Mataifa ya nje ukiharibu biashara zao wanakuwekea vikwazo na kukunyima misaada
Safari mataifa ya ulaya na Marekani wamegoma kutoa misaada ya Hali na Mali kea vyama vya upinzani Tanzania Baada ya wao kupinga bungeni na nje ya bunge kuwa serikali isinunue Ndege za bombarier na Boeing
Sasa hivi wako na Magufuli mdau muhimu Kwao anayewaingizia pesa aliyekayaa presha za upinzani akawapa biashara
Pia wazungu huwa na hasira na serikali Kama hawalipi madeni yao walliyokopesha
Serikali ya Magufuli imekuwa ikilipa madeni Bila shida hivyo kuwa kipenzi Cha nchi za magharibi sababu pesa Yao hailali nje
Akina Tundu Lissu walioongoza kampeni ya kutaka serikali isinunue Ndege hawana uungwaji mkono na Nchi za magharibi
Kwa CHADEMA mgombea pekee anayekubalika na Nchi za magharibi Ni Nyalandu pekee sababu wanamfahamu vizuri katanya kazi nao taasisi kubwa na Hana lolote alilowahi haribia biashara zao
Hahhaa kumbe Magufuli na ccm ni vipenzi vya mabeberu. Subirini ujauzito
Magufuli na mabeberu wamegeuka vipenzi Tena jamani Sasa hivi. Wamegeuka wadau muhimu?
Na bado , hadi mtatembea uchi kwa kusifia.
Hivi wapinzani walipinga ununuaji wa ndege,au walikuwa wanataka uwazi ukweli na uhizinishaji wa hayo manunuzi?
Kweli vita ya mabeberu haieleweki. Leo wenu kesho mnamkataa....
Utopolo first class huu, tuharibu fedha zetu kwa ajili ya kumfurahisha mzungu
Serikali zina hisa KQ, SAA, na mengine mengi, na ukiona shirika binafsi linakufa ndio ujue la serikali litakufa zaidi. ATCL ilikufa wakati wa Mkapa/Kikwete wakati Precision Air ndio inanyanyuka. Jifunze kitu hapo.Mashirika yote ulizotaja ya ndege yaliyokufa duniani kote Ni ya binafsi Sio ya serikali yenye hisa asilimia 100
naona unachanganya mambo
Quot
Maccm yakishiba rushwa ndio yanajifanya kuropoka kwamba kuna mabeberu, wakiwa na njaa wanawaita mabeberu wadau wa maendeleoMagufuli na mabeberu wamegeuka vipenzi Tena jamani Sasa hivi. Wamegeuka wadau muhimu?
Huelewi biashara wewe ndio maana serikali yako ilishindwa kuendesha ATCL tangu zamani na kuishia kufa wakati huo huku Precision Air ikiibuka kuwa kidedea. Magu anafanya biashara ya ndege kama anavyofanya biashara ya ng'ombe. Unakosea unapofikiri serikali haiwezi kupata hasara, na hizo ndio fikra potofu za viongozi wa Tanzania ndio maana hatuendelei. Wenzetu nchi zilizoendelea wanahesabu kila kitu na wanaendesha mashirika hata yale ya serikali kwa mtindo wa kibiashara na sio mtindo wa hasara ya wengi kama sisi.Sio kweli shirika la ndege linalomilikiwa asilimia Mia moja na serikali Sio rahisi kupata kitu kinaitwa hasara kwa sababu huwezi lipima kwa vigezo vya kampuni binafsi vya kuangalia profit au loss sababu serikali ndie mumiliki hata isipopata gawio inakuwa imeshavuna pesa kibao
Mfano wewe ukikata tiketi kule ndani Kuna VAT , Airport charge sijui sales tax ambavyo vyote vinaingia mfuko wa serikali !!! Ikijaza mafuta mafuta Yale yana Kodi ile Kodi inaingia mfuko wa serikali supplies wa huduma zote za ndege viwe vyakula ,nk vina Kodi hiyo Kodi inaingia mfuko wa serikali kwa hiyo mwisho wa siku unatakiwa ukipiga hesabu Kama shirika la ndege limepata faida au hasara angalia kwa mwaka operation zake zimeingiza Kodi shilingi ngapi kampuni binafsi Kodi zote hizo Ni expenditure lakini kwa shirika la serikali Ni income kwa serikali kwa hiyo kucheki shirika la ndege la serikali limeingiza income kwa serikali kiasi gani unachukua mapato Yao ya mauzo ya tiketi inajumlisha kodi zote za mauzo vat etc jumlisha Kodi zote za suppliers then unatoa expenditure ndio unajua shirika Lina loss au la!!! Income tax wao waweza wasamehe ukiona Kuna excess ya income over expenditure before tax ili wajijenge zaidi . Mashirika binafsi huenda mbali wanaongoza kutoa income tax ya kulipa serikalini wakati shirika la umma serikali yaweza acha kuwa msilipe as long as your income exceeds your expenditure that. Excess is a profit so far to the government .Ndio maana nakwambia Sio rahisi shirika linalomilikiwa asilimia 100 na serikali kufa
Pia kumbuka usafiri wote ndani ya nchi wafanyakazi w umma lazima wapande ndege za mwajiri wao ambaye Ni serikali na ndio wapandaji wakubwa
