SoC04 Kuzorota na kutomalizika kwa wakati miundombinu wakati wa utekelezaji wa miradi

SoC04 Kuzorota na kutomalizika kwa wakati miundombinu wakati wa utekelezaji wa miradi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Obadia idd luyagaza

New Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Moja ya kitu Cha kujivunia ni kuzaliwa Katika nchi ya Tanzania, imejaliwa kuwa na vitu vingi vya kuvutia na kupendeza sana vilivyo tapakaa nchi nzima. Mfano wa vitu hivyo ni kama Mlima Kilimanjaro, Mlima meru, Mito mikubwa ikiwemo Malagarasi ,pangani ,Mapolomoko ya Rukwa, Hifadhi za wanyama mfano Gombe n.k.

Vitu vyote vya kuvutia vilivyopo Kila pande ya nchi, havitaweza kufikika Kwa wakati sahihi pasipo Miundombinu thabiti na yenye tija.

Mara nyingi Kampuni zinazopewa dhamana ya kutekeleza Miradi ya Miundombinu kama kutengeneza barabara,miundombinu ya Maji na vingine vingi zimekuwa na tabia ya kulegalega zikidai uhaba wa Malighafi na vinginevyo

Katika harakati za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuibua Mipango ya maendeleo katika Vipindi tofauti vya Bajeti, Sekta ya Miundombinu imekuwa ikipewa kipaumbele Cha Bajeti kubwa Ili kutekeleza sera zake.

Kwa kupitia Jukwaa la Story of change (SoC 2024) la Jamii Forums, Ningependa kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba KUZOLOTA NA KUTOMALIZIKA KWA WAKATI MIRADI YA MIUNDOMBINU ni kwa sababu zifuatazo:-

1. Kandarasi zinazopewa dhamana ya kutekeleza mradi, haziajiri vijana wenye sifa stahiki juu ya kazi husika Ili basi zitengeneze faida.

2. Kandarasi hizohizo hukwepa kuajiri Mafundi wenye Elimu na Ujuzi juu ya kazi husika, badala yake huajiri Mafundi wa mtaani ambao hawana uzoefu wowote, hivyo kupeleke kuzolota na kutoisha Kwa wakati miradi ya maendeleo ya Miundo mbinu.

3. Kutotumia kiwango sawa Cha Malighafi zilizopo Kwa kiwango sahihi Cha maelekezo yaliyotolewa na Serikali. Hivyo basi Kupelekea mradi kuwa chini ya kiwango na kukwamisha Maendeleo.

HITIMISHO YA NINI KIFANYIKE.

Kama mdau wa story of change ya Jamii forum 2024, katika harakati ya kupambana na mzoloto huu wa Miundombinu hafifu katika baadhi ya miradi, Ningeshauri yafuatayo katika Mpango wa maendeleo katika miaka 5 Hadi 25.

1. Serikali ihakikishe kandarasi iliyopewa dhamana ya mradi imekaguliwa ipasavyo juu ya maofisa iliyowaajili Je? wapo eneo la kazi husika.

2. Serikali ifanye ukaguzi wa Miradi mara Kwa mara eneo la kazi, tofauti na mkandarasi kujiongoza mwenyewe wakati wa kazi.

3. Serikali itoe ajira Kwa vijana wenye Elimu husika hata Kwa Mikataba Ili kuimalisha kazi yenye ufanisi ,hatimaye kupunguza kuzolota Kwa miradi.

4. Serikali ibuni mbinu wezeshi ya kulatibu na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu kama, Kuunda kamati wezeshi itakayowajibika mojakwamoja kwenye Miradi ikisaidia Tanroad na Tarura.

 
Upvote 0
Back
Top Bottom