SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ujio wa Kocha Benchikha katika Simba kipindi hiki unadhihirisha kuwa Simba ina jeuri ya pesa ya kumleta kocha au mchezaji yoyote inayemtaka kutoka ardhi hii ya Africa. Kama tumeweza kumleta kocha mwenye profile kubwa hivi aliyetoka kushinda mataji mawili kati ya matatu makubwa Africa kwa level ya vilabu, tunashindwa nini kupata wachezaji wazuri? Pamoja na mpira usioridhidha ulioonyeshwa na Simba hasa kipindi cha pili katika mechi dhidi ya ASEC Mimosas weekend iliyopita, lakini mchezaji wa ASEC alipohojiwa angependa kuchezea timu ipi ya Tanzania bado aliitaja Simba.
Wengi tumekuwa tunalilia wachezaji wazuri wenye viwango ila matumaini yetu mengi yamekuwa hayafikiwi. Ni wakati umefika mdudu anayekwamisha wachezaji wazuri wasije pale Simba au wakija wanashindwa kuperform aondolewe. Inawezekana huyo mdudu siyo mtu ila mfumo unaotumika wa kutafuta wachezaji na kuwasajili, inawezekana ni mfumo wa uendeshaji timu, inawezekana ni mazingira ya kambi, inawezekana ni vifaa duni vya mazoezi, inawezekana ni mfumo usio mzuri wa afya na matibabu, inawezekana ni uhaba wa staff wa kutosha kwenye benchi la ufundi na ufuatiliaji wa karibu wa hali za wachezaji na shida zao.
Wakati umefika tufanye maamuzi magumu. Thank you za dirisha dogo na dirisha kubwa lijalo inabidi zitufurahishe ila tunachotaka zaidi maingizo mapya yatufurahishe zaidi kwa watakachotuletea uwanjani. Sidhani kama Simba inahitaji wachezaji wa gharama kubwa kihiiivyo, labda mmoja au wawili ila wachezaji wa gharama za kawaida wenye viwango na damu inayochemka mbona wapo tu Afrika yote nzima hii? Huko Senegal na Ghana kuna madogo kibao tu wanapiga mpira hatari. Jeuri ya pesa tuihamishie sasa huko mpaka wasemeee.
Ushauri wa mwisho, ni vizuri tuanze kuzingatia suala la lugha na huu ushauri niliwahi kuutoa zamani. Leo hii tuna kocha mwarabu asiyeongea kiingereza kizuri, tuna wachezaji wa Kitanzania wasiojua kiingereza vizuri wala kiarabu, tuna wanaozungumza kifaransa wasiojua kiswahili, kiingereza vizuri wala kiarabu. Tujaribu kupunguza hii changamoto kwa kuangalia lugha za asili za wachezaji na makocha. Bila hivyo tuhakikishe tuna mkalimani kama Cedric Kaze katika benchi la ufundi.