Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asalaaaaam Ndugu zanguni, leo nimeamua kuja kuwatangazia vijana wote wanaotaka kufungua Biashara ya Movie Store yani kwa movie za kiswahili na Movie za Kizungu Karibu sana nipo Nauza Mzigo kwa bei ya Jumla kwa wafanyabiashara wanao anza au wanaotaka kuongeza stock za Ofisi zao.
mimi ni mfanyabiashara wa kuingiza movie na nyimbo kwa wateja nina stock yakutosha kabisa kwakijana yeyote ataehitaji mzigo ambayo akienda kukaa ofisini kwake Hatokosa 30,000 kwa siku huyu ni mgeni kabisa.
Hamna movie inayojulikana midomoni mwa watu Sina, japo sina Movie zote duniani au Series zote duniani lakini ni mtu ambae mteja akija na List ya 10 movies Zitapatkana 8 ztakosekana 2, Akija na list ya 5 series Zitapatikana 4 itakosekana 1, nadhani mtakua mmepata picha ya movie nilizokua nazo.
Bei elekezi ni kama zifuatazo
Kwa Mtu anaetaka kuja kuchukua Mzigo wangu wote yani tunacopy and Paste Kila kitu changu
Bei ni 4M yani milioni 4
Mahitaji yako : Unatakiwa uje na Hard Disk 60TB (Sixty Telabytes) hapo utaweza kubeba kila nilichokua nacho hutoniacha hata na trailer 1 yani utakua umebakisha kunichukua Mimi TU.
kwahiyo huko ulipo tafuta HARD DISK zako kisha njoo Nione,hiyo bei ni ya SOFT MOVIES haijumuishi gharama za Hard Disk, HDD tafuta unapojua wewe za bei utayoafikiana huko na wauzaji.
Huyo ni muuzaji Mkubwa wa Movie,Kwa wale wauzaji wanao anza anza (kama nilivyoanzaga mimi)
Kujaza 4TB Naijaza kwa 300,000 kwahiyo kila 4tb kujaza ni 300,000 hapo kazi itakua ni kwako kwenda kufanya kazi,Movie ni nyingi sana,kila movie ya kingereza ipo na kiswahili yake.
kadhalika na kwa series kila series ya kizungu ipo na ya kiswahili yake, Korean Drama,Animation na kila takataka inayohusiana na BURUDANI basi utaipata kwangu.
Karibuni vijana wenzangu mjikwamue, sio lazima wote twende shamba kulima kwa wale wenye mitaji na wana uelewa wa computer Biashara hii ni nzuri na isiyo na chembe ya mashaka.
Makadirio ya Faida kwa Mtu kama mimi sio chini ya 100k per day na kwa week ends sio chini ya 200k,Kwa mtu anaeanza kwa kujikongoja kongoja kwa siku hatokosa 10k kutegemeana na stock atayokua nayo.
Lakini kwa mtu anaejua location nzuri na ambae anauwezo wa kulenga eneo zuri Hata ukiwa na 4TB kupata 30k ni jambo la kawaida uzuri wateja wa movie sio wachaguaji, Mtu akitaka movie lets say OLD GUARD na stock yako hauna hiyo movie, Una uwezo wa kumwambia na kumuonyesha list ya movie zenye story kama ya OLD GUARD ukamsimulia na akaichukua, kwahiyo mteja wa movie akiingia ofisini kwako kuacha hela labda wewe mwenyewe ushindwe kumshawishi.
Natumaini vijana mnaopenda maendeleo na pesa basi nipo hapa kwa ajili yenu,Lakini pia yawezekana wewe unafanya hii kazi ila huna movie nyingi unataka kuongeza, Karibu sana nipo wazi ofisini anzia saa 5 asubuhi mpk 6 usiku.
Kwa wale wa movie za kina DJ MURPHY,DJ MACK (mzee wa Achecheeeeee) zote zipo miendelezo ya kila Jumatatu huwa nauza File lenye miendelezo yote ya wiki nzima kwa sh. 10,000 Njooo na 10k yako nikupe file lenye miendelezo yote ya wiki husika.
Movie zangu ni HD sinunui movie za kwenye Ma cd kisha nika copy kwenye mashine yangu,Movie zangu za dj murphy nazifata direct ofisini kwa Murphy ananiwekea kwenye external yangu, Movie za achecheee nazifata kwa Mack ananiwekea soft copy.
Sipendi nunua movie za kwenye Ma cd kwasababu mostly zinakua zimeconvertiwa zimepoteza ubora wa Picha, Season zote hadi za kihindi za kina VASCO DJ, MSATI, KONDE BOY, na wengine wote picha zao nilizonazo ni zile HD tunaita 720p to 1080p
Kwa series za kizungu na movie za kizungu Resolution ya movie zangu 80% ni 1080p kwa wateja wenye Flat 65inch 4k movie zao pia ninazo kwahyo ni uchaguzi tu,Mteja wa reja reja ukitaka movie resolution yyte kulingana na TV yako unapata.
