Uchaguzi 2020 Kwa 'Ahadi' hii iliyo muhimu sana kwa Mtanzania yoyote yule Rais Magufuli acha Kuendelea Kupiga tena 'Kampeni' kwani tayari umeshashinda Urais 2020

Uchaguzi 2020 Kwa 'Ahadi' hii iliyo muhimu sana kwa Mtanzania yoyote yule Rais Magufuli acha Kuendelea Kupiga tena 'Kampeni' kwani tayari umeshashinda Urais 2020

Kumbe ni sera ya ccm pia? Niliisikia kwa lissu nikaogopa kuwa ingekuwa kisu cha kuichinja ccm, lakini kama ccm nao wameamka wataokoa kura kadhaa. Kudos
 
Tumshukuru sana Mh.LISSU, amekuwa anatoa ahadi hii, CCM wakawa wanasema haiwezekani,Rejea majibu ya Kafulila humu jamvini yalivyoungwa mkono na makada mbalimbali humu. Baada ya CCM kuona maji ya shingo katika hili sasa wameamua nao kuichangamkia hii ahadi.
 
"Miaka mitano ijayo kila Mtanzania kupata bima ya afya "-Mgombea urais CCM, John Magufuli

Nipashe

Nina uhakika kwa hii Ahadi Kuu si tu kwamba Rais Magufuli tayari ana 'Kura' yangu bali pia ameshapata 'Kura' zote za Watanzania waliojiandikisha.
Mara utasikia kwani mm nimewaambia muambukizane magonjwa, humjui huyu jamaa yeye anachowoza ni madege na madaraja hakuna zaidi anachojua
 
Sishaingai kutoa Bima! Kama wameweza kutoa hospital kila kata pasipo na dawa za kutosha sasa najiuliza hawa wenye Private wanaizidi serikali pesa au ndo ujinga wa kutuaminisha visivyo na maana.
 
"Miaka mitano ijayo kila Mtanzania kupata bima ya afya "-Mgombea urais CCM, John Magufuli

Nipashe

Nina uhakika kwa hii Ahadi Kuu si tu kwamba Rais Magufuli tayari ana 'Kura' yangu bali pia ameshapata 'Kura' zote za Watanzania waliojiandikisha.

Uongo mtupu.
Alipoingia madarakani alisema hayo hayo, baada ya kuingia kashindwa kutekeleza, kinyume chake kaenda kujenga uwanja wa ndege kule chato.
Wamebadilisha bima ya afya kuwa na viwango tofauti vya malipo na pia huduma. Kwa sehemu kubwa wanaotibiwa kwa bima ya afya gharama wanazo kwepa ni za kuwaona madaktari - consultation fees.
Gharama za baadhi ya vipimo, madawa inabidi walipie, kwani wanaandikiwa dawa na vipimo wanaambiwa hapa hatuna, nenda sehemu fulani ukapime, alafu utuletee majibu.
 
Ni kiongozi Bora, mazuri anayachukua haijalishi yametoka wapi.
Aache kuteka na kupoteza raia, arekebishe sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwani sheria ya zamani ilikuwa bora kuliko ya sasa. Sheria zote alizo tunga na kulazimisha zifanye kazi retrospectively azisimamishe ili zifanye kazi ktk utaratibu wa kawaida.
 
Back
Top Bottom