INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

mimi na ona hz inabidi uchague zenye ubora kama vile transender mi ndo naikubali. Na pia sishauri mtu awe na 10TB kwa wakati mmoja bora awe na vipande kama vya 4TB.
Transcend ni nzuri kwa external HDD lakini sipendelei External kwasababu nazo zina changamoto zake,sipendi movable disk mimi kwasabbu najua madhara yake.

Ukifanya biashara ya Movie (kwa upande wangu) kutumia hard disk ndogo ndogo ni Loss kwanza Mother Board za mashine ninayotumia inabeba HDD (5) Mashine yenyewe ina port 6 nyuma + 4 mbele, Port za nyuma zote nimezijaza.

Port za kazi n za mbele tu,na HDD ya storage ndogo niliyonayo ni ya 6TB, so ukipga hesabu unaweza ukaona namna ambavyo ningekua nmetumia HDD za 4TB ingenigharimu na ningekosa pakuweka HDD maana mashine ingekua imejaaa.

Hapa ninavyoandika Mwezi ujao mwishoni Naenda pokea 20TB itakua imeshawasili,nataka Ondoa hizi 10TB zote niziweke pembeni nitumie 20TB tu,ifike hatua HDD zote zinakaa ndani ya mashine TU nisiwe na HARD DISK nnje ya Mashine hata 1.

Kwa mtu anaeanza Ni sawa ushauri wako wa HDD ndogo ndogo hizo za 4TB, lakini kadri unavyo expand na ofisi kuwa kubwa utakuja dharau hizo 4TB utaona n potezaji hela TU, Leo hii uniletee HDD ya chini ya 10TB sinunui hata uwe unaiuza bei ndogo kiasi gani.

Maana nitaiwekea nini? Muhimu ni kujua Namna ya Kutunza HDD zako na kuzifanyia monitoring kila wakati. Nina mwaka wa 4 sasa sijawahi kufiwa na HDD wala computer kuzingua,kna vitu ukishavielewa Changamoto za uharibifu unaziondoa kbsa kama sio kuzipunguza.
 
BEST HARD DRIVE kwa watumiaji DESKTOP ni WD, Hii ni Hard Drive bora sana kwangu kwa wakati wote,kukuta WD imekufa si jambo jepesi tofauti na kina bwana SEAGATE,HITACHI,TOSHIBA,DELL na wenzao..

Unapata WD 10TB unaiweka ndani ya Case ya ORICO ile ya 3.1 Utafanya kazi kwa raha sana na kwa uhuru bila hofu yoyote.

Linko
 
kuna kitu umenifungua ngoja nitarudi kwa swali moja.
 
na hz unazipata mkuu. maana naona iko pouwa.





ikiwa hv naona kama gharama ni nafuu. maana hapo ni 60TB net.
 
kwani wewe unazifata moja kwa moja uhindini na uturuki?
 
Anafanya vitu watu wavione vigumu ili kuwatisha watu!hii si sawa bhana
Vitisho viko wapi? Mil 4 unaona ni hela ya kutisha mtu? Hujawahi ishika au iona?Mbona ni biashara ya mtaji mdogo sana? si lazima kuanza na yote kama

huna anzia na kidogo ulicho nacho,Mkisikia watu wana biashara za mitaji ya mamilioni na nyie mnataka kuanzia kwenye mitaji ya mamilioni? Hamtofika MKUU na matokeo ndio hayo mnaona mnatishwa.

Unapoona biashara ya mtu yeyote ni kubwa,Ukaipenda uliza namna ya kuianza kwa udogo wake usitake kuanza ghafla ghafla kama yeye alipo maana hujui amefikaje pale alipo..

Ondoa mindset ya kutishwa/kuogopeshwa hamna mtu yupo hapa JF kutisha au kuogopesha wengine na ingekua hivyo watu wasingekuja kuuza magari na majumba humu,zingeuzwa baiskeli tu na kupangishwa vijumba vya mwembe yanga vya kodi 15,000.

Unapoona jambo zuri ukalipenda Tengeneza picha kulingana na hali yako uliyonayo kiuchumi,usitengeneze picha ya mtoa thread au muuzaji wa ile bidhaa,Utafanikiwa na hakuna utakachokiona kizuri utashindwa kukifikia.
 
Hii ofisi ya movie store naweza kuifungua kwa Dodoma??
Popote mkuu unaweza ifungua DODOMA hapo hapo nina plan yakuja fungua ofisi na ninavyoandika hapa wapo watu wenye movie store wakubwa tu hapo dodoma,tembelea ofisi zao utawaona wanachokifanya.

Kuna hawa wanajiita Cipherdot Series and Movies wapo mtaa wa Uhindini hapo nenda pale utawakuta utaona ofisi utaona uwekezaji uliofanyika.

Kuna huyu mwingine BABALAO mimi namuita hivyo na ndie ROLE MODEL wangu yeye anajiita BOBPAAK MOVIES huyu yupo mtaaa Mtendeni Street pale National Insuarance,Utawakuta hawa B.O.B wanajua biashara ilivyo na ukienda wagusa ukataka stock yao Bei utayotajiwa usipozimia basi unaweza kuzirai maana watu nmewatajia 4M wanahisi ni pesa ya kutishwa,sasa ukienda B.O.B bei zao n za mwana ukome.
 
Asante sana kiongozi,sasa mm ninayeanza nitawezaje kushindana na hawa miamba?
 
cypherdot huyu mmzee na mpata ana ofisi 4.
 
Asante sana kiongozi,sasa mm ninayeanza nitawezaje kushindana na hawa miamba?
Usijali mkuu halafu ni kwamba usichokijua si kila mtu hupenda kwenda sehemu nzuri na kubwa, hujawahi shuhudia mtu ana hela anaendesha gari zuri lakini hali hotelini yeye ni wa kwa mama ntilie tu?

Si kwamba hana hela ya hotel ila ameshaptia maisha ya chini sana kayazoea na anayaishi hayo maisha hata sasa akiwa na hela (lakini ana pesa) kwahyo mkuu usiogope wewe timiza malengo yako Fungua ofisi yako bila kujali nani katangulia au nani yupo pembeni yako.

Utapata wateja wako na wao watapata wateja wao ujue tu namna ya kufanya biashara, mwisho wa siku utarudi home na pesa na wao watarudi na pesa Wateja hawaishi wapo kila mahali.
 
cypherdot huyu mmzee na mpata ana ofisi 4.
Yeah kwa dodoma ndio baba lao, Huyo B.O.B kafungua dodoma juzi juzi tu hapa (2021) ila kwa moto wa B.O.B cipherdot atapwaya muda si mrefu maana B.O.B ndio VUNJABEI huyo ana sifa hela ipo hapo,ukiingia ofisi zake unaweza hisi upo ikulu kwa mama samia kulivyo kuzuri.

Huyo Kukunja 1M per day ni jambo la kawaida sanaaaa maana ana huduma kibao ndani ya ofisi zake hauzi movie peke ake,ana juice glass ni 10k na maudambwi dambwi mengine kibaooo.
 
hyo naipata iko kwenye kona, kuna moja ipo mipango siku hyo nili mkuta ana weka branding aise, itoshe kusema kuwa naheshimu sana movie store.
nilitaja movie 10 unique lakini mtu anaijua mpaka kero.
na ana mzigo wa kushata tokea 19951-2021 na ni movie zote mpaka latest.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…