Watu wengi nawasikia wakilalamika kuwa movie za kutafsiriwa zina quality mbovu, hii si kwa movie zangu Week end hii hapa inakuja Delivery Pia nafanya.
BEI YA REJA REJA
Single movie 1000 (iwe ya kiswahili,iwe ya kizungu)
Series English 2000
Series swahili (1000 vipande 25) complete isiyozidi episode 60 sh 2000
Korean Drama 2000 (drama isiyozidi episode 20)
Korean Drama zinazozidi episode 20 hata ikiwa episode 23 bei ni 3000,
Korean Drama zinazozidi episode 50 bei ni 5000 (mostly hizi ni zile historical)
Korean Drama za kutafsiriwa Bei ni 2000 (isipozidi episode 60)
Korean Drama za kutafsiriwa zilizozidi episode 60 (bei ni 30 episode 1k)
Karibuni sana Ofisi ipo Kwa Msuguli, kama ukitokea ubungo unashuka kituo KWA MSUGULI kama ukitokea stand ya Magufuli unashuka kituo Kwa msuguli.
Kwa biashara zaidi na mahitaji na maulizo binafsi karibuni PM.
Delivery wateja wa DAR naleta movie hadi mlangoni ila tu movie uchukue sio ya chini ya 30,000, hata kama hauna external/Flash utanitumia list mimi nitaweka list yako kwenye external yangu kisha nitakuja ku copy kwako.
Asanteni sana Movie ni Biashara Movie ni Burudani Changamkieni Fursa wapenda Burudani lakini wapenda Biashara Nipo kwa ajili yenu Pia.
Rudia kusoma thread utaelewa Mkuu,swali lako jibu lipo kwenye thread.Mkuu iyo hela unanipa na external kabisa auu
Watu hawa waheshimu waingiza miziki barabarani wanahisi ni vijana waliokosa kazi za kufanya kazi yao n kudownload nyimbo na kuingizia wateja (as if kudownload ni bure)offisi ya kawaida ila ukiambiwa gharama zake noma sana.
kweli kabisaWatu hawa waheshimu waingiza miziki barabarani wanahisi ni vijana waliokosa kazi za kufanya kazi yao n kudownload nyimbo na kuingizia wateja (as if kudownload ni bure)
Heshima kwa jamii ya Tanzania kwa wafanyabiashara watu hawana kbsa,dharau na kejeli ndio zimewajaa watanzania walio wengi.
Halafu kuna watu humu wanakuja na ofa za Laki 4 mfano wa kina Nazi Ignition na wenzao wanaochukulia poa Movie store wanahisi ukiwa na Internet TU basi unaweza miliki Movie store na hutokosa movie yoyote wanafurahisha haswaa.hyo naipata iko kwenye kona, kuna moja ipo mipango siku hyo nili mkuta ana weka branding aise, itoshe kusema kuwa naheshimu sana movie store.
nilitaja movie 10 unique lakini mtu anaijua mpaka kero.
na ana mzigo wa kushata tokea 19951-2021 na ni movie zote mpaka latest.
hahahahahahaha umenifurahisha balaa.Halafu kuna watu humu wanakuja na ofa za Laki 4 mfano wa kina Nazi Ignition na wenzao wanaochukulia poa Movie store wanahisi ukiwa na Internet TU basi unaweza miliki Movie store na hutokosa movie yoyote wanafurahisha haswaa.
Root anakwambia ukiungwa na faiba ya 200k tu kazi kwishaaaa hahaha bwana Ruti ananipa amani sana nikisoma koment zake.
Hivi ukipata wateja wawili tu na Faiba yako ya 200k lazima utoke jasho hadi la ulimi?
Mteja wa kwanza anakwambia anataka Korean Drama inaitwa KING GWANGWAETO
Mteja wa pili anakuja anakwambia anataka Turkish Series inaitwa ERTUGUL
Ukiwapata wateja hao wawili tu na faiba yako ya 200k Jasho litakutoka mpaka masikioni,Mizigo yote hiyo ina download episode moja moja wateja washasubiri washachoka washasepa😅
Mkuu una uhakika hazipo au wewe ndio huna machimbo? Mimi sijihusishi na biashara hii ila ni mpenzi sana wa movies, series na music.. na hii biashara nitakuja kuifanya siku moja maana nina machimbo ya kila aina ya hizi movies, na kingine mkuu bei zako upo juu sana, ila niskupangie kaka ni maamuzi yako mkuuAchilia mbali Laki 5 hata uunge bando la 1M huwezi pata movie zote mtandaoni kwanza hilo unatakiwa ulifahamu mkuu?
