Kwa akili yangu nimegundua huyu alitaka kunitapeli

Mudugu

Senior Member
Joined
Mar 17, 2018
Posts
141
Reaction score
135
Kuna mwanamke nimekutana nae facebook
Alianza kwaniuliza naishi wapi, nafanya kazi gani nikamwambia,
Nae akasema anafanya kazi ya kutoa taarifa na kulipwa
Katika kampuni moja linaloitwa EDMARK
Akaniambia nikitumia audio ya dk 15 unaweza ukasikiliza? Nikawmbia ndio akaniomba namba ya Whatsapp nikampa akanitumia nikaisikliza wanasema wana frusa mbili za kujiunga katika kampuni yao kuna frusa ya miaka 40na ya miaka 4
Fursa miaka 40 yenyewe haiitaji mtaji unacho takiwa ni kushawishi watu kwenda kununua bidhaa za edmark unalipwa kwa asilimia 10 ya manunuzi wanayo fanya watu ulio washawishi
Yamiaka 4 yenyewe inaitaji mtaji wa 453600
Ukisha lipa hiyo hela wanakupa bidhaa za EDMARK na point 300
Nakulipwa kila mwezi asilimia 10 kila watu wanao fanya manunuzi ya bidhaa za hilo kampuni
Halafu ukipewa hizo bidhaa ukipenda unauza au unatumia mwenyewe.
Baada ya kusikiliza hiyo audio akaniuliza umependa frusa ipi nikamwambia ya miaka 40 akasema hiyo fursa sisi hatuna
Nikaona huyu nikimuuliza maswali atakimbia
Basi nikamwabia hata hiyo ya miaka 4 siyo mbaya naiweza naomba nielekeze jinsi ya kujiunga
Fasta akasema kama upotayari nikutumie forx namba?
Nikamwambia nikotayari tuma tu
Akanitumia namba ya voda
Akaniuliza unatuma lini? Nikamwambia mda wowote akasema nimesha waambia kuna mtu anajiunga leo
fanya haraka kutuma hiyo 453600
Niwahishe mizigo yako stendi nikutumie mie kwa njia ya Bus
Nikamwambia sawa
Mpaka sasa sijafanya chochote
Ananitumia sms kibao nimenyamaza kimya
Nikaamua hii niilete kwenu wana JF wenzangu muione nakufahamishana
Kama hiyo kampuni ya EDMARK
Ipo na inautalatibu huo
Mojakwamoja kwa akili yangu nimengundua huyo alitaka kunitapeli
 
[emoji535][emoji534][emoji3048][emoji531][emoji383][emoji383][emoji523][emoji258][emoji258]

*HAPA NDIPO TOKOMEZA UMASKNI NA JATU ILIPO. UKIELEWA SABABU YA WEWE* *KUJIUNGA NA JATU NA UKATEMBEA KWENYE HII RELI HAKIKA UTAKUWA MIONGONI MWA MABILIONEA WA JATU PLC KUFIKIA 2022 WALIOKUSUDIWA NA MPANGO MKAKATI WA KAMPUNI UNAOITWA VISION 2022.*

*Ukijiunga kwa 30,0000/ IWE CASH AU MKOPO, wewe unaitwa mwanachama mteja au mlaji. Utaanza kununua* *bidhaa za jatu kama mahitaji yako ya kila siku, yaani unga, mafuta na vinavyoendela kuongezeka.*

*Vitu hivyo utavipata toka kwa mawakala wa Jatu walio karibu yako. Yaani* *badala ya kununua bidhaa hizo kwa maduka tuliozoea, sasa utaanza kununua kwa maduka ya jatu.*

*Ukinunua utanunua kama mwanachama na utarekodiwa manunuzi yako, kwa kuweka namba* *yako ya uanachama, na majina yako kamili, na aina ya bidhaa sambamba na ujazo wake.*

*Mwisho wa mwezi report anazorekodi wakala huyo aziwasilisha ofisini na* *watajumlisha manunuzi yako yoote ya mwezi huo na kuangalia kwa manunuzi yako je? Umeleta faida kiasi gani* ? *Sasa hiyo faida iliopatikana kwa manunuzi yako, unarudishiwa 10% ya faida hiyo.*

*Unarudishiwa kama hela. Utatumiwa kwenye namba ulioiweka wewe wakati wa usajili. ( Halopesa, tigo pesa, mpesa n.k)*

*Hiyo ndio faida ya* *kwanza utakayoipata kwa kujiunga kwa 30,000 na kuhakikisha mahitaji yako yote unapata toka Jatu.*

*Faida ingine utakayoipata ambayo ndio kubwa zaidi ya mno* *ni;*
*Kuwashirikisha* *watanzania* *wengine( ndugu,jamaa, majirani, marafiki n.k) wajiunge na jatu na kuweza kupata mahitaji yao duka la Jatu na si kwingineko.*

*Nao watajiunga kwa gharama hiyo hiyo, na kunufaika kama nilivyoeleza hapo juu* ,, *SASA BASI, WALE WOOTE ULIOWASHIRIKISHA WAKINUNUA JATU NA* *KURUDISHIWA 10%YA FAIDA, KAMPUNI NAWE ITAKUPATIA 10% YA FAIDA YA MANUNUZI YA KILA ULIEMSHIRIKISHA,*

*Malipo haya utayapata kila mwisho wa mwezi kwa maisha yako yote na hata kurithisha wanao.*

