Kwa hali hii ungekuwa wewe ndiyo mwenye nyumba ungeuza nyumba yako?

Kwa hali hii ungekuwa wewe ndiyo mwenye nyumba ungeuza nyumba yako?

Kuepuka usumbufu na madalali makubaliano yawe kwa asilimia ya bei ya kuuza. Milioni mbili ni asilimia 8 ya 25. Basi msingi wa makubaliano uwe huo. Kama watauza Milioni 50 wapate milioni 4.
Haiingii akilini dalali apate sawa na mwenye mali.
 
Kilichomkuta dalali yule hatokaa kunisahau nazan atawasimulia na wengine waboreshe mbinu... Hahaha nimecheka et mzee anatamaa wakati wao ndio wenye tamaa aisee pesa nyokoo
 
kanuni nzuri mtumie asilimia hayo mambo ya kutaja kiasi yalipitwa na wakati,

mfano kwenye dau la milioni 25 dalalo achukue 10% sawa na milioni 2.5, kwenye milioni 150 dalali apewe milioni 15
 
Kuna mzee mmoja hapa ubungo alitaka kuiuza nyumba yake kwa Bei ya tsh mil 25,wakapangana na madalali wawili ambapo madali watachukua mil 2 tu.

Sasa madalali wamempata mteja ambae alivoina nyumba akasema yeye atainunua kwa tsh mil150..madalali wakamuambia mzee sisi hio mil 2 usitupe.

Cha msingi wewe chukua chako ulichosema unakiuza mil125 tuachie... Sasa wapo wanaosema mzee kaleta tamaa je wewe ungechukua kinachokuhusu au ungevunja biashara?
Natafuta mtoto/ndugu aje pale afanye vurugu sana (akidai amepata taarifa nyumba inauzwa na hajashirikishwa) kisha anaenda chap mahakamani kufungua kesi kuwa nyumba ina mgogoro isiuzwe kwanza.
 
Madalali wajinga kweli kweli,hapo simple walikua wanatafuta Hela Wanampa mzee million 25,wao wanauza kwa Bei hiyo wanayotaka..

situation hiyo Ina maanisha kua nyumba Ina thamani zaidi ya aliyotaka mwenye nyumba...
 
Hapo jambo la msingi la kujiuliza ni huyo mzee alikuwa na ufahamu gani juu ya thamani ya nyumba yake anayouza?

Kama hajaridhia kuuza baada ya kusikia bei mpya then ni haki yake maana still kuna nafasi ya kunegotiate. Dalali hapo wanatakiwa kupata 20% ya hiyo milioni 150. Mwenye nyumba achukue 80% yake.
 
Back
Top Bottom