Kuzaliwa Kwa Nabii Issa ( YESU)

Kuzaliwa Kwa Nabii Issa ( YESU)

ISA SIO YESU ,TUACHE KUPAKAZIA WATU UONGO ,TUACHE KUJIPENDEKEZA

Jina la Yesu wa Biblia lina uhalisia wa kihistoria unaothibitishwa na wataalam wa tafsiri.

Jina hili alipewa kama inavyorekodiwa katika Luka 2:21, na lilitumiwa na watu wa karibu naye kama mama yake, baba yake wa kambo, ndugu zake, majirani, marafiki, na wanafunzi wake wakati wa maisha yake duniani.

Kwa hakika, jina la Yesu lilikuwa la Kiyahudi, yaani "Yeshua," ambalo lina maana ya "kweli."

Tafsiri ya jina hili kutoka Kiebrania hadi Kiingereza ni "Jesus." Jina hili halikuchaguliwa kiholela, bali Mungu mwenyewe alilitoa (Mathayo 1:21; Luka 1:31), likiwa na ujumbe wa wazi kuhusu sababu ya kuzaliwa kwa Yesu, yaani kuokoa watu wake kutoka dhambini (Mathayo 1:21).

Katika utamaduni wa Kiarabu, jina la Yesu linajulikana kama "Yasu," na si "Isa" kama ilivyo kwenye Koran. Wakristo wa Kiarabu, ambao ni zaidi ya 99.99%, hutumia jina "Yasu" katika makanisa yao, matangazo ya redio na televisheni, na katika maisha yao ya kiimani.

Hili linaonyesha kuwa jina "Isa" ni tafsiri ya Kiislamu ambayo si sahihi kwa msingi wa kiisimu. Katika lugha ya Kiarabu, tafsiri ya jina la Kiebrania "Yeshua" inapaswa kuwa "Yasu," kufuatana na sheria za kiisimu za lugha za Kisemiti.

Mabadiliko ya jina kutoka Kiebrania hadi lugha nyingine yanaonyesha safari yake kupitia historia ya tafsiri. Kutoka "Yeshua" (Kiebrania), jina hili lilibadilishwa kuwa "Ιησους" (Kigiriki), "Yesu" (Kilatini), "Jesus" (Kiingereza), na hatimaye "Yesu" (Kiswahili).

Hatua muhimu ilikuwa tafsiri ya Septuaginta, ambayo ni maandiko ya Kiyahudi yaliyotafsiriwa kwa Kigiriki miaka 200 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Tafsiri hiyo ilifanikisha mpito wa jina kutoka Kiyahudi hadi Kigiriki, na jina hilo likatumiwa katika maandiko ya Agano Jipya.

Lugha za Kisemiti, kama Kiyahudi na Kiarabu, zina uhusiano wa karibu unaoruhusu mabadiliko ya fonetiki, kama vile sauti ya "Shin" ya Kiebrania kubadilika kuwa "Sin" ya Kiarabu. Kwa hivyo, "Yeshua" katika Kiebrania inalingana na "Yasu" katika Kiarabu. Mabadiliko haya ya fonetiki yanathibitisha kuwa "Yasu" ni tafsiri sahihi ya jina la Yesu katika Kiarabu. Kinyume chake, jina "Isa" halifuati sheria hizi za fonetiki na linaonekana kuwa tafsiri bandia isiyo na mizizi katika historia ya lugha.

Kwa muhtasari, jina la Yesu lina asili yake katika Kiyahudi kama "Yeshua," likiwa na maana ya kipekee inayotufundisha kuhusu kazi yake ya ukombozi. Tafsiri ya jina hili katika lugha mbalimbali inaonyesha mabadiliko ya kifonetiki yanayofuata sheria za kiisimu, huku ikiacha wazi tofauti kati ya "Yasu" ya Kiarabu ya Kikristo na "Isa" ya Kiarabu ya Kiislamu. Hivyo, jina la Yesu linabaki kuwa na uhalisia wake wa kihistoria na tafsiri sahihi katika lugha mbalimbali.
 
N
Wanatheolojia wa Roman Cathoric hasa mzee Titus Amigu anasema Nabii Issa na Yesu Kristo ni watu wawili tofauti..

Huyo nabii wenu Issa sijui mudi alimtoa wapi?Hata mimi nakubaliana na Mzee Amigu maana hata mahali walipozaliwa ni tofauti:Yesu Kristof alizaliwa Mji wa Bethlehem ya Uyahudi tena usiku wakati Huyo nabii Issa alizaliwa Uarabuni tena mchana chini ya mti wa mtende mimi sijui kwa nini inalazimishwa ione kana ni mtu mmoja
 
M nataka kujua na huyu father Xmas vp nae maana anachukua nafasi kubwa kuliko
Wajuz wa theology nipeni elimu ya huyu mtu ilikuaje hadi aka jumlishwa kwenye sku hii
 
Malaria 2 kwa nini Waisrael/Wayahudi walipendelewa sana? Wao wana Manabii wengi sana kuliko jamii nyingine yoyote na hata huyu Isa mnasema alitumwa kwao tu. Sababu ni nini ya huu upemdeleo wa wazi wazi?
 
Malaria 2 kwa nini Waisrael/Wayahudi walipendelewa sana? Wao wana Manabii wengi sana kuliko jamii nyingine yoyote na hata huyu Isa mnasema alitumwa kwao tu. Sababu ni nini ya huu upemdeleo wa wazi wazi?
Kwakua walikuwa wakaidi na watata kuliko watu wengine na pia walikuwa wakiwauwa mitume wao , hivyo ikapelekea wawe na mitume wengi zaidi.
 
Kwakua walikuwa wakaidi na watata kuliko watu wengine na pia walikuwa wakiwauwa mitume wao , hivyo ikapelekea wawe na mitume wengi zaidi.
Kwa nn Mungu apeleke mitume kwa watu watata na wakaidi?
 
Wanatheolojia wa Roman Cathoric hasa mzee Titus Amigu anasema Nabii Issa na Yesu Kristo ni watu wawili tofauti..

Huyo nabii wenu Issa sijui mudi alimtoa wapi?
Naunga mkono hoja. Mwaka 1994 niliwahi kuhudhuria Semina ya Neno la Mungu Kanisa la Lutheran Mviringo pale Magomeni. Miongoni mwa watoa mada alikuwa Baba Askofu Mstaafu Dk. Elinaza Sendoro. Naye alisema hivyo hivyo kwamba Yesu Kristu na Nabii Issa ni watu wawili tofauti. Na moja ya hoja yake ni;
a) Yesu Kristu alizaliwa kwenye holi la ng'ombe wakati Nabii Issa alizaliwa chini ya mtende! Kwamba mtu mmoja HAWEZI kuzaliwa sehemu mbili tofauti!!
 
Back
Top Bottom