Wakuu salamuni.
Naombeni mwongozo wenu. Mke wangu amejifungua hvi karibuni, alijifungua salama na hali yake baada ya wiki moja na nusu alikuwa safi, na taratibu akaanza kunisogelea.
Kwa sasa ni wiki ya tatu tangu ajifungue, na tayari tumeanza kujamiana na kuondoa ugwadu. Mimi naogopa kwani nahisi anaweza kunasa mimba nyingine wakati bado tunahitaji kumtunza kijana wetu mpaka akomae vya kutosha.
Tumepanga akienda clinic ya kwanza, atumie moja ya njia za kudhibiti mimba ili kuepuka yeye kupata mimba soon.
Swali langu ni kuwa, Mwanamke kawaida anarudi kwenye mzunguko wake baada ya mda gani akisha jifungua?
Ni njia gani nzuri ya uzazi wa mpango ambayo haitaathiri afya ya wife wangu?
Nawashukuruni wakubwa