Kuna movie ya MB 500 tu ipo mtandaoni ila kuishusha hata ukae wiki nzima haimalizi kushuka, server iko slow bin konokono..
Ukiwa na movie store sio kila movie utaipata mtandaoni utapitwa na wakati sana, mtandaoni utapata hizi za sasa hivi common ambazo kila mtu anazo.
ili mteja anase kwako anatakiwa akija umpe collection ya CHUCK NORIS umpe collection ya Bruce leee kuna zile old movie ambazo kuzipata si rahisi.
Indian movie mteja akwambie umpe DISCO DANCER umpe JANWAR au series za INDIA yani hata uweke bando la 1m ukitaka kupata movie zote labda udownload kila movie, jambo ambalo halitakiwi kwenye movie store.
Movie store its all about Selecting whats trending kwa wakati huo, sasa wewe unadownload peke ako utadownload movie ambazo hutokuja ziuza, utadownload hata 100TB lakini Useless Movies hamna ataekuja ziulizia wala kuzitaka.
Ukiona unauziwa Movie za kufanyia biashara ujue umesaidiwa kupewa CREAM yani zile movie ambazo mteja akiingia tu ofisini kwako ataiulizia, JE ukipewa bando la TB 10000 Utazijua movie wateja wanazopenda kwakujifungia ndani kudownload kwa link?
Kwakua umesema utakuja anza hii biashara,nakusubir ukianza usisahau kurudia kusoma hii comment yako nimekuifadhia hapa.Mkuu una uhakika hazipo au wewe ndio huna machimbo? Mimi sijihusishi na biashara hii ila ni mpenzi sana wa movies, series na music.. na hii biashara nitakuja kuifanya siku moja maana nina machimbo ya kila aina ya hizi movies, na kingine mkuu bei zako upo juu sana, ila niskupangie kaka ni maamuzi yako mkuu
Kuna list ngumu si rahisi rahisi,mimi kuna wateja nawambiaga wasije ofisini kama hawajanitumia list ya movie wanazotaka wiki 1 kabla.hahahahahahaha umenifurahisha balaa.
umenikumbusha kuna sehemu nilienda kuchukua movie nikataja list 5 aise unaweza ona huruma.
Huyu jamaa ana tabia mbaya sana,kanikumbusha mbaliii🤣kuna mwingine nika mwambia aniweke kingsman 2, aise nafika home nakuta korea na ni chafu balaa, nilikasirika sana.
Kumbe Vunjabei ndo BOB PAAKYeah kwa dodoma ndio baba lao, Huyo B.O.B kafungua dodoma juzi juzi tu hapa (2021) ila kwa moto wa B.O.B cipherdot atapwaya muda si mrefu maana B.O.B ndio VUNJABEI huyo ana sifa hela ipo hapo,ukiingia ofisi zake unaweza hisi upo ikulu kwa mama samia kulivyo kuzuri.
Huyo Kukunja 1M per day ni jambo la kawaida sanaaaa maana ana huduma kibao ndani ya ofisi zake hauzi movie peke ake,ana juice glass ni 10k na maudambwi dambwi mengine kibaooo.
Nimekupa hiyo,itunze kwenye notebook, YES ndie sio wa kufukuzana nae huyo mtu unaeza buruza ulimi.Kumbe Vunjabei ndo BOB PAAK
Sikuwahi juaNimekupa hiyo,itunze kwenye notebook, YES ndie sio wa kufukuzana nae huyo mtu unaeza buruza ulimi.
huwezi jua kirahisi na wanaojua ni sisi wenye movie store,Mimi nawajua wamiliki wa ofisi za movie store sio wafanyakazi zao.Sikuwahi jua
Maana yake Boss kawawekea kiwango cha pesa kila sikuhuwezi jua kirahisi na wanaojua ni sisi wenye movie store,Mimi nawajua wamiliki wa ofisi za movie store sio wafanyakazi zao.
na Ni wale wa Movie Store kubwa kubwa Tu ndio tunaojuana,Huwezi mkuta mmiliki wa Movie Store ofisini (ni nadra sana) ndio mana huwezi kujua nani mwenye nayo.
Na chat hapa JF ila huwezi nikuta hata siku 1 ofisni ni nadra sana kunikuta nimekaa ofisini,Mteja nitaempata ONLINE namuelekeza tu ofisini anaenda kukutana na vijana.
Camera zilizofungwa kwenye hizo ofisi hadi mezani unazijua mzeee? Mbali na kamera kuna chawa wambea kiasi kwamba hata ufinye 1000 tu unasemewa. Kosa 1 (huna kazi)Maana yake Boss kawawekea kiwango cha pesa kila siku