Kwa hali aliyonayo Bernard Membe, Kikwete alikuwa sahihi huyu hakustahili kupeperusha bendera ya CCM hata kidogo

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Mhe. Kikwete alikuwa sahihi kukata jina la Membe 2015 kuwa mgombea urais kupitia CCM kwa kweli hana ushawishi wala mvuto wowote kwa watanzania, Kama kikwete angefanya kosa la kumpitisha huyu mtu 2015 Kisha apambane na Lowasa leo tungekuwa tunazungumza Lugha nyingine kabisa kwenye siasa za Tanzania.

Viongozi wa CCM wamekuwa wajanja sana hata uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 walipoona ameanza chokochoko wakamtimua mapema ili asiharibu mipango ya uchaguzi kumbe waliona mbali Bernad Membe hana ushawishi hata kidogo wa kuwa kwenye nafasi kubwa Kama ya urais.

Hana ushawishi ndani ya chama wala nje ya CCM, kwa kifupi watanzania wamempuuza huyu mtu.

Kiuhalisia ukiacha mtaji mkubwa wa wanachama walio nao CCM zaidi ya mil 15 lakini ukweli ni kwamba mgombea urais anapaswa kuwa na mvuto na kukubalika na hata watu wa vyama vingine na wasio na vyama jambo ambalo Magufuli kwa asilimia kubwa analo japo wengi hawataki kutamka wazi hilo.

Sasa kwa Membe yeye hana vyote viwili kwa pamoja. Najiuliza tu hii amsha amsha ya Tundu Lissu ndio angekutana na mtu dhaifu Kama Membe ccm wangeangukia pua mapema Sana.

Mhe. Zitto umekosea umechukua garasa umeshindwa kufikia akili ya Mbowe 2015 hata kwa 2%.
 


Hakuwa Kikwete

Fuatilia kwa kina utajua nani alifanya hiyo kazi
 
Membe yupo vizuri na ni mtu anayeonekana unajua kupanga Mambo kwa ufanisi, sema inaonyesha wazi kamuachia Lissu ajitangaze zaidi, kwa jinsi Wantanzania tulivyo, Membe angekuja na swaga za Lowasa za kulipia wasanii na kuwalipa ulipo tupo Sasa hivi tungekuwa tunasema Membe kila Kona, anaoneka kabisa kwamba ni mtu wa vitendo kuliko maneno na hana jaziba kwenye kujibu hoja.
 
Kikwete hakuwa sahihi Membe ndio alikuwa chaguo lake, ile hali ya wajumbe mule ndani ya mkutano mkuu baada ya Lowassa kukatwa ndio ilimlazimu Kikwete amuondoe Membe ili arudishe amani ndani ya ule mkutano, vinginevyo kama wale wajumbe wangekubali kuwa makondoo Membe ndie angekuwa Rais wa JMT leo hii.
 
Waulize Bawacha walivyokuwa wanamshadadia hahahaha
 

Kwa taarifa yako sio Magufuli wala Membe hakuna mwenye mvuto, wote wanategemea nguvu ya vyombo vya dola. Hata Lowassa angekosea ile 2015 aende chama kingine nje ya cdm, angekuwa kama Membe hivi sasa. Zito alikuwa anang'ang'ania kuungana na cdm maana anajua fika kwa huku bara, cdm ndio chama chenye wafuasi wa upinzani wa kweli. Bahati nzuri wanachama na wafuasi wa Cdm tulisema hatutaki tena taka ngumu toka ccm.

Halafu acha upotoshaji usio na tija yoyote, ccm haina wanachama 15m, kama ina wanachama wa kweli hawavuki milioni 3. Nguvu za vyombo vya dola pekee na tume isiyo huru ya uchaguzi, ndio huficha ukweli huu kuwa hadharani. Kama ccm ingekuwa na wanachama wangalau milioni tano tu hai, isingekuwa inatagemea tume ya uchaguzi kuwapitisha bila kupingwa. Cdm sidhani kama ina wanachama 1.5m, lakini ndio chama chenye wafuasi wengi hasa vijana, ila ni wasio na kadi, mfano halisi ni mimi mwenyewe. Mimi sio mwanachama wa Cdm, lakini ni shabiki wa kutupwa wa Cdm, na watu wa aina yetu ni wengi sana. Hivyo mtu yoyote akiwa ccm atategemea mbeleko ya vyombo vya dola, na akitoka asipoelekea cdm automatically anapoteza mvuto.
 
Mbona Mwalimu hakuwafukuza bali alitumia upendo kwa kuwasubirisha??????
 

Sasa Magufuli ana ushawishi gani? Magufuli ni mnyampala wa barabara tu ndiyo maana baada ya kupewa uraisi bado anajua yeye ni mnyampala wa barabara tu.

Membe ni bonge la raisi sema alitakiwa ahamie ACT tokea 2016. Anachokifanya sasa in maandalizi ya uchaguzi was 2025 maana kwa uchaguzi wa mwaka huu Magufuli kuachia madaraka labda damu imwagike kwanza.
 

Kikwete hakumkata Membe acha uongo! Membe aliingia hadi Tano bora kisha akakwama halmashauri Kuu kura hazikutosha
 

Membe angojee uchaguzi wa 2025? Wakati huo atakuwa na miaka 70+, kwa umri huo atafanya nini?
 
Hicho chama kilianzishwa na kina Kikwete, Membe, Mwigulu nk kama backup ya ccm kupambana na cdm. Hivyo Membe ni mmoja kati ya wamiliki. Sasa mmiliki akichagua nafasi utakataa?
Kumbe[emoji44]
 
Amwage damu na hao jeshi lake la akiba anaenda the Hague
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…