Kuzungumkuti gani hiki kati ya kuongeza bei ya umeme kwa mtumiaji au kupunguza bei kwa mtumiaji

Kuzungumkuti gani hiki kati ya kuongeza bei ya umeme kwa mtumiaji au kupunguza bei kwa mtumiaji

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Leo nimemsikia msemaji wa serikali TBC akitoa taarifa kwamba mitambo minane kati tisa katika bwawa la Nyerere sasa inazalisha umeme. Akasema umeme sasa tunao wa kutosha na ziada kubwa tu. Akasema hata mitambo mingine ikizimwa nchi nzima mitambo ya bwawa la Nyerere itatosheleza nchi na bado ziada itakuepo.
Kilichonishangaza ni pale alipozungumzia kilio cha wananchi na ahadi ambayo Magufuli alitoa kwamba umeme tukifika kujitosheleza kwa bwawa la Nyerere itabidi bei ishuke kwa sababu umeme wetu ni ghali sana na hauvutii wawekezaji wa viwanda kutoka nje hata kwa wawekezaji wa ndani. Kwa nchi za ulaya na marekani unit moja ya umeme kwa mtumiaji bei ni kiasi kama senti 0.2 ya dola ya kimarekani. Ambapo bei yetu Tanzania ni kiasi kama senti 15 ya dola ya kimarekani. Msemaji wa serikali alisema eti bei ya umeme kwa mtumiaji inabidi ibakie juu eti ili kuvutia nchini wawekeza wa kuzalisha umeme.
Binafsi najiuliza maswali hayo hapo chini:-
1. Kama tumeshajitosheleza na kua na ziada kwa uzalishaji umeme tena kwa gharama ya chini ya kuzalisha kwa nguvu ya maji, kwa nini kama nchi tuone tunawajibika kuweka bei kubwa kwa mtumiaji eti kuwavutia wawekezaji kwenye kuzalisha umeme? Kwa nini tunataka kua shamba la bibi kwa uzalishaji umeme.
2. Kama nchi lengo letu ni kuwapatia fursa wawekezaji kuwekeza kwa faida yao au kuhakikisha umeme unapatikana nchini kwetu kwa bei ya chini ili kuvutia wawekezaji wa viwanda wa nje na kua kichochoe cha uzalishaji wa mali nchini?
3. Je lengo na kipaumbele cha nchi yetu ni kua wauza umeme kwa nchi majirani au ni kua na umeme wa bei nafuu kuwavutia wawekezaji na kua kichochea cha maendeleo nchini kwetu?
Kuna faida kubwa nchi kuongozwa na mtu mwenye maono. Inavyoonekana kwa sasa kila kiongozi anavutia kamba pale anaona kuna lishe kwa upande wake.
 
Back
Top Bottom