Mkuu usipo jihusisha na harakati za kichawa utakuja kuwa bonge la kiongozi , kwa sababu tu ni muelewa na hauna ego za kijinga .
Gentleman,
Bila Neema na Baraka za Mungu ni vigumu kudumu kwa uhakika, amani, utulivu na upendo mahali Fulani popote ulipo, iwe kazini, masomoni, michezoni, siasani, uongozini na mahali pengine kokote...
nikuhakikishie tu,
binafsi kwa kudra za Mungu mpaka hapa nilipo ni bonge la kiongozi 🤣
kwasababu isingekua hivyo, mwanainchi gani angeniskiza, msomi gani angenisoma hata humu JF tu, nani angethubutu kufollow account yangu na kunicheck inbox kwa mashauriano, urafiki na salamu?
kwa Imani yangu kwa Mungu, uelewa na ufahamu wangu kidogo mathalani kuhusu siasa na uongozi sina hakika kama kuna ninae muona adui, ispokua labda yeye huyo mwanasiasa mwingine ndio anione mimi adui yake....
binafsi naamini,
siasa ni ushindani tu wa mawazo, fikra mipango, mbinu, ubunifu bora zaidi ya mwingine, wa kuleta au kuchochewa, mageuzi au mabadiliko chanya ya kijamii kisiasa na kiuchumi miongoni mwa jamii fulani...
na duniani, uchaguzi huamua nani au yupi kupitia ilani na sera kua ni bora zaidi ya mwingine...
so,
kwa siasa za Tanzania sijamuona adui yangu bado, bali namuona mshindani ambae pia ni ndugu, jirani, jamaa, rafiki, baba na mama yangu.
afanye siasa zake kwa uhuru nami zangu kwa amani lakini mwisho wa siku udugu wetu uwe Imara zaidi kati hali zote za shida na raha....
nimeeleza kwa kirefu hivi, ili kuondoa hofu na huenda kama kuna sintofahamu au utata dhidi ya siasa na hoja zangu kisiasa humu ndani 🐒