gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Diamond akiwa na Wema na binamu yake aitwae Romeo
Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ile inayoitwa movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, Temptations haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.
Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao, alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
Not the easiest relationship Ive ever had..but its the most intresting! When Im down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I love you baby, aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.
Source Gumzo la jiji:
Ninachojiuliza mimi hivi ni kwamba vijana hawajajitambua?? na je swala la moving from one partner another, kwa mbwmbwe ni ustaa ama ndio ujana??
anyway sina nia mbaya ya kuajdili personal life ya mtu lkn nataka tu tujifunze kwamba we still have long way to go especially kwenye kuwafanya vijana wajitambue. Kukosea kupo sana lkn unapogundua kwamba umekosea simama ifute endelea na safari na usirudi tena kwenye utelezi uliokudondosha.