Kuziona Azam vs Yanga 7000

Kuziona Azam vs Yanga 7000

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangaza viingilio vya mchezo huo ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni, kuwa ni Tsh 7,000 kwa majukaa yenye rangi ya kijani, bluu na rangi ya chingwa, VIP B & C tsh 20,000 na VIP A tsh 30,000.

Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo jumamosi asubuhi saa 2 kamili katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii utachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo, (DSM), akisaidiwa na Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Josephat Daud Bulali (Tanga), mwamuzi wa akiba Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.
 
Wakimataifa haooo god bless jangwani wazee wa anga kwa anga.
 
Hawa watangazaji wa Azam TV hovyo kabisa....Wanatangaza kinasi mnoo...

Hasa huyu Baruany Muhuza...Hafai kabisa kutangaza mpira..
 
Back
Top Bottom