Huku gridi ya taifa ipo ya kutosha kuunganishwa ni kugusa tu, huku ukitokea msiba wa mtu aliyeingiliwa na yule mdudu majonzi huwa ni mengi mno kwani hata waliodhani kuwa ni wazima wanaweza jijua afya zao baada ya chain ya mahusiano ya marehemu kuwekwa wazi na zile stori stori za msibani....unaweza jikuta umeunganishwa kupitia mnyororo wa watu wengine ambao kutokea kwa marehemu. Kwahiyo na ww unaweza jikuta ukiangua kilio kwa uchungu msibani Tena katikati ya watu ikiwa hata huna undugu Wala ukaribu wowote na marehemu huku waombolezaji wakijua uko na uchungu na marehemu kumbe ww uko na maumivu yako.