Nitajaribu kukujibu kadri nitakavyoweza.......
Hyrocephalus maana yake maji kwenye ubongo..."water in the brain"...kwenye ubongo kuna maji huzunguka yanaitwa "celebrospinal fluid" katika njia zinazoitwa "ventricles" ambazo zimetanda mpaka kwenye uti wa mgongo....maji haya hulinda ubongo....maji haya yapo kwenye mzunguko...inapotokea hitilafu katika mzunguko wa maji haya na kufanya kujaa kwenye kichwa hapo ndipo hutokea hydrocephalus.....inaweza kutokea hitilafu katika utengenezaji wa haya maji na kusababisha kutengenezwa kwa wingi kuliko kawaida (hypersecretion) au kuziba kwa njia za kutokea na kusababisha kujaa kwenye ubongo...
Sababu za huu ugonjwa ni nyingi.....inawezekanaa na ikawa tatizo la kuzaliwa la kimaumbile (Arnold-Chiari_malformation,Dandy-Walker_malformation..) au magonjwa baada ya kuzaliwa (meningitis,kansa ya ubongo....)
Kwa watu wazima huwa hawavimbi vichwa maana mafuvu yao yameshakomaa ila hupatwa na tatizo la kuongezeka pressure kichwani na kukandamizwa kwa ubongo kama maji yakijaa wingi...
Tiba ni upasuaji kwa kutumia "cerebral shunts" kukinga maji kutoka katika ubongo...