Pre GE2025 Kuzuia uchafu kwenye uchaguzi, tufute mishahara kwa wachaguliwa wote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tunapenda kuwaza yasiyowezekana na kuacha kufikiria kufanya yale yenye kuwezekana hata kama ni kidogo kidogo.
Hebu taja hayo kidogo kidogo yaliyoshindikana miaka zaidi ya 30 Sasa, huku chaguzi zikizidi kuwa za kihayawani.
 
Hebu taja hayo kidogo kidogo yaliyoshindikana miaka zaidi ya 30 Sasa, huku chaguzi zikizidi kuwa za kihayawani.
Sasa mkuu kama hayo madogo tunakubali tumeshindwa kufanya sasa hayo makubwa unafikiri yatatokea kwa miujiza?
 
Umeangalia mbali sana... Mkuu
 
Sasa mkuu kama hayo madogo tunakubali tumeshindwa kufanya sasa hayo makubwa unafikiri yatatokea kwa miujiza?
Pitia kilichotekea Libya, Sudan, Egypt, Gabon nk, huko kote hayo madogo hayakuwa yanawezekana, yalikuja kuwezekana hayo makubwa tu. Au ilikuwa ni miujiza?
 
Hivi haiwezekani ukaanzishwa mjadala wa kitaifa juu ya kuondoa malipo kwa wabunge na madiwani ?
Walio tayari ningependa waseme. Kukiwa na uungwaji mkono mkubwa wa wazo hili, na wakawepo walio tayari kujitolea kushirikiana katika kuhakikisha mjadala huu unafanikiwa, mimi nipo tayari kuanzisha kongamano la kitaifa la wapiga kura kwa lengo la kujenga hamasa ya aina ya viongozi sisi wapiga kura tunaowataka..
 
Well Said
 
Pitia kilichotekea Libya, Sudan, Egypt, Gabon nk, huko kote hayo madogo hayakuwa yanawezekana, yalikuja kuwezekana hayo makubwa tu. Au ilikuwa ni miujiza?
Sio kila kilichotokea huko kinaweza kutokea na sehemu zengine, hii dunia ina historia nyingi na mifano mingi tu sasa wewe umechagua mifano ya matukio yaliyotokea katika hizo nchi haina maana na sisi lazima tutapita huko huko. Ukiangalia mazingira yetu sioni dalili ya hicho kitu kutokea sasa kukaa na kusubiri kitokee ndio sawa na kusubiri miujiza.

Kama machafuko tungeyaona ile 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…