Kwa akili ya kawaida bila VAR lile sio goli

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ukiwa na D mbili tu za form four utajua kuwa lile sio goli kwani sote tumeona uwanja uko flat hakuna mabonde wala nundu nundu.

Katika hali ya kawaida mpira ungevuka goal line,ungedundia ndani ya nyavu.

Ukiitafu fizikia ya mpira kuvuka msitari kisha udundie nje unaikosa labda lingekuwa goli la maajabu sana.

Hata hivyo sishangai kwani wanaolalamika wengi aidha wanaongozwa na hisia tu ama walimbetia yanga, ama walitamani wamsute Mo awaachie timu wakaifilisi.

Bado kuna VAR wamethibitisha sio goli.

Yanga tumewazoea maana kwa hapa kwetu hata wachezaji wao wakiumwa mafua tu wanamlaumu Karia ndiye analeta virus
 
Umethibitisha vipi kuwa uwanja ni perfectly flat? Hufahamu kuwa chini pana nyasi bandia ambazo ukikanyaga zinabonyea na kufanya usiwe sawa kila sehemu?

Nakushauri nenda ukaangalie kwa Mkapa.
 
Tukienda kwenye physics basi lile ni goli. Umesoma Mambo ya concarve na convarxe
 
Hata ukiwa na A+ mbili za Physics form 6 bado hujaiva kuweza kuelewa dynamics of rotating bodies, kwa hiyo utaishia conclusion shallow kama hii.
 
Nadhani wewe ndiye unayetakiwa kuficha ujinga,maana umeacha hisia zikuongoze,utawezaje kufikiri?
Ukiambiwa ufiche ujinga jitahidi kweli ufiche ujinga. Hii si mara ya Kwanza tukio kama Hilo kutokea na likaonekana ni goli. Magoli ya Frank Lampard na Finidi George Kwa nyakati tofauti yamewahi kuthibitisha Hilo. Nenda Google utayalkuta. Lampard WC 2010 na Finidi kwenye penàlt shoot out dhidi ya Cameroon.
 
Teknolojia ya VAR ilikuwa bado haijaanza kutumika.
 
Wazazi wako either walichezea pesa zao kukusomesha ama ada yako ilipatikana kutoka kwenye kamari
 
Wazazi wako either walichezea pesa zao kukusomesha ama ada yako ilipatikana kutoka kwenye kamari
 
Ukiweka unazi pembeni unajua wazi kua hio miaka ya giza ambayo technology ilikua chini ufisadi ilikua mwingi mpaka leo tunalia na Manchester united kubebwa na marefa miaka iyo mtu ukileta ubishani ukatolea mifano ya 2020 kurudi nyuma nakuona hujui mpira

Kilicho kua kinatatua huu utata wa hili goli ni goal line technology TU na sio VAR kutokana na Angle za camera
Your browser is not able to display this video.
 
Simba kapigwa goal hiyo siku ,mpira ulidunda ndani na ukatoka nje
 
Angalia marudia ya penati za jana kati ya asec mimosas na es tunis penati ya nne upande wa mpigaji wa asec mimosas halafu uje na iyo fizikia yako
 
Akili za watu wa Simba zinafanana na viongozi wao... Kama Mangungu aliwaletea manzoki kwenye uchaguzi walampigia kura, try again akawaambia ameongea na Rais wa Fifa akamwambia et Simba inacheza vzr kma Madrid wakakenua meno, Aly Ahmed akawaambia muombe msamaha Ayuoub, Kajura akawaambia moja yaafanikio ni kufungua chanel ya whtsup yakacheka... Juzi mayele kuwatembelwa yamechekelea... Nalo ni mafanikio.... Kupitia haya yote... Lazima muwe na poor logic km hizi.
Kwan watu wanaofuatilia mpira sio Mara ya kwanza kufungwa Gori la hivyo, mpira unadundia ndani unarudi uwanjani na refa anaweka Kati.

N:B mechi ya Simba na yanga n trh 20 tunataka tuchokonowe tulipoacha tobo trh 5.🤣🤣🤣
 
Ila Africa tuko nyuma.

Yaani hadi sasa hvi video kuhusu lile goli inayooneshwa ni moja tuu.


Kuna wakati ukiangalia ile video inaonesha kama ni goli.
Kuna wakati inaonesha si goli ( kwa maana ya mpira kudunda kwenye msitari)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…