Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,926
- 4,110
Miaka ya karibuni kumeibuka kasumba ya wazazi wengi kupeleka watoto shule za mchepuo wa Kiingereza sababu ikiwa ni kuwafanya watoto waweze kuzungumza Kiingereza vizuri. Ada ya mtoto wa chekechea ni zaidi ya ada ya chuo kikuu. Najiuliza kwa hali hii ya maisha ilivyo sasa kwa nini kutumia gharama kubwa ya fedha ili kujua Kiingereza?
Nikiangalia watu wengi wenye nguvu kisiasa, na kiuchumi katika Taifa hili wamesoma shule za kawaida tu yaani "Saint Kayumba". Lakini ndio hao ambao taifa linawategemea kwa kiasi kikubwa. Tukianza na Rais wa sasa Mama Samia, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Mzee Warioba, Mzee Mwinyi, kina Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Sugu, (bila kujali mgogoro wao na Chadema) kwa uchache.
Njoo wasanii wa mziki Diamond, Konde Boy, Kanumba R.I.P, Rayvanny na wengineo.
Nadhani muhimu ni kuwekeza kuwafundisha watoto kujua vizuri utamaduni na lugha yetu, wajue ufugaji na kilimo bora,ufundi na sanaa, inayoendana na utamaduni wetu. Maana mwisho siku wataenda kuishi na kujitaftia liziki kwenye jamii hiyo hiyo.
Msanii wa Tanzania hawezi kutunga mashairi mazuri ya wimbo wa mapenzi kwa lugha ya Kiingereza kuliko Mwingereza mwenyewe au Mchekeshaji (Joti) akawachekesha wazungu kwa Kiingereza kwa kiwango cha kina Eddie Murphy, haiwezi tokea.
Katika jamii yetu ambayo ndiko tunakoishia kufanya kazi lugha inayotumika ni Kiswahili. Nenda halmashauri, hospitali, Sokoni na vijijini kote ni Kiswahili, sa kwanini kutumia gharama kwa kitu kisicho na uhitaji (Useless)! After speaking English then so what? Je, Kiingereza kinalima shamba au Kiingereza kinaleta chakula mezani?
Fursa nyingi za ajira zilizopo mtaani ni Bodaboda, Mama lishe, kuuza matunda, biashara za kutembeza, na zinazoendana na hizo. Fursa za ajira zinazotaka mtu ajue Kiingereza hazipo na ikitokea zikawepo ndo hizo ambazo nafasi 2 wanaomba watu elfu 20.
Kwa mtazamo wangu kumpeleka mtoto shule za Kiingereza ni kumuandaa mtoto kuwa mtazamaji mzuri wa tamthilia au kuwa mshiriki wa mashindano ya urembo na mitindo. Lakini sio kumwandaa mtoto kupambana na mfumo wa maisha ya sasa yanayohitaji kujichanganya. Kazi za "White collar Jobs" siku hizi hazipo. Ofisi zimejaa na hazihitaji watu, Field zenyewe ni shida. Kwanini tunatengeneza tatizo la kujitakia?
Nawasilisha.
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app