Nenda kasome hiyo comb na utakuja kukumbuka maneno yangu. Hiyo sayansi unayopenda tafuta wenzio walioisoma halafu uangalie maisha yao: shida tupu! Katika nchi zenye uchumi duni kama ya kwetu wanaosoma sayansi wanaishia kujazwa misifa ya kijinga tu kuwa walikuwa "vipanga" nk lakini maisha yao ya baadae ni masikitiko. Kuna wachache sana wenye nafuu. Nchi ya uchumi wa udalali na uchuuzi (hakuna uzalishaji ambao ndio unaohitaji wanasayansi, wala wataalam wa tiba hawatambuliwi kila siku unasikia migomo utaishia hukohuko shauri yako). Uchumi huu wa udalali na uchuuzi unahitaji maarifa ya hiyo HGE unayokataa, hao ndio wako kwenye mabiashara, taasisi za fedha, BoT, TRA, stock markets nk na ndio wanaofaidi matunda ya nchi. Narudia, Dogo nenda form five hiyohiyo uliyopata utakuja kuyakumbuka sana maneno yangu,