Kwa anaefahamu dawa ya kufukuza Nyani

Kwa anaefahamu dawa ya kufukuza Nyani

Ha ha haaa sasa ikiwaingia machoni si unaweza baki unacheka tu!!!!
Tena hii pilipili nasikia hata Tembo anaikimbia!!!

Jamani tujuzeni hii mbinu inaonekana ni nzuri kopo la aina gani plastic au bati na ukitoboa chini si pilipil itamwagika? pia hiyo pilipili itawazuru vipi ndani ya kopo?
 
Bro Malila nitapataje mtu wa kunipigia risasi hawa wadudu wananiludisha nyuma sana mpaka nakata tamaa plz naomba msaada ata wa kuniunganisha na hao maliasili.

Ingia pm nikupe simu ya mzee akusaidie, yupo Mkuranga na ana bunduki halali.
 
NYOKA wa bandia wanasaidia. Mimi nilikuwa nafanya research yangu huko Mang'ola basi wakawa wananiibia chakula kila mara! Nikawauliza wenyeji wakanambia wanaogopa nyoka sana. Nikaja mjini nikanunua nyoka wa bandia mkuubwa tangu siku hiyo walikuwa wakija wanaliaa haooo wanaondoka!
 
Back
Top Bottom