Jamani, kutokana na ushuhuda mwingi ambayo nimesikia toka kwa watumishi wa Mungu, nawashauri akina baba wenye watoto wafanye DNA test za watoto wao, hasa kama watoto kama hawafanani kabisa na baba yao, ila wanasingiziwa kufanana na babu wa babu au bibi wa bibi etc.
Nimegundua kuwa kuwa akina baba wengi wanalea watoto wasio wao kutokana na kuwaamini sana wake zao, na baadhi yao (akina mama) baada ya kumjua Mungu wanashindwa waanzie wapi kuwafahamisha waume zao. Unaweza kufanya test tu hata bila ya kumwambia mama yao. Mtoto ana haki ya kumjua baba yake wa damu.
Duh kwa ninavyompenda mwanangu halafu nikaambiwe sio wangu ntafia huko huko DNA room. Acha tu niendelee kuamini ni wangu
Kitanda hakizai haramu..................
Zamani, kuzaliana ilikuwa ni kawaida tu, na kulikuwa na amani sana. Nawafahamu watu kibao ambao wamekulia kwa mzee fulani, kumbe masikini si watoto wa mzee husika!
Ukianzisha huo mchezo hapa kwetu, utangulize kwanza nafasi za magereza na makaburi, maana watu watachinjana sana!
Kitanda hakizai haramu..................
Jamani, kutokana na ushuhuda mwingi ambayo nimesikia toka kwa watumishi wa Mungu, nawashauri akina baba wenye watoto wafanye DNA test za watoto wao, hasa kama watoto kama hawafanani kabisa na baba yao, ila wanasingiziwa kufanana na babu wa babu au bibi wa bibi etc.
Nimegundua kuwa kuwa akina baba wengi wanalea watoto wasio wao kutokana na kuwaamini sana wake zao, na baadhi yao (akina mama) baada ya kumjua Mungu wanashindwa waanzie wapi kuwafahamisha waume zao. Unaweza kufanya test tu hata bila ya kumwambia mama yao. Mtoto ana haki ya kumjua baba yake wa damu.
Ni jukumu letu kulea watoto wote walio kwisha zaliwa. Muda utumike kuhamasisha familia zenye uwezo wa ''adopting'' na ''fostering'' kufanya hivyo. ukipita kwenye orphanages zetu nyingi utaona umuhimu wa jambo hili. Na mifano ya watu waliotunzwa na wazazi wa kufikia ni mingi tu!
hata kama si mtoto wako wa kweli si atakuwa kapitia kila kitu through wewe kama huyo mtoto wa kweli kasoro mbegu tu? tafuta wa pili kama una wasi wasi sana lakini kama uko powa chukulia kama ume-adopt tu ndio maisha hayo.
nashauri kama maisha ni shwari nyumbani hakuna haja ya DNA. That should be considered only and only if unaona kuna conspirancy kati ya mtoto na Mama. Otherwise hakuna sababu ya kutafuta ugonjwa wa moyo.
Ukishamjua what next! Mie naona yaliyopita bora kuyaacha yaende km yalivyo ni kujipanga kwa yanayokuja. Hivi mtoto ana 15 yrs ukampime DNA kisa ushuhuda. Huyo ni vyema kumuona mwanao tu na kujipanga na wadogo zake.