Kwa bahati mbaya mke ameshika ujauzito tena

Kwa bahati mbaya mke ameshika ujauzito tena

Kinacho kusumbua ww ni ego yako.

Swallow your pride accept it. Isitoshe ni mke wako, mambo ya kuonekana primitive ni ya kizamani, kwani kuna chochote wanakusaidia?

Ww una hofu kumtia mimba mke? Wenzako wana tia mimba michepuko na mke ni mzazi na bado hawa panic
Af mshaaaaaambaaaa tuuu.

Hana anachokijua
 
I'm too weary, yaani tuna mtoto wa miezi karibia 9 sasa, ila mke wangu jana kapima ujauzito baada ya kuhisi uchovu, kwa masikitiko makubwa ni mjamzito. Nitaficha wapi sura yangu Mimi? Naheshimika mno inakuwaje wakijua mke wangu mjamzito tena?

Yaani nionekane primitive Mimi? Nafikiria nimuambie tutoe ila navuta muda, mke wangu ndio chanzo cha yote, ananipa show huku mzunguko kausahau, na mimi siku reason!

Nafikiria nimuambie akaitoe, naombeni mawazo yenu Wanajamvi!! Ndo nadhalilika hivyo
Nendeni Hospital.


Huko ndio watakuwa na majibu ya uhakika.

Kama hiyo mimba itakuwa risk kea hicho kinachonyonyeshwa basi wataitoa.

Otherwise mtazaa tu.
 
Mimba ni binadamu ambaye yupo tumboni kwa mama yake.
Anaweza kuwa binadamu hai au binadamu mfu,binadamu hai ni yule ambaye anacheza tumboni na mfu ni yule ambaye hachezi tumboni.

Hakuna roho nusu,roho kama roho ni kamili.

Haya maamuzi yako ndio ukatili kwa sababu uko tayari binaadamu anayeendelea kutengenezwa asije duniani kwa sababu tu binadamu aliyekuwepo atakosa kunyonya maziwa kwa muda wa mwaka mmoja.

Wakati huo huo binadamu huyu unayemhofia ameshafikisha miezi sita kwa maana anweweza akupewa chakula kingine na maziwa hivyo hatokuwa mtegemezi sana wa maziwa kiasi kwamba ukatae asitengenezwe kiumbe mwingine kwa sababu huyu aliyekuepo atakosa maziwa.

Huu ni ukatili kwa kiumbe ambacho kinategemea kuja duniani.



Mtoto wa mtoa mada ameshafikia miezi 9 kwa maana ni zaidi ya 6months hivyo anaweza kupewa supplementary foods sio kwamba atategemea maziwa tu pekee.

Hii maana yake unataka kusitisha kuja binadamu duniani kwa sababu binadamu wa duniani atakosa maziwa ambayo hayategemei kwa 100%.

Lakini pia mtoto huyu unayemhofia haina maana kwamba akikosa maziwa atakufa ataendelea kuishi ila kuna nutrients ambazo ndo atazikosa kidogo kutoka katika maziwa ya mama.

Sasa kutoa mimba kwa kuhofia madhara kwa mtu mwingine madhara ambayo hayaleti mauaji huo utakuwa sio uungwana kaka mokaze.

Ndio maana hata maulamaa wameruhusu kutoa mimba hata ikiwa imepuliziwa roho endapo tunahofia huyu mama atapoteza uhai wake.

Mfano mama ana ectopic pregnancy ambayo kimsingi haiwezi ikafikia miezi hata saba lazima itarupture tu,katika hali kama hii maana yake tunahofia kifo kwa mama endapo mimba ikikua.

KUTOA MIMBA KISHERIA YA DINI NA DUNIA HASA KWETU TANZANIA IWE KWAMBA HIYO MIMBA KUBAKI KWAKE KUTALETA MADHARA YA KUUA MTU MWINNGINE AU MATATIZO MAKUBWA SANA KIAFYA KWA WALIO HAI.

Mtoto wa mtoa mada asiponyonya maziwa ya mama na akaendelea kupata vyakula vingine huku mimba ikiwa inaendelea ATAKUFA ? ATAPATA MADHARA GANI MAKUBWA ?



Mkuu ni kweli maziwa ya mama yatabaki kuwa maziwa ya mama,lakini sio lazima kabisa kwa mtoto kwamba anyonye maziwa tu lazima apate vyakula vingine.

Kwa sababu katika vyakula vingine kuna nutrients ambazo pia ni muhimu katika kila nyanja ya mwili.

Kama vile mayai ya kuku,kwale,samaki,supu ya kuku,viazi mbatata,maziwa ya foruma,ndizi mbivu,maji n.k

Haya yote mtoto akiyatumia pia anakua vizuri sana kiakili sio kwamba maziwa pekee ndio yanaleta akili wakati Mungu kaumba mbadala wa vyakula vingi sana.

Hivyo hakuna sababu kuubwa ya kuharibu kiumbe kinachotengenezwa kwa kuhhofia hoja ya maziwa kaka mokaze.


Kila hoja uliyoijibu ninayo majibu yake mujarabu, lakini
Mimba ni binadamu ambaye yupo tumboni kwa mama yake.
Anaweza kuwa binadamu hai au binadamu mfu,binadamu hai ni yule ambaye anacheza tumboni na mfu ni yule ambaye hachezi tumboni.

Hakuna roho nusu,roho kama roho ni kamili.


