INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

Turkish series zipo za kutosha mKUUU tukianza na Dingi lao la historical Ertugul

ukiachana na ertugul kuna list kadhaa ya Hot Turkish Love stories kwa Historical series zote zipo boss...

Bir Umut Yeter (Action Kali sana)

Sampiyon (action iliyo emotional sana) Hapo utakutana na single father aliemlea mwanae aliezaliwa na mama mtu kufariki,Baba mtu hana kazi yani Kama machozi yapo karibu hii sio movie ya kutazama.

ICERDE (mashine ya Action)

Kurulus Osman (Historical)

Sanger (Historical)

Ask mantik itikam (Love story)

Teskilat (Hatari na Nusu)

Soz (Millitary Action Mchaka mchaka mwanzo mwisho kutana na bwana Agaaaaaaah na kina Yavuuuz)

ADA MASALI (ukitaka enjoy Week end Anza na hii)

Kis Gunes (hatari sana)

Marasli

Ariza

AND many many many more Turkish zote zilizopo nikimuwekea mteja hawezi ishia njiani, Turkish series ni nzuri wanajua sana.

Wale wa kutafsiriwa DJ murphy ana Turkish series za Hatari sana

Seen
Sanger
Alparslan
Soz
Icerde
Marasli
Teskilat
Kis Gunes
Sampiyon
Ferhat

Hiyo ni list ya DJ MURPHY moja ya ma DJ BORA kwa wakati huuu anae ingiza maneno kwa ufasaha akitafsiri movie safi kabisa No matusi, no lugha za kihuni DJ mstarabu na SMart..

Wapenzi wa Turkish karibuni

Wapenzi wa Philipines karibuni

Mataifa haya mawili Philipines na Turkish ni special case wana movie kali sanaaa ila wateja wengi hawajajua kuwa kuna vitu wana miss kwa kutoangalia movie toka sehemu hizi mbili, nadhani kama ni drama n love story philipines ni habari ingine.
Una La Revenge ile ya Mexico English version?
 
Una La Revenge ile ya Mexico English version?
Hapana sina,Movie ambazo mteja anahitaji na sina kwenye Store Huwa nazi download mteja unaifata movie yako kesho au jioni kutegemea na umekuja saa ngapi na speed ya internet kwa siku husika.

Lakini huwezi fika ofisini ukakosa movie labda uwe huna subira ya kusubiri movie yako ishushwe,kama uvumilivu upo basi hata uje na movie list mkeka mzima utapata movie zote.

Karibu
 
Kwa staili hii vijana hawakupigi kweli au umeweka camera?
Napigwa sana na najua napigwa,Muhimu hesabu yangu ya kila siku ifike,Nina Chat ambayo inaonyesha kila siku hesabu inahtajika sh ngapi.

Sijaweka kama Boda Boda,wao wanaambiwa hesabu sh 10,000 kwa siku,Mimi kwangu ipo tofauti.

Mfano wa Chat ni kama huu (hzi bei n mfano)

J3 = 100,000 (kiti ki 1 @50k)
J4=150,000 (kiti ki 1 @75k)
J5=200,000 (kiti ki 1@100k)
ALH=200,000(kiti ki 1@100k)
IJUM=200,000(kiti ki 1@100k)
JMOS=300,000(kiti ki1@150k)
J.PILI=300,000(kiti ki1@150k)

Nikisema kiti ki 1 maana yake ofisi zote zina computer mbili yani vijana wawili kila mmoja na mashine yake,na kila mmoja ana hesabu anatakiwa afikishe asipofikisha watajua na mwenzake wanasaidianaje jioni nikirudi nipate hesabu kamili.

Kijana atae ingia kazini anajua kabisa leo J3 boss akija kuchukua hesabu anakuja fata kiasi kadhaa, ninapoenda jioni siulizi A wala B nawambia tu wanipe changu.

wao wapate wasipate changu wananipa,na haijawahi tokea siku wakashndwa kunipa,Ofisi ina Generator umeme sio kigezo cha kukosa hesabu yangu.

