Kwa hali ya TRA ya sasa wamekuwa kama mchwa watakavyoniandama

Heron

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2013
Posts
1,946
Reaction score
1,800
Kuna Kabiashara kadogo nataka kukaanzisha, lakini kutokana na usumbufu wa TRA kwasasa,je naweza kuwafuata nikawaomba japo miezi 6 kisha ndio nianze kulipia?
Kwa hali ya TRA ya sasa wamekuwa kama mchwa watakavyoniandama.
Msaada tafadhal
 
mbuzi unaenda kwa muuza supu.......acha uoga Fanya tu biashara, mpaka ukigumiana nao, mnayajenga tu........kama mmiliki wa makampuni ya mafuta wezi wa kodi, sembuse were muuza perfumu
 
Kama mtaji wako mkubwa onana nao TRA usije ukaotewa wakakufilisi, kama unanjunga pambana kimya kimya
 
1. Ungeifafanua vema biashara hiyo unayotaka kuanzisha
2. Kama biashara yako hiyo unayotarajia itakuwa na mauzo zaidi ya mil 4 utawajibika kulipa kodi.
3. Fika ofisi za TRA zilizo karibu nawe upate mwongozo na ushauri mzuri zaidi juu ya kulipa au kutolipa kodi nk nk
4. Laah tumia washauri wa kodi kukupa mwongozo sahihi juu ya masuala haya ya kodi.
Kujificha kutokulipa au kukwepa kodi kwa makusudi au kwa kutokujua ni hatari kwa ustawi wa biashara yako.
Kuna Kabiashara kadogo nataka kukaanzisha, lakini kutokana na usumbufu wa TRA kwasasa,je naweza kuwafuata nikawaomba japo miezi 6 kisha ndio nianze kulipia?
Kwa hali ya TRA ya sasa wamekuwa kama mchwa watakavyoniandama.
Msaada tafadhal
 
Kuna Kabiashara kadogo nataka kukaanzisha, lakini kutokana na usumbufu wa TRA kwasasa,je naweza kuwafuata nikawaomba japo miezi 6 kisha ndio nianze kulipia?
Kwa hali ya TRA ya sasa wamekuwa kama mchwa watakavyoniandama.
Msaada tafadhal
Kuna kitu inaitwa tax holiday na ipo kisheria kwa kila biashara mpya japo TRA hawapendi kuizungumzia!
 
We fanya biashara bana,hii nchi ni huru,wakikukuta ongea nao vizuri tu,aafu uache kuvaa singlet...
 
Shukran sana nitalifanyia kazi panapo uhai soon
 
mbuzi unaenda kwa muuza supu.......acha uoga Fanya tu biashara, mpaka ukigumiana nao, mnayajenga tu........kama mmiliki wa makampuni ya mafuta wezi wa kodi, sembuse were muuza perfumu
Pamoja Mkuu
 
Nilifungua saloni kijijini,nikajipeleka mwenyewe TRA hatari,kasalon kenyewe mtaji haufiki m 2.jamaa walinikamua 150k. mwaka huu nimechukua kitambulisho cha magufuli.Ingawa pia lengo lilikuwa kupata leseni na TIN number.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…