Kwa ambao hamjui siri ya mafanikio ya Yanga hii hapa

Kwa ambao hamjui siri ya mafanikio ya Yanga hii hapa

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Kuna mstari mwembamba unaotenganisha mchezaji anayejua kukaba na mchezaji anayejituma.

Yanga husajili wachezaji wanaojua kucheza katika nafasi zao pia wanaojua kukaba yaani ikimsajili mchezaji ambaye ni striker basi lazima awe na sifa kama za kiungo mkabaji.

Hivyo hivyo kwa wachezaji wengine ndio maana unakuta mchezaji mmoja anacheza namba nyingi mfano MAX, PACOME, AUCHO, MUDATHIR, LOMALISA, AZIZ KI, MZIZE, MUSONDA, MKUDE, YAO, JOB, BACA, KIBABAGE, GUEDE, n.k, hawa wote wanauwezo wa kucheza namba nyingi uwanjani pia wanasifa ya kiungo mkabaji.

Hapo jangwani mchezaji akikosa hiyo sifa hupewa dakika chache uwanjani mfano; OKRAH, SKUDU, FARID, n.k, ndio maana hapo Jangwani ni rahisi kwa namba 6 , 7, 11 au 10 kukuta ana magoli mengi kuliko namba 9 kwa sababu wachezaji wote wanauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja.

Msije kusema hatukuwaambia.
 
Sijaona SIRI yoyote hapo, unaelewa maana ya SIRI??
 
Back
Top Bottom