Kwa Augustine Okra Yanga SC nawapa "Big Yes" lakini kwa Saimon Msuva nawapa "Big No"

Kwa Augustine Okra Yanga SC nawapa "Big Yes" lakini kwa Saimon Msuva nawapa "Big No"

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Naam! Kuna tetesi nyingi zinavuma kuwa Augustine Okra atasaini Yanga Sc katika dirisha dogo na kelele za Saimon Msuva kutua Yanga Sc.

Hii ni kwa wenye kufuatilia na kupenda football hakuna atakaeweza kupinga talanta ya Bwana mdogo Agustine Okra the magician left footer.

Okra ni winga namba 11 lakini pia namba 7 huwa anagusa kipindi yupo Simba SC niliona talanta yake kwa kweli Kasi na uwezo wa kudribo mpira uwezo anao tena mkubwa.

NALIA NGWENA nilisikia kuwa anatua Yanga Kama tetesi zinavyodai kwa uchezaji wake na Kasi yake nawapa Big Yes viongozi wa Yanga Sc Kama ni kweli wamemsaini huyu winga.

Tujikumbushe kidogo kwa Saidoo ntibazonkiza alitoka Yanga Sc na kwenda Geita na kuibukia Simba sc, mashabiki wa Yanga SC walimkejeli lakini alichokifanya Simba sc ni kikubwa mpaka Sasa ni chaguo la kila kocha anayekuja Simba SC.

Ujio wa Agustine Okra the magician left footer ndani ya Yanga Sc siyo mbaya japo mashabiki wa upande wa Simba sc wanaongea na kuzomea kuwa Okra ni mlevi, Mara kashuka kiwango hayo ni maneno tu na tukija upande wa uwanjani (talanta) Nina Imani kubwa okra Atafungwa midomo ya wapiga Kelele.

Nasema "Big No" kwa Msuva kwa kuwa Msuva kiuhalisia kashuka kiwango labda aje Yanga Sc kisiasa na nguvu ya madalali kuwa kubwa (wazee wa ten percent) Ila kwa upande wa kiwango ni Bora hata tuisila kisinda.

Nawasilisha hoja.
 
Kama kwa okra swala la kushuka kiwango yalikua ni maneno tu kwanini nakwa msuva nako tusione ni maneno yako tu.
 
Back
Top Bottom