Baba Kabunyee
Member
- Jul 30, 2024
- 10
- 12
Nikicheki kwa jicho la mwewe ni kuwa kitendo cha kutumia nguvu kubwa sana kudhibiti haya maandamano ya CHADEMA ni kuihujumu serikali ya Mama Samia na kuipaka uchafu. Wanaomshauri Rais wapigwe tu chini. Ingawa CHADEMA nao walizingua kuja na kauli ya "Samia must go" , serikali ingetumia busara kuwaacha tu waandamane ili mradi hawavunji sheria na kufanya uhalifu.
Ninaona kuna watu wabaya wanaocheza karata zao vyema pande zote yaani CCM na upinzani. Naona huenda waliona Mama asingewanyima kibali CHADEMA kuandamana na hivyo lengo la kuipaka uchafu serikali lingekwama kwahiyo wakaamua kuwajaza ujinga CHADEMA waje na kauli ya kihaini ili wanyimwe kibali.