Kuzaliwa na maji kichwani(Hyrocephalus)

Kuzaliwa na maji kichwani(Hyrocephalus)

Columbus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
2,002
Reaction score
651
Hii hali ya mtoto mchanga kuzaliwa na hatimaye kichwa kuendelea kuwa kikubwa inasababishwa na nini? siku hizi nimekuwa nikishuhudia ongezeko kubwa la watoto wa jinsi hii na hata ukitembelea hospitali mbalimbali hapa Dar utashuhudia akina mama wakiwa na watoto hao. je hii hali inaweza kumpata mtu ukubwani?
 
Nitajaribu kukujibu kadri nitakavyoweza.......

Hyrocephalus maana yake maji kwenye ubongo..."water in the brain"...kwenye ubongo kuna maji huzunguka yanaitwa "celebrospinal fluid" katika njia zinazoitwa "ventricles" ambazo zimetanda mpaka kwenye uti wa mgongo....maji haya hulinda ubongo....maji haya yapo kwenye mzunguko...inapotokea hitilafu katika mzunguko wa maji haya na kufanya kujaa kwenye kichwa hapo ndipo hutokea hydrocephalus.....inaweza kutokea hitilafu katika utengenezaji wa haya maji na kusababisha kutengenezwa kwa wingi kuliko kawaida (hypersecretion) au kuziba kwa njia za kutokea na kusababisha kujaa kwenye ubongo...

Sababu za huu ugonjwa ni nyingi.....inawezekanaa na ikawa tatizo la kuzaliwa la kimaumbile (Arnold-Chiari_malformation,Dandy-Walker_malformation..) au magonjwa baada ya kuzaliwa (meningitis,kansa ya ubongo....)

Kwa watu wazima huwa hawavimbi vichwa maana mafuvu yao yameshakomaa ila hupatwa na tatizo la kuongezeka pressure kichwani na kukandamizwa kwa ubongo kama maji yakijaa wingi...

Tiba ni upasuaji kwa kutumia "cerebral shunts" kukinga maji kutoka katika ubongo...
 
Samahani, nilipata kusikia kuwa tabia fulani fulani za mama mjamzito pia zinaweza kusababisha ugonjwa huu. Kwa mfano mama mjamzito akiwa na tabia za hasira au mawazo kupita kiasi kunaweza kusababisha uumbaji wa mtoto aliyeko tumboni kupata madhara ikiwemo tatizo hili la kujaa maji kichwani. Pia inasemekana tabia za ulaji chakula wa mama mjamzito zinaweza kusababisha hitilafu hii?
 
Kwasababu ugonjwa huu usababishwa pia na matatizo ya kimaumbile ya kuzaliwa (malformations) , ni kweli chakula kwa mama mjamzito hasa vitamin B (folic acid) ni muhimu kuzuia malformations hizo za kuzaliwa....ila sidhani kama kuna vyakula fulani vinaweza kusababisha ugonjwa huu naona labda ni upungufu wa virutubisho fulani.....

Kuhusu hasira kipindi cha ujauzito aisee hii sijasikia popote ila ni vizuri kipindi cha ujauzito mama awe kwenye afya nzuri ya kimwili hata kiakili ili kuepuka complications........

Natumai nimejibu swali lako.
 
Back
Top Bottom