Kwa akina Baba tu wenye watoto................

Kwa akina Baba tu wenye watoto................

hizo ni heresay tu kaka. ukitaka kufa haraka, anza hako kamchezo

Heresay? unaishi dunia gani rafiki? Kuna mada moja hapa ililetwa zamani na mwanamke akisema kuwa yamemtokea yeye na hajua aanze vipi kumwambia mume wake!!!

Kwa nini nife haraka? Kupima ni kama kupiwa ukimwi vile. Ni bora kujua. Kwanza haka kamchezo hakatazidi idadi ya watoto niliyonayo/nitakayokuwa nayo. Kila mtu huchukua maamuzi tofauti kwenye hali fukani, Mwingine atasema poa tu, namtunza ila niambie baba yake, mwingine atamfukuza mke na mtoto, mwingine atajinyonga.... Sasa wewe usifikiri hatua utakayochukua wewe ni sawa nitakayochukua mimi. Ukweli unabaki kuwa ni muhimu kujua watoto wote wewe ni baba yao.

hata kama si mtoto wako wa kweli si atakuwa kapitia kila kitu through wewe kama huyo mtoto wa kweli kasoro mbegu tu? tafuta wa pili kama una wasi wasi sana lakini kama uko powa chukulia kama ume-adopt tu ndio maisha hayo.
Huko ni kujiliwaza tu. Mtoto ana haki vile vile ya kumfahamu biological father wake na wadogo zake wengine
 
Mimi simo, na ninaamini wote ni wangu ili mradi waniheshimu na wanajua mimi ni baba yao. Kazi kwa mama yao aje awaambie mimi siyo baba yao wakiwa wakubwa nimeshawasomesha.....huo moto atauzima peke yake.

Hako kamchezo kwa kupimana pressure mimi simo. Imagine wewe unaambiwa kuwa yule mzee aliyelima vibarua, akakusomesha kwa shida, siyo baba yako. Bali baba yako ni yule tajiri katika kijiji au mji uliokulia na ulifanya kibarua kwake na alikuwa anajua kuwa wewe ni mwanae. Utamwelewa, si unaweza kuua mtu.
 
Seconded mia kwa Mia. Kama wewe si Biological father basi ni Legal father na inaruhusiwa/ inakubalika. Uwe na amani, Mtunze mtoto wako maana umeisha wekeza sana kwake tangu siku ya kuzaliwa hadi umri alionao; na yeye pia anakutambua kama baba tangu apate fahamu na hamujui baba mwingine. Kwa nini unataka kumvurugia mwanao maisha. Ebu fikiria unwe wewe leo umri wa Miaka 30 au 40 unaambiwa kuwa huyo unayemuita baba si baba yako bali baba yako ni fulani na ambaye aliuzini mama yako wakati akiwa kwenye ndoa ya huyo baba. Utajisikia je siku hiyo? Nasema hivi kama Mama alijichanganya hiyo imekula kwake. Haki ya Mtoto kumjua baba naamini ubaba unaokusudiwa si ule wa kutundika mimba na kujificha; naamini ni ule wa kuwajibika kulea na kumtunza mtoto. Huo ndio UBABA. Hayo mengine ni hadithi. By the way hizo DNA test nazo haziaminiki. Angalia Sinema ya Shades of Sin inayoendelea ITV utaona jinsi results zinavyoweza kuhujumiwa na iwapo ikakutokea unaweza ukakosa raha maishani mwako. Ya nini ufe mapema bwana! Kisa ... eti mtoto!!!!!!!!

Nataka niwe legal father kwa kuamua mwenyewe na sio kutokana na fate. Na wala sijasema kuwa nikifahamu hivyo then kuwa legal father kuna-cease. Kutaendelea tu kwani nimemlea kipindi chote. Hiyo definition ya UBABA kwa kweli siyo universal. DNA zinaaminika ndio maana zinatumika kama evidence kwenye mahakama. Poa tu kama mama ataniambia mimi sio baba yake. Kwanza nitashukuru sana na nitakuwa radhi kwa lolote. Labda Bakhresa ndio baba yangu LOL. Kufa mapema kutokana na kujua? Labda wewe rafiki ila si mimi.
 
Mimi simo, na ninaamini wote ni wangu ili mradi waniheshimu na wanajua mimi ni baba yao. Kazi kwa mama yao aje awaambie mimi siyo baba yao wakiwa wakubwa nimeshawasomesha.....huo moto atauzima peke yake.

Hako kamchezo kwa kupimana pressure mimi simo. Imagine wewe unaambiwa kuwa yule mzee aliyelima vibarua, akakusomesha kwa shida, siyo baba yako. Bali baba yako ni yule tajiri katika kijiji au mji uliokulia na ulifanya kibarua kwake na alikuwa anajua kuwa wewe ni mwanae. Utamwelewa, si unaweza kuua mtu.

Nitamwelewa fika. Period. Kama alinikataa nikiwa mdogo basi nitamjali yule aliyenitunza na vile vile nitawafahamu ndugu zangu wengine
 
eeeh wewe kweli umeamua .. una wasiwasi na mtoto wako na wewe?
 
Yote haya ni matokeo ya kutokuwa waaminifu katika mahusiano. Uaminifu uanzie mapema kabisa kabla hata hamjaoana. Nimesema hivyo kwa maisha ya kileo ambayo wachumba wanavunja kwanza amri ya sita kabla ya ndoa. Zamani ilikuwa ni marafuku kabisa kukutana kimwili kabla ya ndoa. Hii ilisaidia sana kuweka uaminifu na kama utamkuta binti si bikra basi ni lazima ajieleze. Sasa inakuwa ngumu na ndiyo maana haja za DNA zinajitokeza. Watoto wangu ni wangu 100%. Poleni, kwa wengine!!!
 
eeeh wewe kweli umeamua .. una wasiwasi na mtoto wako na wewe?

Bahati nzuri/mbaya sina mtoto kwa sasa. Lakini hii ni sera yangu hasa baada ya kugundua mwandani wangu ambaye nilimwamini vilivyo kumbe ana-cheat.
 
Back
Top Bottom