*Kwenye kununua bidhaa(Masoko) kampuni ikaona* *itengeneze mfumo mzuri kabisa na wa kisasa (mfumo wa biashara ya karne ya 21). Ili kumuwezesha* *mtanzania anufaike kwa kile anachokula yeye na woooote atakao washirikisha kujiunga na Jatu.*

*Sasa basi, kama ukijiunga kwa hiyo 30,000/ unaruhusiwa kununua bidhaa zako* *kwa bei ya wanachama na kugaiwa 10% ya faida kwa kila kilo moja.*

*Je unanufaika vipi na matumizi ya wale wote uliowashirikisha?*

*Wale uliowashirikisha wakajiunga na jatu kwako wanahesabika ni kizazi chako cha kwanza* . *Nao wakiwashirikisha wengine, watahesabika kizazi chako cha pili, hawa nao* *wakiwashirikisha wengine, kwako watahesabika kizazi chako cha tatu............*
*Mfumo wa kampuni yetu ya Jatu umeandaliwa kunufaika hadi kizazi cha tano. Kama ifuatavyo;;*

*Kizazi 1- 10%*
*Kizazi 2- 8%*
*Kizazi 3- 6%*
*Kizazi 4- 4%*
*Kizazi 5- 2%*

*Jumla ni 40% ya manunuzi yako na mtandao wako wote, utakayo kuwa ukilipwa(Gawio).*
*_Angalia mfano wa chat hii[emoji116][emoji116]_*

*Ufafanuzi wa huo mchoro hapo juu uko hivi! Nao ni kwa mfano wa kadirio la chini la idadi ya watu utakao* *washirikisha kujiunga. TUNATUMIA MFANO WA WATU 10 TU BASI. NA WOTE MKAWA* *MNANUNUA BIDHAA MCHANGANYIKO WENYE KUFIKIA UJAZO WA KILO/LITA 100 KWA MWEZI.*
*NA PIA FAIDA NI SH. 300 KWA KILA KILO/LITA MOJA.*

*WEWE mtu 1: 10%. 100kg x 30/(300x10%) = sh.3,000/*
*KIZAZI 1 watu 10: 10%. 1000kg x 30/ = sh.30,000/*
*KIZAZI 2 watu 100: 8%. 10,000kg x 24/= sh.240,000/*
*KIZAZI 3 watu 1000: 6%. 100,000kg x 18/= sh.1,800,000/*
*KIZAZI 4 watu 10,000: 4%. 1,000,000kg x 12/= sh. 12,000,000/*
*KIZAZI 5 watu 100,000: 2%. 10,000,000kg x 6/= sh.60,000,000/*

*Sasa hapo Hayo ndio malipo yatakayo kuwa yakijitengeneza yenyewe kama utawashirikisha na ndugu zetu wanunue* *mahitaji yao yatu.*

*Utajitengenezea hadi jumla tsh 74,073,000/ kwa kushirikisha watu kumi tu ambao nao watashirikisha wengine 10 10 tu hivyo hivyo hadi kizazi cha tano.*


Jamani ni wewe tu kuamua kuanza lkn hali halisi ya mafanikio yako ndio hiyo.
*Jatu kula kwa faida*
 
Mimi ni mwanachama wa EDMARK, hakuna mtu anayejiunga na EDMARK kwa mtindo huo.
Iko hivi:
EDMARK wanauza bidhaa zao ila ukiwa mwanachama unauziwa kwa bei ya mwanachama. Sasa ukishakuwa mwanachama si kwa kutuma hela bali kwa kununua bidhaa zao za kiasi fulani na inaanzia laki na 80 na kuendelea kulingana na uwezo wako. Sasa hizo bidhaa unaziuza kwa bei ya soko au unatumia mwenyewe.
Mimi nanunua za kutumia kwa sababu kuzipata kama mwanachama ni bei ndogo kuliko kuzinunua kwa bei ya soko na kila manunuzi ninayofanya napata gawio kwa bidhaa nilizonunua na hela inaingizwa kwenye account yangu.
Kwa hiyo basi unaponunua nyingi zaidi unapata gawio kubwa zaidi na kama unaziuza unapata faida kwa sababu unauza kwa bei ya soko
 
Kumbe siyo kutuma hela nikununua bidhaa tu
 
Naona ume mfata adi uku ,,[emoji41]
 
Ndyo, Kuna demu alikuwa ananiconvice sana
mara anitumie picha akiwa Serena hotel
Nilicho mwambie...
Mafanikio ni safari ambayo kila mtu Ana njia yake, usitake kila mtu aufuate njia yako
Mkuu hapo ulimkatisha tamaa kabisa
Mimi nimeamua nimwangalie tu
 
Kama upo dsm fika ofsn kwao usimtumie hiyo pesa
 
huu ni utapeli wa kiwango cha phd ,na wewe naona unapigia debe watu wakaingizwe choo kama vile na wewe ni mmojawao hao jamaa
 
Mm niliwahi tapeliwa laki 7 mwaka 2016 na mdada anaitwa Rose Kowero Facebook,akanidanganya vifaranga vimekamatwa vimepigwa moto na atanipa refund,last year kabadili namba zake,beware na huyu mdada jamani asijeingiza mjini mtu mwingine.
Hebu mkuu tupe full stor ilikuwaje
 
UzuRI, wajinga huwa hawaishi mjini...hilo tu ndio linafanya biashara nyingi za kitapeli kuendela ku-operate fresh bila wasiwasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…