Kwa ambaye amewahi kuagiza gari kupitia autotrader

Kwa ambaye amewahi kuagiza gari kupitia autotrader

mzee wa manzese

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2012
Posts
670
Reaction score
216
Kwa wadau wote wa jamii forum napenda kufahamu jinsi ya kuagiza gari uingereza kupitia mtandao uitwao Autotrader,napenda kujua taratibu zikoje kuagiza gari huko na njia salama ya kutuma pesa,kwa yoyote aliyewahi kuagiza gari basi anifahamishe,gari ninayotaka kuagiza ni Toyota Avensis 1.8 cc vvti

nawasilisha
 
Autotrader Si mtandao wa kuagiza magari. Ni mtandao unaolist magari wanayouza watu na dealers. Hawahusiki kabisa na Mauzo mtakayouziana baina yako na muuzaji. Soma terms na conditions zao.
Kifupi ni kwamba, Autotrader wanafanya biashara ya kulist magari, kuuza insurance, kufanya HPI check nk... Ili kununua gari UK inabidi uwe na mtu unayemuamini, Akuangalizie gari unayoitaka kutoka Autotrader, itakuwa inauzwa na mtu binafsi au kampuni (dealer), aende akaikague, akiridhika nayo afanye malipo. Kisa akufanyie taratibu za kuipeleka bandarini na kukutumia gari yako. Autotrader hawahusiki kabisa, tena kabisa na asije akakuambia mtu kuwa unaweza kununua gari direct kutoka autotrader.
Wapo MaDealer wanaouza magari UK na wanaweza kufanya Export (hasa wa magari makubwa) Lakini ni "BUY AT YOUR OWN RISK", Wakikuliza huna pa kuwapeleka. Hata ukienda ubalozi wa uingereza kuuliza watakwambia hivyo.
Mchanganuo wa kuagiza gari kama avensis ni huu..
1: Chagua gari uliyoipenda
2: Mwambie Jamaa yako akaikague, na akiridhika nayo Ailipie
3: Atajaza V5 certificate (Log book), yaani kadi ya gari, na kusema kuwa anaisafirisha nje ya UK
4: DVLA watamtumia Logbook mpya inayoonyesha kuwa gari ina jina la mnunuzi mpya na kuwa imetolewa nchini...
5: Atakutumia documents zote za gari (mainly V5, na MOT certificate)
6:Utampa Clearing agent wako hapa, na atafata taratibu zote za kulitoa gari bandarini likifika, then gari unayo mkononi.

NB: Angalizo, kuna gharama za kutuma Gari Tanzania... kama vile Gharama ya kutuma hizo Doc za gari (V5 na MOT) kwa DHL...Ni kama £45, Kuna gharama nyingine ya kwenda kulikagua gari yaani kama mtu wako ataenda that means, atatumia usafiri, either binafsi au wa jumuia (treni, basi nk) na kuna gharama ya kulitoa gari lilipo mpaka kwa jamaa yako wakati anasubiri tarehe ya kulipeleka Melini... Mwisho kuna gharama ya kulipeleka melini na kulipia nauli ya meli... Kwa gari ndogo Meli mpaka Dar ni £750, na 4*4 ni £850, na kwa malorry inavary kulingana na Cubic metres...

Kwahiyo kama avensis umeona inauzwa £1500, ongeza kama £500 ya mambo mengine na £750 ya usafiri mpaka TZ... Hiyo 500 ya mambo mengine inaweza kupungua au kuzidi, kulingana na umbali wa gari ilipo na jamaa yako na umbali wa port, mfano kama jamaa yako anakaa Northumbaland na Gari ipo Southampton, basi ujue unaumia hapo.. ila kama lipo mile 20 kutoka kwenye post code yake, basi utapata unafuu...

Ni hayo tu.
Kama unataka msaada wa Kununua gari UK nipigie 0714881500.
 
Back
Top Bottom