Kwa CCM ni ipi dhana ya kuwa uchaguzi kwa watia nia?

Kwa CCM ni ipi dhana ya kuwa uchaguzi kwa watia nia?

Mafanikio 07

Member
Joined
Jun 18, 2019
Posts
57
Reaction score
37
Habari wakuu!

Kila siku Kuna habari mpya nchi Tanzania kutokana na Taifa linaenda kuingia katika uchaguzi wa viongozi.

Mnamo 20/07/2020 uchaguzi kwa WATIA NIA ya kugombea upande wa chama Tawala ulianza na mpaka hivi Sasa unaendelea, lakin Jana mida ya saa 1 nimepata kuona kapost Fulani inaeleza jinsi mchanganuo wa kupata Wagombea utavyokuwa unaelekea.

Ukweli ni utaratibu kwa CCM kuwa na machujio tofauti Ila Cha kujiuliza kwa Nini mtu akishachaguliwa na wanachama mwisho wa siku mnaenda kumkata mbele wakati mliweka uchaguzi huru kwanini mnaingilia maamuzi ya wanachama!he hakutokuwa na harufu ya Bias?kwanini kusiwepo na mwenendo wa kutoa vigezo labda Kama elimu,na sifa zengine hatuoni kuwa tunachukua maamuzi ya watu??

Mwisho niseme tu, CCM ijitathmini katika hili huu ni ukandamizwaji wa katiba.

Mwisho niwapongeze washindi wa swali katika majimbo pia kuwapa pole walioshindwa.

#TuijengeTanzania.
 
Unaweza ukawa na sifa zote za kuwa kiongozi mzuri na mjenga hoja mzuri sana lakini wanachama kwa sababu zao binafsi au za kimazingira wasikuchague.

Hii kazi ya kuchagua wakiachiwa wanachama pekee hakuna masikini atakayetoboa. Wewe siumeona mpaka watu maarufu wameangushwa sembuse masikini.
 
Kama kuna mtu alikwambia kwenye hicho chama kuna mambo ya uzalendo alilidanganya,chama hiko kila mtu ana angalia maslahi yake kwanza,watamchagua alieawapa chochote,kama ataleta maendeleo au hatoleta wao haiwahusu ilimradi chao walishakula.Chukua chako mapema
 
Back
Top Bottom