The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Japo neno kukinukisha linaweza kusababisha mashtaka ya uhaini uchwara, majirani zetu p
Pale chini, Madagascar wamekinukisha. Je, ni ajali kuwa kufanya hivyo kumekuja siku chache baada ya Kapteni John Charles Tesha kukinukisha?
Rais wao Andry Rajoelina amekimbia nchi baada ya kugundua kuwa the game was over. Kanali Michael Randrianirina anatamkwatamkwa kama mkuu wa mapinduzi haya. Rajoelina amepinduliwa kwa sababu ya vitu vya kawaida kama vile kukatikakatika kwa umeme na maji.
Makosa yake ni madogo ikilinganishwa na kwetu Tanzania ambako tunatekwa, tunauawa na kupotezwa na bado tunaimbiwa wimbo wa amani na wavunja amani. Kweli tunazo au hamnazo? Je, tatizo ni mfumo au woga wetu kama binadamu kama siyo ubabaishaji na kujipa matumaini?
Inakuwaje watu wachache tena waliomo kwenye ofisi zetu japo si kwa ridhaa zetu bali kuchakachua wanatuzidi akili na nguvu kama sisi siyo mataahira?