Kaka, ndio maana nikasema hii maada mzizi wake wote upo hapa kwamba mimba ni "BINADAMU".
Na inashikiliwa kwamba mtu akitoa mimba tayari anakuwa ni muuaji wa binadamu, kaka, mimi narudia kusema kwamba Kutoa mimba bila sababu za MSINGI ni uhalifu lakini sio uhalifu kama ule wa kuua binadamu huru (an individual), sio sawa na kumpiga mtu risasi, shoka nk hadi akafa.

Binadamu anaanza KUTENGENEZWA kutokana na udongo (vyakula tunavyokula akina baba), kisha zinapatikana mbegu ambazo zikiingia kwa mama ndipo mchakato mwingine unaendelea; mbegu inakuwa pande la damu ambalo linakuwa pande la nyama ambalo nalo linakuwa mifupa ambayo nayo huvikwa nyama na baadaye huumbwa kiumbe kingine (Roho), hiyo ndiyo baraka ya Allah mbora wa waumbao.

Kwa habari nyoofu Soma Qur'an (23:12-14)

Na maneno hayo yanapata support kutoka katika aya zingine aya zifuatazo:--

"Na kumbuka mola wako alipowaambia malaika hakika mimi nitaumba mtu kwa udongo utoao sauti kwa matope meusi yaliyobumbwa."

"Basi NITAKAPOMKAMILISHA na kumpulizia roho yangu ndipo umwangukie kumtii. (Qur'an 15:28-29).

Hapo sasa utaona kwamba mimba ni mchakato wa kumpata mtu kamili, angalia hayo maneno; "nitakapomkamilisha na kumpulizia roho", anapopuliziwa roho ndipo anakuwa mtu kamili na ndipo anazaliwa/anakuja duniani, huyo sasa ndiye mtu/binadamu.

Sasa huwezi kusema mimba ya mwezi mmoja ni binadamu sawa na wewe au mimi.

Katika Qur'an kuna aya kadhaa zinaanza na; "Yaa bani adama---" ku tu adress mimi na wewe tunaoisoma Qur'an na sio ku adress hao unaowaita binadamu-hai na mfu waliomo matumboni ambao hata hawajui watazaliwa lini, na isitoshe mimba inao uhai tangu ikiwa bado mbegu kutoka kwa baba, ikifa tu basi mara moja mchakato mzima wa kumtengeneza mtu tumboni unasimama na mimba inatoka (miscarriage).

Mtu/binadamu ni nani??--- ni yule mwenye roho na nafsi inayojitegemea, anakula, anakunywa, anapumua hewa ya nje nk, haitaji msaada kama jinsi mimba inavyohitaji msaada kutoka kwa mbebaji, mbebaji akinywa sumu wote mimba na mbebaji watakufa au akinywa pombe na mimba nayo italewa pombe na kinyume chake mbebaji akila chakula safi na mimba nayo hushamiri.

Mama mjamzito akifa na kuzikwa wala haisemwi kwamba wamezikwa binadamu wawili lakini Mama akifa na kichanga chake hapo tunasema wamekufa binadamu wawili na watazikwa katika makaburi tofauti.

Lengo hapa ni kuwapa picha mjue mimba ni mchakato wa kumpata binadamu na kutoa mimba sio sawa na kuua mtu/binadamu (an individual).


Kwanza tuishie hapo baadaye nitakuja kwenye mengineyo.
 
Kaitoe kunusuru afya ya huyo mtoto (mtu kamili) wa miezi 9, hiyo mimba haina thamani kuliko huyo mtu.

Usitoe… acha mtoto azaliwe. Unahofia watu kwani wanakutunza wewe.
Mimi nilijikuta nna mimba tena mtoto akiwa na miezi 7, sasa hivi wanakimbia kule. Tena miezi 7 ya kuzaa kwa C-section nikawa na mimba ingine. Nilichanganyikiwa ila alizaliwa
 
I'm too weary, yaani tuna mtoto wa miezi karibia 9 sasa, ila mke wangu jana kapima ujauzito baada ya kuhisi uchovu, kwa masikitiko makubwa ni mjamzito. Nitaficha wapi sura yangu Mimi? Naheshimika mno inakuwaje wakijua mke wangu mjamzito tena?

Yaani nionekane primitive Mimi? Nafikiria nimuambie tutoe ila navuta muda, mke wangu ndio chanzo cha yote, ananipa show huku mzunguko kausahau, na mimi siku reason!

Nafikiria nimuambie akaitoe, naombeni mawazo yenu Wanajamvi!! Ndo nadhalilika hivyo

Pole kwa hofu Mkulungwa01 ila sasa ondoa shaka. Wewe andaa mazingira mazuri kwake na watoto. Wale vizuri, mke apate usaidizi wa kutosha na mapumziko

Wapo wanaopata uja uzito mtoto akiwa na siku 60 huyo wenu mwenye siku 270 ni mkubwa kabisa

Tafuta pesa kwa wingi ya maziwa, chakula bora cha watoto na mama, diapers, miundombinu itakayomrahisishia mama watoto malezi na mengine.

Mungu awatangulie
 
Kuua nini??, kuua mimba au kuua mtu??, kuua mimba kwa kunusuru uhai wa mtu kwa sababu za msingi sio dhambi kwani mtu anayo thamani kubwa kuliko mimba.
Tangu day 1 Mimba ni uhai na ni roho
 
Back
Top Bottom