Kwa baadhi ya wafanyabiashara, kwanini simu yenye Lipa number hamuwaachii wafanyakazi wenu dukani?

Kwa baadhi ya wafanyabiashara, kwanini simu yenye Lipa number hamuwaachii wafanyakazi wenu dukani?

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Malalamiko kuhusu baadhi ya wafanyabiashara kuwachelewesha wateja wanaolipia bidhaa kwa kutumia namba za malipo (Lipa Namba) yameibuliwa na mtumiaji wa Instagram, Malisa G, aliyewataka wafanyabiashara kuboresha mifumo yao ya kupokea na kuthibitisha malipo.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Malisa amesema baadhi ya wateja hulazimika kusubiri madukani baada ya kufanya malipo kwa sababu wafanyakazi wanahitaji kupata uthibitisho kutoka kwa wamiliki wa biashara kabla ya kuwaruhusu kuondoka na bidhaa walizonunua.

Chapisho la instgram la Malisa G lina ujumbe ufuatao :
Kwa baadhi ya wafanyabiashara, kwanini simu yenye Lipa number hamuwaachii wafanyakazi wenu dukani? Je hamuwaamini au mnaogopa wataibiwa? Hakuna kitu kinakera kama umemaliza kununua bidhaa, unalipia kwa lipa number, halafu unaambiwa subiria tupige simu kwa boss aconfirm kama ameona muamala wako.

Boss anapigiwa simu mara 3 hapokei. Unapewa kiti ukae usubiri mpaka boss "atakapojisikia" kupokea simu. Unatamani kurudisha bidhaa ukanunue kwingine, lakini ndo ushalipia, ukirudisha bidhaa hela yako unapataje? Kwahiyo unakua mpole unakubali kupotezewa muda mpaka huyo "boss" atakapojisikia kupokea simu na aconfirm kwamba ameona muamala wako ndipo uruhusiwe kutoka. Kwa kifupi ulikua "detantion" kwa muda. Bila "boss" kuconfirm hutoki.

Aisee inaboa sana. Kwanini usiache simu dukani ili mteja akilipia muamala uonekane hapo hapo?? Au kama huwaamini wafanyakazi wako, kwanini usiunganishe simu ya dukani ipate notification? Siku hizi unaweza kuunganisha simu mbili kwa lipa number moja. Hela inakuja kwenye simu yako lakini dukani kwako wanapata notification. Kwanini msifanye hivyo badala ya kuwaweka wateja "detantion" bila sababu? Hamuoni mnapoteza wateja kwa ujinga?? Customer care bongo miyeyusho sana.!
 
juzi kiduka cha mangi mtaani hapa kimenuka kisa lipa namba hiyo hiyo, mteja kaona lipa namba kalipa , anashangaa mangi amsikilizi ,kuuliza anaambiwa hujanipa ,akamwambia nimelipa lipa namba, mangi anasema ngoja nimuulize Boss kama kapata , kumbe ile lipa namba hana ,anayo boss mwenyewe
 
Back
Top Bottom