Kwa Fungu la Bilioni 1.3 kwajili ya kuwaendeleza ndugu kijijini ni bora kuwapeleka shule au kuwawezesha kibiashara?

Kwa Fungu la Bilioni 1.3 kwajili ya kuwaendeleza ndugu kijijini ni bora kuwapeleka shule au kuwawezesha kibiashara?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Mhusika kajisevu sevu ana fungu la Bilioni 1.3 kalitenga kuendeleza huko kwao

Options ni mbili

A. Kuwachukua wanaofaulu vizuri form 4 Kuwasomesha chuoni mpaka wanapomaliza degree. sharti ni kusomea kozi za sheria, Engineering, udaktari, ufamasia na uhasibu.

2. Kuwapa mikopo isio na riba kuanzia milioni 10 hadi 50, kigezo mtu awe na uzoefu kwenye biashara na muhimu zaidi nidhamu ya pesa.
 
Kama una kampuni ya kuwaajiri wakimaliza masomo ok.

Vinginevyo utatengeneza umaskini zaidi.

Wanasema kijana msomi asiye na ajira na mtaji huwa maskini zaidi kuliko kijana asiye msomi.
 
Mhusika kajisevu sevu ana fungu la Bilioni 1.3 kalitenga kuendeleza huko kwao..
Rafiki , ukweli ni kuwa kizazi cha kitanzania hatujajaaliwa na hatujafunzwa nidhamu ya pesa.

Nikupe kongole kwa kiasi cha hela hicho ulichokusanya na hivyo nikuombe kuwa unaweza kufanya yafuatayo, kukusanya hicho kiasi itoshe kusema wewe umeshajinasua kwenye utumwa wa pesa na sasa una nidhamu ya pesa .

Ila sikushauri kwenda kijijini kwenu na kuwapa watu hiyo hela sijui mkopo , sijui kuwasomesha ila nakushauri nenda kijijini kwenu kawasalimie hata mwaka mzima , kaa na watu wa huko uzione interest za walio wengi kwenye kutengeneza pesa.

Kaa karibu na mizimu yako na mwisho utapata kitu ambacho ukoanzisha basi utaweza kuwaajiri ndugu zako hapo walio na elimu na wasio na elimu.

Hii itawafanya kukishukuru kizazi kwa kizazi maana utakuwa umetengeneza mfereji wa hela kwa wanakijiji huku na wewe ukinufaika pia.

Kuliko kuwekeza kwa wanadamu maana hatutabiriki.

Kudos sana mwamba.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Wazungu wengi na warabu msaada wanaoleta huwa wa ki taasisi mfano kuwajengea shule, hospitali nk.

Wewe Unahitaji kuwa na taasisi imara itakayowawezesha kupata skill sets and mind transformation kwa mambo yote utayoyafanya.

Binafsi sijapiga hatua yoyote ya kuweza kuwasaidia home ila plan zangu kama zitakwenda sawa nitakwenda kuanzisha mashsmba ya kisasa ya ya chikichi, ndizi na ufugaji wa samaki kisha nitawafanyia incubation.

Incubation maanake ni uatamizi. Ni kama kuku unamuatamia anatotoa unamkuza kifaranga na kukua kisha anamwacha aendelee na maisha yake.

Wachaga na wakinga na waha forget about Infuans na Arabs wanafanya incubation katika primitive way ila imeleta matunda.

Mimi nakushauri ukitoa mitaji wafanyie incubation mpaka pale unapokuwa umejiridhisha kuwa kijana kakomaa.
Naye unamrithisha hizo skill na inakuwa circle.

Tujikumbushe kuwa raisi kikwete alileta mabilioni ya kikwete vijijini lakini yalipotea, watu waliishua kulewea na kuhonga, na hata TASAF nao wamepeleka miradi vijijini kakini imefeli.

Hata nawe unaweza kufeli ukifuata njia za kikwete na TASAF.

Unaweza kujifunza namna ya kufanya incubation. TZ haijatumika sana ila wenzetu wanefanikiwa.
 
Back
Top Bottom