Yanayoendelea huko Ukraine na Russia nilifikiri ni mihemko na ujuaji mwingi tu wa wabongo.......kumbe ni kweli mzee mzima putin anakutana na wakati mgumu;
Vyombo vyote ninavyoangalia sasa, hata vile visivyo rafiki wa marekani, vinatangaza tu sasa kuyumba kwa urusi.
Nikikumbuka jinsi dunia 'yetu sisi wengine' ilivyokuwa inamuogopa putin hadi akawa anaitwa 'the most powerful person in the world', nachoka kabisa.
Nikifikiria jinsi 'babu' Joe Biden alivyokuwa anaongea huku anasinzia kuhusu nini wanaenda kuifanyia Russia, nilikuwa nacheka tu kipindi kile kwa kudhani kuwa hawa marekani wameishiwa. Leo yanatimia yaleyale aliyoyaongea 'the sleepy' Joe.
Nikifikiria jinsi nchi za ulaya zilivyoamrishwa na marekani kukata mahusiano haraka na urusi nilishangaa sana kwanini zote zinafuata tu hata zile zinazoathirika moja kwa moja kwenye uchumi wake; kumbe walijua aisee nini kingewapata kama wangeenda against. Aisee tumwache tu mmarekani aitwe mmarekani!!
Nikiangalia yaliyomkuta macho madogo mchina, ya kupelekewa vifaa vya kijeshi barazani kwake huku akiwa anafokafoka tu asijue la kufanya, nimechoka. Ikumbukwe kuwa, kama ilivyo kwa mrusi, mchina nae alikuwa anatukuzwa mno humu.
Lakini kumbukumbu zangu kama ziko sawa, nakumbuka mwaka fulani kama sio 2001 basi 2002 marekani hii iliwahi kuiingia ndege yake ya kijeshi huko anga la China.
China akatuma ndege na yeye kwenda kuifukuzia, kilichotokea ziligongana zile ndege na ya China kuanguka huku askari wake kadhaa wakifariki huku ile ya marekani ikipata hitilafu na wakaishia kukamatwa.
Mgogoro ulikuwa mkubwa wa kutaka kuachiwa hao askari lakini mwishowe mchina aliufyata na kuwaachia hao makomandoo.
Walipokelewa kwa sherehe kubwa sana na Bush. Miaka 20 baadae leo, nilijua mchina ameshajidhatiti vya kutosha kuweza kumkabili mmarekani kumbe wapi!!! Tumwache tu mmarekani aitwe mmarekani!
Kwa hali hii, na kwakuwa huyu mtemi anahusudu na kupambania ndoa za jinsia moja; wadau jiandaeni tu kuolewa!!