kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,375
- 4,893
Nilisikiliza kipindi cha michezo cha Sports HQ E FM radio, walikua wanazungumza kipigo ambacho timu yetu ya akina dada walipigika na Japan.
Ndipo muongoza kipindi alimtaka mchambuzi Bin nani sijui atoe maoni yake juu ya kipigo kile. Bin alitoa mapovu ambayo ukiyasikia hutaamini. Aliiponda vibaya ile timu, alienda mbali akasema ile timu haina uwezo wa kupiga pasi, sijui wamefikaje pale walipo.
Alipooulizwa na muongozaji wa kipindi kuwa huenda ni mechi iliwakataa, maana tayari walikua wameonesha michezo mizuri huko nyuma ndiyo maana wakafuzu hiyo michuano mikubwa, bwana mchambuzi alikataa kata kata, hadi akahusisha pengine walifika pale kwa figisu za mpira wa ki Afrika.
Mchambuzi yule, alisema ikiwa tumepigwa na Japan, basi tukikutana na Ufaransa itakua aibu kuu. Mara baada ya kushinda dhidi ya Ufaransa, mchambuzi amegeuka na kuwa mtu wa kusifu sana. Ukiangalia alichoandika Instagram yake huwezi kuamini kuwa ni mtu yule yule aliongea mwanzo bila akiba ya maneno.
Mchambuzi huyo imefika wakati anaandika maneno haya kwenye page yake, ".....amemkata govi kwa kushinda goli...." au ".... wamewatatua marinda kwa kuwafunga magoli.....". Maneno kama haya yanaongelewa na mchambuzi ambaye anadai alifanya kazi kwenye shirikisho la mpira wa nchi hii! Ni vituko.
Kama haitoshi mchambuzi huyu ambaye baada ya kusemwa sana ndiyo kaanza kuwa nadhifu na kujipenda maana hapo nyuma! Alifika wakati akasema viongozi wa yanga ni "Masela" hawajui walifanyalo. Achana na vituko vyake juu ya mchezaji Ki Aziz na sarakasi zake na Manara, mchambuzi huyu ni mtu wa hovyo mno.
Watu wa namna hii ndiyo hupata dhamana ya kusikilizwa na wengi, ndiyo maana miaka nenda rudi tunaonekana kuwa wababishaji kwenye kila kitu.