tu huko mbele ya safari naamini haitakuwa lazima kuwa na mtoto; na jamii haitatokwa na povu la dharau na condemnation kwa mhusika.
 
Kwani alikuja duniani kufanya nini? zaliwa, zaa ili unapoondoka duniani uache uzao wako, maana hata hao waliokuzaa wangekuwa na mawazo kama haya Tanzania tusingefika milion 60, na ukiangalia sababu kuu ya kukataa kuzaa ni ufuska tu hakuna sababu nyingine yenye mashiko
 
Kuishi kwa kutegemea maoni ya wanajamii...it costs
 
Sasa ukifa unaacha nini hapa duniani?

Wewe ni mkatili sababu hutaki kuendeleza kizazi cha ukoo wako, lazima uzae ili uendelee genesis ya ukoo wako wazee wako wamekuachia wewe uendeleze kizazi halafu unaleta mambo ya kutaka uhuru!

Acha usaliti wa ukoo wenu
 
Kwani lazima kuacha genesis za ukoo wako... ukatili ni kuleta kiumbe katika dunia hii yenye mabalaa Kila uchwao
 
Hizi zote ni Heka Heka za Ujana.

Usipokuwa na Miongozo sahihi Ujana Unakufanya Ufikilie kila jambo kwanini Lipo ivyo kwanini nisilibadilishe. Na hata ukiambiwa Hekima yake utaona ni Hadithi tuu.

Lakini Utakapofika Umri furani(Uzee) Ndio utajua umuhimu wa Kuwa na Mwenza wako Na kuwa na Watoto tena sio watoto bali ni watoto wengi.

Lakini Katika huo umri wa ujana Umri wa Nguvu na Ufanisi Utaona Unaweza kuishi mwenyewe ukafurahia Uhuru wako kumbe ni kwa Sababu Una Pilika Nyingi zimekuzunguka Hivyo hauoni haja ya Kuwa Na Familia imara.

Katika Umri wa Ujana Wapo Vijana hufikiria kubadili Jinsia zao Lakini Bila Shaka Majuto ni Makuu watakapofika Uzee (Bora hata Wasifike huo Uzee)

Limit akili yako katika mambo ya Kijamii kwani Hizi Tamaduni na Desturi za Jamii Zimepitia Vipindi (phase) Nyingi sana hadi Zinapatikana Standard Cultures Usidhani Ilitokea tuu from no where Watu wakawekeana Sheria Furani au Tamaduni furani katika jamii zao.

Walipitia Miaka mingi ya Kuangalia mazingira yalivyo na mwisho kuja na Best Solutions ambazo leo hii sisi tunataka ku challenge kila kitu na kupinga huku tukiwa hatuna cha mbadala wa kuweka Mambo yawe Vizuri zaidi.

Jiulize;
Kila Mtu awe Huru kubadili Jinsia yake.

Kila Mtu awe huru Kufunga kizazi kama hataki kuzaa.

Kila mwanamke awe huru kutoa mimba kama haitaki.

Awe huru Kufanya chochote juu ya mwili wake hata kama ni Umalaya.

Kusiwepo wa Kumuongoza mwenzake kati ya Mume na Mke yaani Haki sawa.

Mzazi Asiwe na Haki ya Kumuadhibu Mtoto wake wala kumkaripia kisingizio Child Abuse under child Rights.

Jee katika hayo yote Tunaenda kuipata Jamii bora kuliko jamii za Zamani au tunaenda kuangamiza Hiki Kizazi??

Ni nani atadhubutu kusema kuwa Kupitia haya Tunaenda Kuipata Jamii imara jamii Timamu Jamii yenye Mwelekeo??
 
Hizi Tamaduni na Desturi za Jamii Zimepitia Vipindi (phase) Nyingi sana hadi Zinapatikana Standard Cultures Usidhani Ilitokea tuu from no where Watu wakawekeana Sheria Furani au Tamaduni furani katika jamii zao.

Walipitia Miaka mingi ya Kuangalia mazingira yalivyo na mwisho kuja na Best Solutions ambazo leo hii sisi tunataka ku challenge kila kitu na kupinga
Mkuu hizi nondo ulizopiga sio za nchi hii. Thanks.
 
Katika jamii nyingi za Kiafrika, kuna mtazamo uliojengeka kwamba mwanamke ni lazima azalie watoto ili awe "kamili" au awe amekamilisha wajibu wake kwa familia na jamii. Lakini hivi kweli tunapaswa kufikiria hivyo? Mbona kuna wanawake wanaoamua kwa hiari yao kutopata watoto, wakisisitiza kuwa maisha yana maana zaidi ya kulea familia? Na je, uamuzi huo ni wa kuonekana kuwa ni uasi wa tamaduni zetu au ni jambo la kawaida kabisa?

Kwa upande mmoja, kuna watu wanaoamini kuwa jukumu la mwanamke lina mizizi katika kuzaliana na kulea kizazi kijacho. Hii ni sehemu ya utamaduni na mfumo wa jamii nyingi – wanawake wamekuwa wakihimizwa tangu zamani kulenga katika familia, kutunza watoto, na kuendeleza ukoo. Hii inachukuliwa kama sehemu ya urithi wa kiutamaduni na vilevile usalama wa jamii. Sasa, pale mwanamke anapoamua kutozaa, mara nyingi anakutana na maswali, shinikizo, na wakati mwingine lawama kutoka kwa familia na jamii kwa jumla. Inachukuliwa kama "kukwepa" wajibu au "kutoroka" majukumu yake kwa jamii.

Lakini upande mwingine wa sarafu ni kuwa, kuna wanawake wanaochagua kutozaa kwa sababu zao binafsi, zikiwemo kupenda uhuru, kutaka kujikita zaidi kwenye kazi au malengo yao binafsi, au hata kwa sababu za afya au kifedha. Kwao, kuzaa si lazima – ni chaguo. Wanajiuliza, hivi, kama wanaume hawakosolewi wanapochagua kutopata watoto, kwa nini mwanamke achunguzwe kwa kila hatua anayochukua kuhusu mwili na maisha yake? Pia, wanaamini kuwa mtu hawezi kuwa mzazi bora kama hataki kwa hiari, na kuna vitu vingi vya kufanya ambavyo pia vinaweza kuchangia jamii, si lazima kwa kuzaa tu.

Jamii zinapaswa kuelewa kuwa si kila mwanamke anayeamua kutopata watoto anakosea au "kupoteza mwelekeo." Badala yake, tunaweza kuunga mkono wanawake hao na kuacha kuwashinikiza. Uamuzi wa kuzaa au kutozaa unapaswa kuwa wa mtu binafsi, si wa jamii. Tunaweza kujadili pamoja kama hivi vyote ni sehemu ya uhuru wa mwanamke au ni kujinasua kutoka kwenye utamaduni wa zamani. Hivyo, je, ni lazima kila mwanamke awe na mtoto? Au ni wakati tufikirie upya jinsi tunavyoona wajibu wa mwanamke katika jamii yetu?
Wewe ungeandikaje huu uzi mama yako angekuwa na mawazo kama yako ya kutozaa?
 
Kwani lazima kuacha genesis za ukoo wako... ukatili ni kuleta kiumbe katika dunia hii yenye mabalaa Kila uchwao
Wazazi wako kukuzaa walikosea yaani walifanya ukatili?
Nakupongeza kwa upuuzi wako mkubwa kabisa kuwahi kuuonesha .

Haya usizae kwanza unawapotosha watu wewe ukute umezaa watoto mpaka 9 huko!

Yaanj mpaka unakufa wazazi wako hawana mjukuu kweli?
 
Back
Top Bottom