Kuzindika gari

kagari kangu mwaka wa tano huu hakajaniletea ajali yeyote. Na pia nasafiri sana safari za usiku tenda za umbali mrefu 700+km sijakutana na mauzauza.

NB. Kuna jamaa nilikua nae kwenye gari tupo speed usiku kama saa 5. Kufika home akaniambia kuna sehem moto umekatiza mbele yetu japo mimi sikuuona. Kumbuka hapo tupo kwendo,
 

Acha mambo hayo..

Kata bima kubwa ndo jambo la maana
 
Mungu hawezi kukusaidia kwenye ajali.

Angekuwa anasaidia kuepusha ajali basi kungekuwa hamna ajali.
Maana kila siku watu wanamuomba.
Kwa hiyo zindiko ndio linaweza kusaidia eennhh??.
 
Wewe gari lako umlifanyia zindiko/kafara?
 

Wewe mkristo au Muislam? Fata muongozo wa dini yako. Kama hauna dini uliza wazee wako
 
Unajua ndugu ni rahisi sana kutoa kauli zisizo na adabu ili upate sifa au umaarufu. Mungu ni mwema kila wakati, si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa rehema. Utakuja kujua hujui.

Wafia dini kwa vitisho hamjambo!
Basi mwambie mungu aniue nifie mbali.
Yaani Mungu anapata hasira?
Mbona huyo mshikaji ana sifa za binadamu sasa?
 
Mkuu Mambo haya Africa yapo Sana.
Kama madereva wanaona mauzauza wakiwa kwenye usukani,

Je bado unaamini ajali hazitengenezwi??

--Hivi ushajiuliza kwa nn madereva wa magari ya mbali wanavaa ringi za Shaba mkononi?

--ushajiuliza kwann madereva wanapoendesha magari usiku wanapenda kuwe na mtu pembeni wanazungumza na kutia story?

Huwa hawapendi kuendesha peke yao huku watu wote ndani ya gari wamelala.

--kwann ajali nyingi za usiku hutokea dereva akiwa peke yake?

Ushuhuda..
siku moja,,nilipanda bajaji ya jamaa fulani usiku mida kama saa Saba hivi nikirudi zangu home.

Tukiwa kwenye mwendo wa Kasi,,tukapita mahali fulani kwenye kona tukakutana na Lori mbele yetu na basi linatanua huku likija kwetu kwa kasi ya ajabu sn kuelekea tulipo..

Mimi na dereva tulifumba macho kwa kujuwa ndy mwisho wa maisha yetu.

Mwanzo dereva alitaka aende kwenye korongo ili aepuke kugongana uso kwa uso na either Lori au basi ..

Nikamwambiya usipinde popote nyoosha usukani huenda jamaa wakatukwepa,

lakini tulishachelewa tukawa katikati ya yale magari mawili yaliyotokea mbele yetu ghafla,

Tulimulikwa kwa taa Kali hadi tukachanganyikiwa..
Dereva mikono ilikufa ganzi kwa hofu ya kifo huku tunajiona.
Tukabaki kusali sala za mwisho za kuomba toba.
Kilichofata ni ajabu kabisa......

Hadi leo naamini Mambo hya yapo,,na walozi wapo.


Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Ingia barabarani bila kuzindika ili uone kama kweli kuna maluelue.
 
Mungu hawezi kukusaidia kwenye ajali.

Angekuwa anasaidia kuepusha ajali basi kungekuwa hamna ajali.
Maana kila siku watu wanamuomba.
Mpinga Kristo unajitahidi sana kutetea upagani wako, lakini sisi tuliowahi kupewa hadi vitisho vya ajali za kutengenezwa kimakusudi na kichawi kisha Mungu alisimama pamoja nasi tukaepushwa nazo, tusemeje sasa kwa huo ukuu wa Mungu?[emoji848]

Mungu yupo na anatenda miujiza, endelea kudanganya Watoto tu ndipo utaeleweka maana ni huyo huyo Mungu utayemwomba akuponye na maradhi yakikukuta hapo sasa hivi, ila nyuma ya keyboard unamkataa kama vile kweli [emoji38]
 
Malizia basi
 
Kuna muda naamini kuna muda siamini na kinachosababisha hayo nimedumu kwenye udereva miaka 13 masafa marefu kilometa 2200 kila baada ya wiki mbili ila kusema kweli sijawahi ona wala kupata hizo ishu zaidi zaid kuvamiwa na majambazi kuwekewa magogo njiani kutekwa usiku ila kuhusu haya mambo huwa nasikia tu wana kuwa wanaona nyoka kwenye steling mara wanaona barabara nane zimefanana asee wakuu nipo kwenye utafiti siku yakinikuta nitakuja kusema
 
Malizia basi
Tuliwekwa kati kati ya Lori na basi mbele yetu.
Sote tulifumba macho na kuamini tunagongana uso kwa uso na gari zile.
Baada ya akili kuturudia tukajikuta zile gari zimetupita na hakuna dalili yeyote ya kugongwa wala kukwaruzwa na chochote.

Dereva alishuka akakimbia na Mimi nimebaki ndani ya bajaj kwa hofu..
Kumbe tungesema tukwepe tuingie kwenye korongo ilikuwa ndy safari ya milele ungetuangazia..
Zile hazikuwa gari za kawaida bali ni mauzauza ili tutumbukie kwenye korongo.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Ushirikina hautokusaidia zaidi ya ww kuanza kujiandikisha mwenyewe na kutumikishwa kma wanavotaka

Kuna nyuzi moja ya Mshana Jr kaisome ameandika vzr kuhusu ayo mambo
 
nina endesha Ist DV.. 341 toka imeingia bongo land mwaka jana mwanzoni mpaka sasa na dunda nayo tu japo nimewahi pigwa pass siku moja pale kawe round about ila namshukuru mungu gari bado mpya ina hali nzuri tu na mimi ni mzima haswa, kikubwa mtegemee mungu pekee uta tusua hawa waganga sometimes marue rue juzi nimesikia dada mkoja kauwawa kisa ana zindika 9M kwa mganga kafa na M9 yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…