Elections 2010 Kwa hali ilivyo Bungeni, CCM bye bye 2015!

Elections 2010 Kwa hali ilivyo Bungeni, CCM bye bye 2015!

Mimi niko huku "site" wakinamama hawaelewi kwa nini Serikali yao ipandishe bei ya mafuta ya taa tena kipindi ambacho hakuna umeme; kwa jinsi walivyolipokea hili nadhani CCM wasihangaike kuandaa khanga 2015 maana hawatazihitaji
 
Bye Bye ki vipi, kwani CHADEMA wameshajua jinsi ya kuzuia uwizi wa kura, wakina KIRAVU na species zao si bado wapo. Magamba wanawapenda sana CHADEMA kwa sababu kila ukiwaibia wanamuachia mungu.
 
Hali itakuwa mbaya sana na watu wanamuona SITTA kama ndio mnafiki mkubwa sana na pamoja na mambo yake yote ila naye ni vuvuzela katika kusimamia mambo muhimu sana katika Taifa hili
 
Mwisho wao umefka ndo maana hata hujibuji wao wa maswali haueleweki. Yaan hapo wapinzani wachache wanachanganyikiwa je wangekuwa nusu yao c pacngetosha. Kazen buti CDM hao ni waoga kama makunguru ya zenji. Ucwaogope hawana hoja hao zaidi ya kukimbilia kuwachafua wala msjali cc 2ko nyuma yenu.
 
Hivi wabunge wa ccm mie siwaelewi,!!!!!!! inamaana wote ni mawaziri maana wanajibu vitu vinavyohojiwa na wapinzani
kama vile wenyewe ni mawaziri au hawajui majukumu yao bungeni????
 
Wachakachuaji wakubwa sana hawa, kamwe hawatakubali kuachia madaraka kirahisi rahisi. Itabidi Watanzania nchi nzima tulale katika vituo vya kupigia kura na kuhesabia kura ili kuhakikisha hawapati nafasi ya kuchakachua hata kwa sekunde 1. Vinginevyo ni lazima watashinda tu 🙁

Hawa jamaa sijui tutawafanyaje!

Bila kulinda, kura zitachakachuliwa tuu!! Hata kama tukilala kituoni si unaona hata wana uwezo wa kupindisha matokeo kule kule wilayani wanakotangazia matokeo? Nashindwa kupata dawa ya hawa jamaa! Labda kuingia mitaani kwa nguvu zote? Mwanza waliweza lakini, labda hicho kitatusaidia.

Angalia pale Shinyanga wamepindisha matokeo kwa nguvu zao zote. Hawana hata aibu mbwa koko hawa!!
 
Bas na nyie hamfai kuongoza nchi ni wazembe mnakuwa wap mpaka mnaibiwa
Hawa jamaa sijui tutawafanyaje!Bila kulinda, kura zitachakachuliwa tuu!! Hata kama tukilala kituoni si unaona hata wana uwezo wa kupindisha matokeo kule kule wilayani wanakotangazia matokeo? Nashindwa kupata dawa ya hawa jamaa! Labda kuingia mitaani kwa nguvu zote? Mwanza waliweza lakini, labda hicho kitatusaidia.Angalia pale Shinyanga wamepindisha matokeo kwa nguvu zao zote. Hawana hata aibu mbwa koko hawa!!
 
Kinachotokea kwa hivi sasa bungeni ni dalili za wazi za CCM kuaga uongozi wa Taifa hili. Kwanza kabisa wabunge wa CCM wameshindwa kabisa kufanya kazi yao ya kuisimamia serikali na badala yake wamejipachika jukumu la kuipongeza hata pale isipostahili pongezi. Wamekuwa ni mabingwa wa kupinga hoja zote hata zenye maslahi kwa taifa na wananchi wake ili mradi tu hoja hizo zimetolewa na wabunge wa upinzani hususani CDM. Wabunge wa CCM hawana kabisa uwezo wa kujenga hoja yoyote na kuisimamia isipokuwa kugonga meza na kuomba mwongozo wa spika/mwenyekiti. Wote kwa pamoja wakishirikiana na mawaziri wao wamekuwa wakijaribu kupooza hoja za wapinzani zenye nguvu na maslahi kwa Taifa kwa kutumia vijembe, kebehi na mipasho badala ya kujibu hoja hizo kwa hoja nyingine. Wanajaribu kutumia wingi wao bungeni kuwakandamiza wapinzani ili kuficha udhaifu wao na serikali yao. Hata mzee Sitta ambae kiasi fulani alijijengea heshima, kwa sasa imeshuka mno hasa baada ya kupewa nafasi ya kukaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Majibu aliyoyatoa Sitta dhidi ya Mh. Kafulila na kuwatukana wapinzani kuwa ni wanafiki yameonyesha unafiki mkubwa wa mzee huyu. Inawezekana vita yake haikuwa dhidi ya ufisadi bali "TATIZO NI UWAZIRI MKUU" ndio maana baada ya kukaimishwa pale mjengoni amelewa sifa za Ki-CCM! Spika, naibu wake na wenyeviti wa kamati wote wanapwaya katika nafasi zao kwa ushabiki na upendeleo wa wazi. Mbunge mmoja wa upinzani perfomance yake bungeni ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Lakini napenda kuwataarifu kuwa wananchi tunaona na tunapambanua mambo yote yanayoendelea bungeni! Na kwa hili nawatakia safari njema 2015!
Nawasilisha!

Kaka kuongea sio kufanya kazi, Magwanda wenzio kazi yao ni kuongea tu na si kufanya kazi.
 
Wachakachuaji wakubwa sana hawa, kamwe hawatakubali kuachia madaraka kirahisi rahisi. Itabidi Watanzania nchi nzima tulale katika vituo vya kupigia kura na kuhesabia kura ili kuhakikisha hawapati nafasi ya kuchakachua hata kwa sekunde 1. Vinginevyo ni lazima watashinda tu 🙁

Hawa wetu kwani kilichotokea 2010 kimetufumbua macho we subiria tu hiyo 2015!!
 
Ni nani ambaye hakuona kile kiganja kilitokea makao makuu ya CC Magamba na Ikulu kwa jaa la kaya kikiandika hivi "MENEMENE TEKELI NA PERESI. Ufalme wa JK na magamba tayari umefitinika. Dalili za kufitinika kama vitabu vitakatifu vilivyoandika ni kugombana wenyewe kwa wenyewe, kugawanyika katika mapande ya kimtandao. Na kikwete aliingia na hilo pepo.
thats it. Ufalme umefitinika na soon lile joka kuu yaani chechemee litatupwa gizani! Cant wait to see the day bendera ya magamba ikishuka na ile ya HAKI ikipandishwa!!
 
KIFO CHAMA CHA MAGAMBA- EEH MUNGU NASHUKURU KWA KUSIKIA KILIO CHANGU Amen
 
Back
Top Bottom