Uchaguzi 2020 Kwa hali hii, CHADEMA wanajiandaa kuvunja Muungano

Uchaguzi 2020 Kwa hali hii, CHADEMA wanajiandaa kuvunja Muungano

Hawezi naana Lisu kamwe hawezi kuwa rais
 
Ubishi wa maccm ndo utavunja Muungano,

Muungano unatakiwa kulindwa na Katiba ambayo imetengenezwa kwa maridhiano na imepipigiwa Kura ya maoni,

CCM hawamtaki Katiba Mpya ya selikari tatu, wakati tuna vyama vingi

Sasa ikitokea znz akishinda act Bara akashinda CDM Katiba hii mbovu ya ccm inasemaje.
Automatically Muungano hakuna
 
Sijajua kwanini huu uzi bado upo, una maneno mengi ya kichochezi
 
Hapana Muungano usivunjike lakini kama kuna vitu haviendi sawa basi viwekwe sawa ili kila mhusika wa Muungano atendewe Haki.
Ccm wamekuwa wakiahidi kutatua kero za muungano miaka na miaka lakini kimya, hata hao wapinzani hawajaahidi kuuvunja bali wameahidi muungano wa manufaa kwa pande zote
 
Faida za Muungano zimebakia ni za ki-academic au kihistoria. Watu wanaogopa kuvunja Muungano utadhani kabla ya 1964 kulikuwa hakuna Tanganyika au ZNZ.

Tunaichelewesha bure ZNZ kupata maendeleo kipitia kipaumbele vyao na raslimali zao. No uwongo kusema tunawaenzi Nyerere na Karume kwa kudumisha MUUNGANO kwa kuwa siku zote walitaka identity ya ZNZ kama Taifa isipotee. Nyerere kwa ninavyomuelewa angekuwa hai angetambua kwamba sababu za kuwa na MUUNGANO wa Serikali 2 zimepitwa na wakati kwa hiyo angeshauri ifanyike referendum kwa wananchi kutathmini kama tunamtaka Muungwana.
Wanaoogopa Muungano usivunjike Ni wale ma mwinyi wa unguja ambao hawamtaki kufanya kazi, kwa CCM ndo chakula yao, wanategemea kulindwa na Bara ili waendelee kuishi bila kutoa jasho
 
Ccm wamekuwa wakiahidi kutatua kero za muungano miaka na miaka lakini kimya, hata hao wapinzani hawajaahidi kuuvunja bali wameahidi muungano wa manufaa kwa pande zote
Kweli kabisa mkuu
 
Hawawezi maana huu muungano tumeapa kuulinda mpaka kwa tone la mwisho la damu zetu
Peleka ujinga huko! Katiba yenyewe mmeshindwa kuilinda dhidi ya mshamba mmoja itakuwa muungano? Kwa taarifa yako Lissu na Seif ndio watakao jenga muungano huru na wa kisasa kabisa duniani.
 
Muda wa kubembelezana umekwisha ,msitupangie cha kuzungumza ,what the hell is muungano tutabadili hadi wimbo na bendera ya taifa
 
Msanii JF

Hii thread yako imekaa "kisanii" kwakuwa haina mashiko isipokuwa kasumba ya itikadi ya chama.

Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ni Muungano wa Chama na wanachama wa CCM tu, haukuwa na wala hauna ridhaa ya wananchi wa pande zote za muungano, Wananchi WENGI SANA wa upande mmoja wa huo muungano wanayo malalamiko kuhusu huo muungano, sasa katika hali hiyo ni ni cha kufanya??

kwa Ule upande wenye malalamiko ifanyike kura ya maoni juu ya Muungano uwepo au usiwepo, kama wengi watasema uwepo (jambo ambalo ni impossible), basi kifuatacho ni:- aina gani ya Muungano uundwe.

Kumbuka huo Muungano ni kitu kilichoundwa na binadamu wawili (nyerere na karume) hao SIO miungu, kilichoundwa na Mungu tu kinaweza kutobadilika kuendana na wakati na haja, hivyo tusifanye huo muungano kuwa ni sheria ya Mungu isiyohitaji marekebisho au kufutwa kabisa, kumbuka binadamu ni kiumbe dynamic ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kila uchao anapata maendeleo.

Tusiwe na mawazo mgando kuhusu huo Muungano, tuchukue hatua thabiti pale mshirika mmoja wa Muungano anapoona anadhulumiwa.

Mbona kuna nchi kadhaa zimevunja miungano yao "for the better".
 
Maagano gani ya kishirikina, ushirikina ni nn according to u? Je ukristo/ uislam si ushirikina? I thought u were smarter

Mimi siamini huo uislamu wala ukristo hali kadhalika, lakini bora huo ukristo na uislamu wangalau wanafanyia ibada zao hadharani, tofauti na hilo agano la kuchanganya udongo, lisilo na maelezo ya kina.
 
Maelezo ya kina utayajuaje ilhali unaudespise muungano, hata ukiyajua yatakubadilisha? Unaichukia ccm to the level you just want everything else to fail without even knowing, maelezo ya kina. Nmegundua upinzani too much unakinga reasoning.
 
Uwepo usiwepo nothing special, labda uniambie nini haswa umuhimu wake.
Uwepo usiwepo Nothing special, duuh, hata nikikwambia umuhimu wake, kwako utabaki, nothing special.
Yani hata ile common sense ya kujua umuhimu wa muungano, haipo.
Thought u were smarter, baki na fikra zako, ila October kibaraka wenu anapigwa chini tena, na muungano utabaki intact, mpende msipende.
 
Muungano hauna faida kwa sasa. Sanasana unawachelewesha Wazanzibari wasipige hatua kuchumi. Tunaweza kuitisha referendum ili kupata ukweli
 
Lissu yupo Zanzibar kusaka kura za urais wa Jamhuri.

