Kwa flyover ya Tanzania kufurika hivi, kosa la nani kiutalaam

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna hii picha inasambaa kwenye mitandao, inaonyesha jinsi flyover ya Tazara pale Tanzania ilivyofurika baada ya mvua ya siku moja, najiuliza hivi hii Afrika ina maana wachoraji wa miundo mbinu/ architectural designer huwa wamelala au ni umbumbubu tu.


Cc NairobiWalker
 
Namshukuru Mungu nafsi ilikataa kuelekea njia hiyo leo.
Tanzania tuna ulipuaji wa miundo mbinu ya barabara kuliko tunavyodhani
 
Ngoja ya ubunge interchange ije ibonde wananchi hako cha mfugale ni kadaraja tu.
 
Miradi ya Magufuli ni ya hovyo kabisa.
Viwango vya ubora havizingatiwi, yeye siasa mbele quality and standards will come after.
Kwenye Hostel za Chuo Kikuu mabweni yalipotoka nyufa akamleta engineer wake wa Kinyakyusa, akatuletea msamiati EXPANSION JOINT.
Sasa flyover imekuwa Beach, nadhani sasa itaitwa Beach Kidimbwi Flyover
Lile boat lake la MV Dar es Salaam, safari ya kwenda Bagamoyo ilichukua zaidi ya masaa nane na ilikula mafuta mengi sana, kwa aibu akawapa wanajeshi
 

Hahaha..........Umenikumbusha mbali wakati hili daraja likijengwa tuliambiwa liko modern na bora kuliko yale tuliyo nayo Kenya. Nilijaribu kuelezea wabongo hiyo ni excitement too lakini wapi.

Kwa swala la uhandisi, mara nyingi vitu zikijengwa Afrika hujengwa tu vizuri ila kinachokosekana ni miundombinu ya kusupport hicho kilichojengwa. Kwa mfano unapojenga Daraja kama hili, unafunika ardhi nyingi kwa saruji na lami na kuzuia maji ya mvua kupenyeza kwa hivo unaachilia maji mengi kubaki kwa surface ya ardhi. Suluhisho la hili ni kujenga drains kubwa zaidi ambazo majiji mengi ya Africa hayana. Halafu kingine kando ya drainage system isiyoweza kusupport hiyo infrastructure, majiji mengi ya Afrika ni machafu na hayatilii maanani utupaji wa taka mahali kunakofaa - makaratasi mengi huingia kwa hizo drain na kuzifanya ziwe ndogo zaidi. Ndio maana kila kukijengwa barabara kubwa kwenye majiji ya Afrika, kunatokea na hii shida ya flooding. Ile nashukuru serikali ya kenya kwa kuban makaratasi ya nylon maanake yalichangia sana kublock drains mjini. Mwaka uliopita kulikuwa na mvua nyingi na hakukuwa na flooding yoyote Nairobi kama inavyokua miaka mingine.
 
Baada mkataba wa ajabu na indo power (korosho) tunashuhudia mapungufu mengine ya kitaaluma.
 
Good analysis.
 
Mbona hawajaweka drainage. Unaona sasa ukumbavu ya kupewa vitu vya bure? Afadhali kitu umelipia mwenyewe.
 
inasemekana kuwa kampuni toka Kenya imepewa kandarasi ya ku supply nyambizi......

hongera jpm!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…