Kwa anaejua kuhusu hizi mambo za BIASHARA YA MTANDAONI anieleweshe

Kwa anaejua kuhusu hizi mambo za BIASHARA YA MTANDAONI anieleweshe

Kuna jamaa yangu aliniambia kuna biashara nzuri nataka nikuunganishe upate hela bila kutumia nguvu nyingi, na wala hutumii ela nyingi,
Nikimuuliza biashara gani hasemi, siku akaniambia kama una mda njoo maeneo ya sinza kwa remy nikipeleke kwenye mchongo wa ela,

Nikafika pale kanielekeza alipo tukaonana kanipeleka nyumba moja tukaingia, nikaambiwa nikae mapokezi pale kuchungulia kuta za mle ndani naona mipicha ya watu wanapiga picha na magari, nyumba na mavitu kibao nkawa nahisi kinachoendelea,

Wakaja watano na jamaa yangu wa sita wanakaribisha kwa mbwembwe hao!!
Wakajitambulisha pale kisha nikaelekezwa chumba cha semina, kaja jamaa yangu na mtoa semina akaanza ngonjera zake, mara taasisi yao wana bidhaa ambazo huwezi pata popote duniani, wakati fb naona zinatangazwa(nilijua baada ya kuonyeshwa picha)
Wakasema ukinunua bidhaa 1 unakua umejiunga nao, nkawaambia sawa huku akilini najiambia wahakikishe tu hiyo bidhaa haizidi laki 3 ndio niliyokua tayari kupoteza, kumbe baada ya hapo unatakiwa na wewe ushawishi watu wawili wajiunge na wakijiunga unapata dola 250, na mtandao unavyokua ela inaongezeka (hapa nkahisi na ela yangu itakua imerudi, nitakula faida tuu)
Sasa kasheshe bei ya bidhaa sasa! Ya bei rahisi yenye sifa ya kukufanya uwe mwanachama sio chini ya milion 6, nilichoka nkawaambia narudi baada ya mwaka mpya nijiunge nao,
Sasa wakuu kama wapo humu wanaoijua hiyo biashara je ni kweli inalipa?ni kama kamari tu.

Sent using Jamii Forums mobile app


Usiingie kwenye huo mtego. Utapoteza zaidi unazopata pamoja na muda wako.
 
Biashara zoooote za networking waliopata faida na utajiri ni wale mataicoon wa mwanzo mwanzo kabisa wa hizo biashara lakini waliofatia hesabuni mko kwenye chungu cha umasikini.
 
Mi nilichobaki nacho ni kifurushi cha kusoma bachelor ya business administration with IT online, hapa nilipo natafuta wa kumpa hii package walau hata nifute machozi ya mbwembwe zao
 
Hahahaaaa, mi ntarudi tena pale ila sio kujiunga, kuna mdada mmoja mhaya pale alinivutia sana yeye ndio alinipa semina ya 2, mi nkawa namuwazia yeye tu hata sielewi anachoniambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rudi akushawishi kununua ndio hakupe papuchi.
Umejiunga JF miaka mingi na Kuna nyuzi nyingi zinasema ubaya wa Qnet Leo hii na ww unataka kuingizwa mkenge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom