Chigwiyemisi
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 531
- 228
Kinachotokea kwa hivi sasa bungeni ni dalili za wazi za CCM kuaga uongozi wa Taifa hili. Kwanza kabisa wabunge wa CCM wameshindwa kabisa kufanya kazi yao ya kuisimamia serikali na badala yake wamejipachika jukumu la kuipongeza hata pale isipostahili pongezi. Wamekuwa ni mabingwa wa kupinga hoja zote hata zenye maslahi kwa taifa na wananchi wake ili mradi tu hoja hizo zimetolewa na wabunge wa upinzani hususani CDM. Wabunge wa CCM hawana kabisa uwezo wa kujenga hoja yoyote na kuisimamia isipokuwa kugonga meza na kuomba mwongozo wa spika/mwenyekiti. Wote kwa pamoja wakishirikiana na mawaziri wao wamekuwa wakijaribu kupooza hoja za wapinzani zenye nguvu na maslahi kwa Taifa kwa kutumia vijembe, kebehi na mipasho badala ya kujibu hoja hizo kwa hoja nyingine. Wanajaribu kutumia wingi wao bungeni kuwakandamiza wapinzani ili kuficha udhaifu wao na serikali yao. Hata mzee Sitta ambae kiasi fulani alijijengea heshima, kwa sasa imeshuka mno hasa baada ya kupewa nafasi ya kukaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Majibu aliyoyatoa Sitta dhidi ya Mh. Kafulila na kuwatukana wapinzani kuwa ni wanafiki yameonyesha unafiki mkubwa wa mzee huyu. Inawezekana vita yake haikuwa dhidi ya ufisadi bali "TATIZO NI UWAZIRI MKUU" ndio maana baada ya kukaimishwa pale mjengoni amelewa sifa za Ki-CCM! Spika, naibu wake na wenyeviti wa kamati wote wanapwaya katika nafasi zao kwa ushabiki na upendeleo wa wazi. Mbunge mmoja wa upinzani perfomance yake bungeni ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Lakini napenda kuwataarifu kuwa wananchi tunaona na tunapambanua mambo yote yanayoendelea bungeni! Na kwa hili nawatakia safari njema 2015!
Nawasilisha!
Nawasilisha!