Hahaha..........Umenikumbusha mbali wakati hili daraja likijengwa tuliambiwa liko modern na bora kuliko yale tuliyo nayo Kenya. Nilijaribu kuelezea wabongo hiyo ni excitement too lakini wapi.
Kwa swala la uhandisi, mara nyingi vitu zikijengwa Afrika hujengwa tu vizuri ila kinachokosekana ni miundombinu ya kusupport hicho kilichojengwa. Kwa mfano unapojenga Daraja kama hili, unafunika ardhi nyingi kwa saruji na lami na kuzuia maji ya mvua kupenyeza kwa hivo unaachilia maji mengi kubaki kwa surface ya ardhi. Suluhisho la hili ni kujenga drains kubwa zaidi ambazo majiji mengi ya Africa hayana. Halafu kingine kando ya drainage system isiyoweza kusupport hiyo infrastructure, majiji mengi ya Afrika ni machafu na hayatilii maanani utupaji wa taka mahali kunakofaa - makaratasi mengi huingia kwa hizo drain na kuzifanya ziwe ndogo zaidi. Ndio maana kila kukijengwa barabara kubwa kwenye majiji ya Afrika, kunatokea na hii shida ya flooding. Ile nashukuru serikali ya kenya kwa kuban makaratasi ya nylon maanake yalichangia sana kublock drains mjini. Mwaka uliopita kulikuwa na mvua nyingi na hakukuwa na flooding yoyote Nairobi kama inavyokua miaka mingine.