Magufuli amefanya kwa Precision alichofanya kwa CHADEMA na vyama vingine, ametumia nguvu na ubabe kuua ushindani wa kibiashara lakini kwa taarifa yako Precision Air imesimama na taarifa ni kwamba ATCL itakufa na kuacha PA inapaa. Ukitaka kujua hilo fungua hii link angalia live arrivals and departures uwanja wa ndege Dar ndio utajua, hakuna safari hata moja ya ATCL, ni PA pekee aliyepo kuacha hizi chartered flights ndogo ndogo Dar-es-Salaam Julius Nyerere International Airport Arrivals, Dar-es-Salaam DAR Arrivals | AirportiaHizo precision zilikuwa ndege za mifisadi serikalini na majina wanajulikana wakawa Wana force wafanyakazi wote wa umma wapande ndege lao ndio kisa Cha ATCL kuyumba, mifisadi iliponogewa ikaanzisha shirika lingine la Fast Jet mijizi na mifisadi
Magufuli alilipokuja Ile kusema tu marufuku mfanyakazi wa umma kutumia usafiri wa ndege binafsi Fast Jet ikafa kifo Cha mende na Precision inapumulia mashine ICU wakati ATCL inakata mbuga hewani kila kona
Mataifa ya nje ukiharibu biashara zao wanakuwekea vikwazo na kukunyima misaada
Safari mataifa ya ulaya na Marekani wamegoma kutoa misaada ya Hali na Mali kea vyama vya upinzani Tanzania Baada ya wao kupinga bungeni na nje ya bunge kuwa serikali isinunue Ndege za bombarier na Boeing
Sasa hivi wako na Magufuli mdau muhimu Kwao anayewaingizia pesa aliyekayaa presha za upinzani akawapa biashara
Pia wazungu huwa na hasira na serikali Kama hawalipi madeni yao walliyokopesha
Serikali ya Magufuli imekuwa ikilipa madeni Bila shida hivyo kuwa kipenzi Cha nchi za magharibi sababu pesa Yao hailali nje
Akina Tundu Lissu walioongoza kampeni ya kutaka serikali isinunue Ndege hawana uungwaji mkono na Nchi za magharibi
Kwa CHADEMA mgombea pekee anayekubalika na Nchi za magharibi Ni Nyalandu pekee sababu wanamfahamu vizuri katanya kazi nao taasisi kubwa na Hana lolote alilowahi haribia biashara zao
Nafikiri unabisha kwasababu ya ujinga tu nani atarusha ndege tupu unajua gharama ya kurusha ndege ya kawaida tu kutoka Dar hadi K'Njaro? Zaidi ya 10M. Kwa taarifa yako tunachangia kwa kodi zetu kufidia hasara ya ATCL na hilo wanajua wachache nyie endeleeni kushabikia watu tu.Huniambii kitu bila kutoa idadi ya abiria wanaruka kila flight Huwezi Ni convince!! Kuna kuruka tu ili uonekane uko hewani!!
CLASSIC MATERIALS HERE!Usiweke mabandiko ya aina hii kama una nia ya dhati ya kuitukuza serikali ya JPM; labda kama unacheza mchezo wa “sarcasm” ambao unatumiwa sana na mdau mmoja maarufu wa JF.
Kwanza, jua tu kuwa hizo ndege zimenunuliwa kwa “cash money” ambao ni mtindo wa kifisadi wenye manufaa makubwa sana kwa makampuni husika ya ndege. Hapo hatujui cha juu kilichopigwa ni kiasi gani. Mashirika makini ya ndege duniani hutumia zaidi mtindo wa “lease purchase”. Hawanunui wala kumiliki ndege kikamilifu (100%) na mikataba yao huruhusu kuzirudisha kwa kulipia kiasi walichotumia tu kibiashara.
Pili, rasilimali kuu ya shirika la ndege ni soko la usafiri (routes) zinazopatikana kwa mikataba baina ya nchi (BASAs) kulingana na mpango wake wa biashara. Ukiwa na soko na “business plan” imara, watengeneza ndege kama Boeing wako tayari kukupatia hata Dreamliners 10 kwa kianzio kidogo sana cha pesa wakitarajia mapato yako yatalipa kwa muda muafaka. Ndivyo wanavyofanya Ethiopian ambao hawatufikii kwa “utajiri”.
Tatu, tofautisha kati ya makampuni ya watengeneza ndege na serikali zao. Kuna wakati Serikali ya UK ililihukumu shirika la huko la mitambo ya anga (BAE Systems) kwa kutuuzia rada iliyopitwa na wakati kwa “bei ya kuruka” mahakama yao ikaamuru tulipwe fidia (maarufu enzi zile kama “chenji ya rada”). Ajabu wakuu wetu huku wa CCM muda wote wakiilalamikia serikali ya UK kuwa hatujaibiwa; tumeridhika na hiyo bei! Lakini chenji ilipowasili waliipokea kwa mikono miwili na bila kupoteza muda nayo wakaifisidi!
Sasa tukiona hela yetu inatolewa kinyemela kwa haya makampuni ambayo mara munayaita ya kibeberu tunapata taabu kuelewa mnasimamia nini hasa? Lengo kweli ni kufufua shirika la ndege (ATCL) au kufisidi hazina ya taifa kwa kushirikiana na makampuni ya watengeneza na wauzaji ndege?
Sikukatalii. Umesema kweli. Sasa hivi Boeing, Airbus na Bombardier na makampuni yao tanzu ya mauzo wanachekelea kweli kupata mshirika wa kibiashara kama Tanzania (awamu ya tano). Haijawahi kutokea. Na sitashangaa kabisa wakiwaona wapinzani kama Lissu na Zitto kama watu fitna. Sasa pima mwenyewe; wewe unapigania au unashabikia nini hapa?