Wanapiga pesa refu zaidi najua, maana wafanyakazi wangu Siwalipi mishahara wanajilipa wenyewe na ofisi zangu zinaenda,Japo kuibiwa nishaibiwa sana mpk hapo nilipokuja na huu utaratbu wakuweka hesabu.

Maana najua siku gani zina hela na siku gani hazina hela Najua.
 
Mkuu mi nataka nifungue hii mkoa muda baada yakama. Miezi miwili hivi... nilitembelea ofisi ya cipherdot kuchukua series jamaa huwa mnatumia siftware gani...

Je kwa mwanzo ntahitaji nini na nini mkuu kwamtaji wa kama milioni nne hivi
 
1.Computer (Yenye Window Ten na SSD 256GB atleast)
2.STORAGE DEVICES (hard disk internal plus external)
3.Mzigo wa kazi

Mengine ni mbwembwe zako kulingana na malengo yako ktk hii kazi huko mbeleni,hivyo malengo yako ndio yatafanya gharama zpande au zishuke,4M unaweza anza na maisha yakaenda. (bila mbwembwe)
 
Ombi
Kwa yeyote mwenye office au atakayefungua office ya Movies kwa dar,kijana wenu nipo hapa naomba Fursa ya kukaa golini,mwaminifu na naijua computer vizuri ,pia nitakusaidia katika kuandaa matangazo ya kuvuta wateja hasa wa online. kwa ujuzi wangu wa Photoshop,After effects na social media .najua nitaongeza value kubwa sana katika biashara yako. Tafadhalini sana wakuu [emoji120]
 
Napigwa sana na najua napigwa,Muhimu hesabu yangu ya kila siku ifike,Nina Chat ambayo inaonyesha kila siku hesabu inahtajika sh ngapi.

Sijaweka kama Boda Boda,wao wanaambiwa hesabu sh 10,000 kwa siku,Mimi kwangu ipo tofauti.

Mfano wa Chat ni kama huu (hzi bei n mfano)

J3 = 100,000 (kiti ki 1 @50k)
J4=150,000 (kiti ki 1 @75k)
J5=200,000 (kiti ki 1@100k)
ALH=200,000(kiti ki 1@100k)
IJUM=200,000(kiti ki 1@100k)
JMOS=300,000(kiti ki1@150k)
J.PILI=300,000(kiti ki1@150k)

Nikisema kiti ki 1 maana yake ofisi zote zina computer mbili yani vijana wawili kila mmoja na mashine yake,na kila mmoja ana hesabu anatakiwa afikishe asipofikisha watajua na mwenzake wanasaidianaje jioni nikirudi nipate hesabu kamili.

Kijana atae ingia kazini anajua kabisa leo J3 boss akija kuchukua hesabu anakuja fata kiasi kadhaa, ninapoenda jioni siulizi A wala B nawambia tu wanipe changu.

wao wapate wasipate changu wananipa,na haijawahi tokea siku wakashndwa kunipa,Ofisi ina Generator umeme sio kigezo cha kukosa hesabu yangu.

Wanapiga pesa refu zaidi najua, maana wafanyakazi wangu Siwalipi mishahara wanajilipa wenyewe na ofisi zangu zinaenda,Japo kuibiwa nishaibiwa sana mpk hapo nilipokuja na huu utaratbu wakuweka hesabu.

Maana najua siku gani zina hela na siku gani hazina hela Najua.
Shukrani sana chief
 
Mkuu hujawahi kuwaza hii ya kuuza online hasa kwa link ama telegram, maana naona hii kama ipo vizuri pia, hasa kwa hizi movie zilizoingizwa maneno ya kiswahili. Maana huwa unanunua mzigo kila wiki wa ofisi, hivyo inakuwa kama unakaba kote. Mfano huyu castillarmovies jamaa yeye anauza online tu promo zake naziona kwenye pages mbalimbali za public figures.
 
Back
Top Bottom