Kuzuia uvuvi ziwa Victoria hakuna tija na ni kero kubwa

Kuzuia uvuvi ziwa Victoria hakuna tija na ni kero kubwa

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kumekuwepo utaratibu wa kusitisha uvuvi ziwa Victoria Kwa kipindi sasa.

Kwamba wanasitisha uvuvi kwa muda kama kulipa likizo ziwa na samaki ili wazaliane Kwa kipindi hicho.

Lakini tija ni ndogo na kero
Na hii inaibua nafasi za rushwa maana kuna wavuvi huingia ziwani na kuvua kipindi hicho cha zuia na kuuza samaki na dagaa Kwa bei kubwa maana zinakuwa zimeadimika mitaani

Uvuvi haiwezi kumaliza dagaa wala samaki ziwani. Waziri wa mifugo na uvuvi litazame hili

Kama mnafunga ziwa funga Kwa wote. Sio kipindi cha kufunga, tunaona wavuvi wakubwa wakiuza samaki sokoni huku wengine wakiwa wamezuia kupisha samaki na dagaa kuzaliana.
 
Tujifunze kufanya uvuvi endelevu. Siko kila kitu cha kupinga tena bila hoja za msingi. Hata nyumbani kwako hupiki na kula muda wote.
 
Huwezi kumaliza samaki kwa kuwavua? Jamaa umeandika Nini hapo
 
Mbona unaonekana kama ndugu umehamaki kwenye hili..... mamlaka zinafanya hivyo kwa nia njema na sio kuwakomoa wananchi......

Mamlaka ziangalie namna ya kuwadhibiti hao watumishi wasiokuwa waaminifu wanaokula rushwa na kukwamisha juhudi za serikali
 
Ziwa limefungwa Tanzania? Wamekubaliana Kenya na Uganda na wao wafunge huko?
 
Wanaingiza boti zao za uvuvi, ili wapige pesa kwa haraka.
 
Victoria limefungwa
Ni kero kuna wanategemea uvuvi ili wapate kukidhi mahitaji yao. Na muda waliosema watafungua ili shughuli ziendelee umeshapita. Kama ulivyosema kuna watu wanafaidika na hii ishu.
 
Back
Top Bottom