Kwa aina hii ya wachambuzi, michezo imeingiliwa na mamluki. Ni hatari

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
2,375
Reaction score
4,893
Nilisikiliza kipindi cha michezo cha Sports HQ E FM radio, walikua wanazungumza kipigo ambacho timu yetu ya akina dada walipigika na Japan.

Ndipo muongoza kipindi alimtaka mchambuzi Bin nani sijui atoe maoni yake juu ya kipigo kile. Bin alitoa mapovu ambayo ukiyasikia hutaamini. Aliiponda vibaya ile timu, alienda mbali akasema ile timu haina uwezo wa kupiga pasi, sijui wamefikaje pale walipo.

Alipooulizwa na muongozaji wa kipindi kuwa huenda ni mechi iliwakataa, maana tayari walikua wameonesha michezo mizuri huko nyuma ndiyo maana wakafuzu hiyo michuano mikubwa, bwana mchambuzi alikataa kata kata, hadi akahusisha pengine walifika pale kwa figisu za mpira wa ki Afrika.

Mchambuzi yule, alisema ikiwa tumepigwa na Japan, basi tukikutana na Ufaransa itakua aibu kuu. Mara baada ya kushinda dhidi ya Ufaransa, mchambuzi amegeuka na kuwa mtu wa kusifu sana. Ukiangalia alichoandika Instagram yake huwezi kuamini kuwa ni mtu yule yule aliongea mwanzo bila akiba ya maneno.

Mchambuzi huyo imefika wakati anaandika maneno haya kwenye page yake, ".....amemkata govi kwa kushinda goli...." au ".... wamewatatua marinda kwa kuwafunga magoli.....". Maneno kama haya yanaongelewa na mchambuzi ambaye anadai alifanya kazi kwenye shirikisho la mpira wa nchi hii! Ni vituko.

Kama haitoshi mchambuzi huyu ambaye baada ya kusemwa sana ndiyo kaanza kuwa nadhifu na kujipenda maana hapo nyuma! Alifika wakati akasema viongozi wa yanga ni "Masela" hawajui walifanyalo. Achana na vituko vyake juu ya mchezaji Ki Aziz na sarakasi zake na Manara, mchambuzi huyu ni mtu wa hovyo mno.

Watu wa namna hii ndiyo hupata dhamana ya kusikilizwa na wengi, ndiyo maana miaka nenda rudi tunaonekana kuwa wababishaji kwenye kila kitu.
 
Yanga hawampendi jemedari bin kazumari kwa kuwa anabifu na manara. Yani manara anajua kucheza na akili za utopolo ugomvi au furaha zake ananafanya inakuwa ya taasis
 
UTOH mna fuatilia mapungufu ya kazumari ili muwe na la kuongea... jamaa ni mchambuzi mzuri sana sema yuko tofauti na mienendo ya Yanga ndo maana munamuandama sana
 
Ile kanzu ya mchambuzi na kubazi alizo vaa uku caption ikidai ni wakala asiyejua ki English Kwa hakika Aliye mpiga Ile picha alimuonea sana.
 
Wafuasi wa Yanga akili zap haziko sawa hili jambo aliwahi kulisema msemaji wao kipenzi, Wameingia kwenye mtego wa Manara kipuuzi sana. Jemedari hana shida na Yanga ila huwa ni msema ukweli kitu ambacho Manara hapendi hivyo amewatumia hawa mapopoma kuwaaminisha kuwa Jemedari anaichukia yanga na wao wamejaa
Hivi mchambuzi gani Manara hajagombana nae? Jemedari imekuwa ngoma ngumu coz jamaa mmbishi anasimamia ukweli. Ukimuuliza Shabiki wa Yanga kwann hampendi Jemedari majibu atakayokupa ndipo utaamini hawa jamaa ni weupe kichwani.
 
1. Amecheza Mpira na anaujua vyema

2. Ni Mwerevu ( ana Akili )

3. Ni Mkweli.

4. Siyo Mnafiki.

5. Hanunuliki hovyo na Wapuuzi.

6. Anajiamini.

7. Ndiyo Mchambuzi Bora sasa nchini.

Namkubali sana hata Yeye anajua.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwahiyo ww ulitaka asifie ule ujinga walofanya mechi ya kwanza!??
 
Yanga hawampendi jemedari bin kazumari kwa kuwa anabifu na manara. Yani manara anajua kucheza na akili za utopolo ugomvi au furaha zake ananafanya inakuwa ya taasis
Kwa hii reasoning kweli watanzania tutaendelea kua hamnazo, yaani hapo ndio umetoa points zako?
 
Kwa reasoning hii ya u simba na yanga nchi hii inalea vijana hovyo, wapumbavu na washenzi. Mada mezani ipo very clear, kuhusu uchambuzi wa team ya taifa ya wanawake na ukigeu geu wa mchambuzi, lakini mmeacha mada maksudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…