Nimeanza na dibaji hiyo kwa minajili ya kusema yafuatayo:

1. Katika kunadi sera zake na ahadi za mgombea wa Urais hajawahi kuzungumzia namna atakavyolinda na kuuenzi Muungano ulioasisiwa na mababa wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.

2. Akiwa Bungeni, Mhe. Lissu aliwahi kuzungumzia Muungano akionyesha kutoukubali na utayari wa kuuvunja.

3. CHADEMA katika harakati zake inakwepa kujadili Muungano wetu.

4. Hawajaweka mgombea wa urais wa Zanzibar na wametangaza kumuunga mkono Maalim Seif ambaye siku zote amekuwa akidai Muungano hauna manufaa na akiupata urais wa Zanzibar atavunja Muingano huo.

Hivyo, endapo Lissu atashinda Bara na Maalim akashinda visiwani basi meza ya muungano itapinduliwa kirahisi kifuta historia tukuka ya Muungano na mshikamano wa kitaifa.

5. CHADEMA haikutangaza awali kumuunga mkono Maalim Seif hapo awali lakini baada ya Seif kuhamasisha wafuasi wake kubeba majambia, mashoka na mundu ili kuleta machafuko, hatua hiyo imeipelekea CHADEMA kuona wamepata mshirika anayeendana na malengo yao.

Ikumbukwe CHADEMA ilipozindua kampeni zake pale Zakhiem ilitangaza maandamano ya nchi mzima kipindi hiki kwa minajili ya kushinikiza hoja zao na kuleta machafuko nchini.

Kwa sababu hii na nyinginezo inapelekea allegations za CHADEMA kujiandaa kuvunja Muungano wetu tukuka.

Hivyo, sisi wapigakura tunajua nini cha kufanya hapo Oktoba 28 ili kuulinda na kuuenzi Muungano wetu.

Msanii JF
Haya ni matumizi mabaya ya akili. Kuzungumzia kero za Muungano siyo kuivunja bali ni kutaka kuuimarisha na Lissu siye wa kwanza kuzisema hizo kero. Semeni tu mumezidiwa hoja na hamna majibu nanyi mumezoea kujibu hoja kwa risasi.
 
Lissu yupo Zanzibar kusaka kura za urais wa Jamhuri.

Nimeanza na dibaji hiyo kwa minajili ya kusema yafuatayo:

1. Katika kunadi sera zake na ahadi za mgombea wa Urais hajawahi kuzungumzia namna atakavyolinda na kuuenzi Muungano ulioasisiwa na mababa wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.

2. Akiwa Bungeni, Mhe. Lissu aliwahi kuzungumzia Muungano akionyesha kutoukubali na utayari wa kuuvunja.

3. CHADEMA katika harakati zake inakwepa kujadili Muungano wetu.

4. Hawajaweka mgombea wa urais wa Zanzibar na wametangaza kumuunga mkono Maalim Seif ambaye siku zote amekuwa akidai Muungano hauna manufaa na akiupata urais wa Zanzibar atavunja Muingano huo.

Hivyo, endapo Lissu atashinda Bara na Maalim akashinda visiwani basi meza ya muungano itapinduliwa kirahisi kifuta historia tukuka ya Muungano na mshikamano wa kitaifa.

5. CHADEMA haikutangaza awali kumuunga mkono Maalim Seif hapo awali lakini baada ya Seif kuhamasisha wafuasi wake kubeba majambia, mashoka na mundu ili kuleta machafuko, hatua hiyo imeipelekea CHADEMA kuona wamepata mshirika anayeendana na malengo yao.

Ikumbukwe CHADEMA ilipozindua kampeni zake pale Zakhiem ilitangaza maandamano ya nchi mzima kipindi hiki kwa minajili ya kushinikiza hoja zao na kuleta machafuko nchini.

Kwa sababu hii na nyinginezo inapelekea allegations za CHADEMA kujiandaa kuvunja Muungano wetu tukuka.

Hivyo, sisi wapigakura tunajua nini cha kufanya hapo Oktoba 28 ili kuulinda na kuuenzi Muungano wetu.

Msanii JF
Lissu hafai kuwa Rais kwa mstakabali wa taifa letu.
 
Uwepo usiwepo Nothing special, duuh, hata nikikwambia umuhimu wake, kwako utabaki, nothing special.
Yani hata ile common sense ya kujua umuhimu wa muungano, haipo.
Thought u were smarter, baki na fikra zako, ila October kibaraka wenu anapigwa chini tena, na muungano utabaki intact, mpende msipende.

Huna utetezi wowote wenye mashiko wa huo muungano, ndio maana unaleta porojo. Kuwepo utakuwepo lakini ni kwa shuruti sio kwa ridhaa ya wengi, haswa wazanzibari.

Hiyo October unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Huo muungano unatusaidia nini hasa. Turudi nyuma miaka sitini ambapo huo muungano haukukuwepo wananchi walikosa nini ambacho hawakuwa nacho hadi pale huu muungano ulipokuja.

Huu muungano ni usanii mtupu na hauna maana yoyote kwetu hata ukivunjika hatutakuwa tumepoteza chochote na sana sana tutapata unafuu tu. Sababu zilizopelekea kuundwa kwa huo muungano hazipo tena.
 
Huna utetezi wowote wenye mashiko wa huo muungano, ndio maana unaleta porojo. Kuwepo utakuwepo lakini ni kwa shuruti sio kwa ridhaa ya wengi, haswa wazanzibari.

Hiyo October unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Ujinga wa mtu mweusi, as if wazungu hawalaumiani kwenye chaguzi zao, you're just a brainwashed nyumbu.
 
Back
Top Bottom